Kwenye sakata la mchanga wa dhahabu, nafahamu ukweli wa ndani

Ya nini kusafisha mchanga, wajenge kiwanda waondoke na finished products. Hiyo ndio muhimu. kuwe na asilimia 0.02 au zaidi wachukue hiyo mchanga watuachie. Maana mchanga unaobaki nao ni muhimu kwetu, mimea itaota, mazingira yatakuwa safi. wsitutendenezee machimo marefu kwa kwenda na mchnaga japani, ujerumani, n.k
 
...

Wizi upo lakini sio katika kuweka dhahabu kwenye makontena.

Kama swala nikukataza kusafirisha unrefined dhahabu, basi hata geita wapigwe marufuku kwani gold bar yao sio 100% pure.

Ni mapema mno kuanza kusema kuna nini katika hayo makontena! Hata vile siyo vizuri kupuuza kiwango cha 0.02% cha dhahabu kwa tani ya mchanga, mbali na madini mengine yaliyomo. Hicho kiwango ni 20gm kwa tani ya mchanga x uzito wa ujazo wa kontena moja x kontena zinazosafirishwa kila mwaka.
 
Naomba ni declare interest kuwa, mimi ni mmoja wa wataalam wanaouhusika na ishu iyo ya mchanga.

Kifupi naomba nieleze kile ambacho kipo kwenye makontena. Kilichopo kwenye makontena kwa asilimia kubwa ni copper(Cu) , ifufuatiwa na silver (Ag) na dhahabu (Au) haizidi asilimia 0.05.

Yule Afisa wa Bandari aliyesema kuwa zaidi ya asilimia 90 ni dhahabu ni muongo na anapaswa kuiomba radhi ACACIA na watanzania kwa ujumla na atumbuliwe kwenye nafasi yake.

Kiwango kilichopo kwenye yale makontena zaidi ya 256 ni kati ya sililimia 0.012 -0.02, g/t

Mh spika alidhani kiwango cha asilimia 0.02 kuwa ni kidogo na hauwezi kupata faida iwapo utalisafirisha kontena kutoka mgodini mpaka China, Japan au Ujerumani.
Naomba nimuulize, anajua gharama ya kusafirisha hilo kontena? Kifupi haizidi milioni 8.

Nikija kwenye mchanganua wa hiyo asilimia 0.02 kwa contena, naomba nimfafanulie mh spika kama ifuatavyo:-

(1) 0.02% hii ni gram kwa tani, kwa maana hiyo hii ukiizidisha kwa tannage zilizopo (eg 20.5tn), utapata 0.41%.
(2) Hii 0.41 ili upate ppm, unatakiwa uizidishwa kwa 10000, utapata 4100ppm au g/t.
kwa maana nyingine, yule mtaalam wa TMAA aliwaambia kwenye kila container kuna takriban kilo 4.1. sasa hii ni ndogo?
(3) Kwa sasa kilo ya dhahabu ni takribani mil 90. 90x4=36m.
sasa iwapo utasafirsha container moja kwa 10m, huoni kuna faida?

Pia Kamati ya Bunge kupitia Spika alidai kwa mwaka ACACIA, Buzwagi na Bulyanhulu huzalisha takribani idadi ya makontena elfu 50, na kwa maana hiyo contena milioni moja yameisha safirishwa. HUU SIO UKWELI.

Ukweli ni kwamba hizo ni tani za mchanga wa dhahabu na sio idadi ya kontena.

Mpaka sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wameisha safirisha makontena yasiozidi elfu 50.

Mpaka sasa Bulyanhulu peke yake wamesafirisha contena sizizozidi elfu 42. Sasa hizo contena 1m, zimetoka wapi?

Mh. rais kuna wanakupotosha, na hili utalithibitisha kupitia sample zilizochukuliwa na Mh Waziri Mkuu jana katika mgodi wa Buzwagi, kwani kati ya makontena aliyochukua sample, moja wapo ni kontena ambalo lililkua na seal na document zote za serikali na lilikua tayari kusafirishwa kwenda Ujerumani. Baada ya tamko la rais kontena hilo lilirudishwa mgodini pamoja na makontena mengine 3, yakiwa tayari yamefika Isaka.

