Kwenye Umeme ni Usanii Mtupu

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Taarifa ya Msigwa ni kwamba TANESCO wanazalisha megawat 1,609. Matumizi yetu ni megawat 1,273. Hivyo tuna ziada ya megawati 336.

Tunaambiwa kuwa ukame umesababisha kupungua megawati 280!

Hii ina maana umeme uliopungua kutokana na unaotajwa kuwa ni ukame, haumalizi hata ile ziada ya umeme uliokuwa ukizalishwa.

NI KWA NINI TUNA SHIDA YA UMEME WAKATI KUNA ZIADA?

Hii nchi, kuna watu wamefanya Watanzania wote kuwa ni punguani.

Watanzania tubadilike, upole wetu sasa umegeuzwa kuwa ni uwendawazimu. Watu wachache wanatuchezea kwa kadiri watakavyo kwa vile wamewaona watanzania ni punguani.

Watanzania ni lazima tuungane kudai mfumo utakaotuhakikishia yafuatayo:

1) Tunaongozwa na watu ambao ni intelligent na waadilifu kwa kauki na matendo. Ukiwa na kiongozi dull atawateua dulls wenzake kwenye ngazi zote. Hakuna kitakachoenda. Tutaendelea kuwa mkia badala ya kuwa kichwa.

2) Wanaotuongoza ni lazima wakati wote watuongoze kwenye ukweli, na siyo kwa uongozi wa kilaghai na hila.

3) Tuwe na sheria inayompa haki mwananchi kumshtaki kiongozi yeyote kwenye ngazi yeyote anayetoa taarifa za uwongo, kuhadaa wananchi au kuwalaghai. Na kiongozi atakayethibitika kuwa ametenda makosa hayo, adhabu yake iwe jela bila ya nafuu nyingine yoyote, na akishahukumiwa hivyo, iwe mwisho wa kuwa kiongozi, na asiruhusiwe kuomba uongozi kwenye ngazi yoyote ile maisha yake yote.

4) Kusiwepo na kiongozi yeyote ambaye hairuhusiwi kushtakiwa.
 
Hizo takwimu ni za ki-JPM, si unajua alisema hakuna korona Tanzania na ikasemwa hivyo na viongozi wote wa serikali?
 
Back
Top Bottom