My take:-

Kwenye hili sakata la mchanga, mihemuko isitumike. Wawekezaji wa ACACIA hawamuibii mtu kwani hata kama kungekua na 90% ya dhahabu, TMAA huchukua sample pia, kiasi kwamba wangeweza kuiambia serikali kuwa ACACIA wanawaibia kwa kutoa takwimu za uongo.

Iwapo mikataba haiwafaidishi watanzania, ifanyiwe review kwani ACACIA hutumia mikataba hiyo hiyo kufanya calculation zao.

Iwapo itathibitika kuwa ACACIA pia hawawaibii watanzania kwa kuficha dhahabu kwenye mchanga, basi pia Katibu Mkuu aombwe radhi.

90% ya dhahabu vs Nina uhakika 90%

Pambanua na u-edit post yako
 
Hahaha...! akili ya kuambiwa...! nimewasikiliza wataalam wa madini toka ACACIA wanadai mchanga ule hauna faida yoyote. SWALI: Kama hauna faida mnausafirisha wa nini?
 
Amesema ana uhakika 90% ya kilichopo kwenye mchanga kuna dhahabu,na sio ana uhakika 90% ya mchanga ni dhahabu

Huyo Eng. Kakoko kasema vyote viwili ulivyoandika!! Amedai kuwa asilimia 90 ni dhahabu na pia akadai kuwa anauhakika 90 % kuwa kuna dhahabu!!

Actually, kama ni uhakika kwamba kuna dhahabu kwenye mchanga basi ni 100 %. Ndiyo maana wanasafirisha mchanga nje!!
 
90% ya dhahabu vs Nina uhakika 90%

Pambanua na u-edit post yako
upload_2017-3-28_13-23-42.png
upload_2017-3-28_13-23-42.png

Soma hapo kwenye iyo blue katikati
 
Of course haileti maana hata kwa mtu mjinga kiasi gani kwamba vilivyo kuwa kwenye makontena 90% ni dhahabu. . . labda cjui alimaanisha nini kwa sentesi hiyo, ila kama maana ilikua ni kama sentesi ilivyo basi ni uongo.

Kwenye haya mambo ya viongozi kusema mambo ua ajabu ambayo hata mtu mwenye uelewa wa kawaida anaweza akashangaa kwa jinsi swala lilivyo na uongo wa dhahiri kuna Mawili
1. Wahusika huwa wanatoa taarifa potoshi makusudi . .
2. Viongozi huwa wanapewa taarifa sahihi ila kutokana na uelewa mdogo. . hasa unakuta kwenye swala husika wana likuza akilini mwao alafu wanatamka mambo ambayo sio sahihi. . . na kwenye hili hata waandishi wa habari na watu kwenye mitandao huwa wanabugi sana. Wanatoa taarifa kwa umma, taarifa ambayo yeye mwenyewe mzungumzaji au mwandishi hajaielewa, hajaifanyia utafiti hata kidogo, au kusoma soma juu ya swala husika angalau ajue kidogo juu ya swala husika. . .

Matokeo yake ndio kutoa, kutamka vitu vya ajabu ambavyo unayeelewa ukisikia unamshangaa anayoyasema

Eb imagine contena lenye 90% gold. Ivi jamaa anajua density ya dhahabu?
Mimi sio mtaalamu wa miamba na madini ila physics ya form 2 ninayo ikumbuka najua contena lenye dhahabu 90% ni zito sana sijui utalisafirisha kwa bara bara gani?
Waandishi wetu ni vimeo sana mkuu, nakuhakikishia asilimia 80% ya habari tunazosoma leo tunadanganywa sana, na kwasababu hatupendi kuchunguza inakuwa tabu tupu mitandaoni.
 
Ikena

Maelezo mazuri lakini subiri kuitwa majina kama wewe fisadi, mpiga dili, dalali n.k.

Hutajibiwa kwa hoja. Watu wameamua kufanya vitu kwa hisia.

Hii ni zaidi ya sukari.
 
Ikena

Maelezo mazuri lakini subiri kuitwa majina kama wewe fisadi, mpiga dili, dalali n.k.

Hutajibiwa kwa hoja. Watu wameamua kufanya vitu kwa hisia.

Hii ni zaidi ya sukari.
Tushazoea mkuu, si unakumbuka tulishaambiwaga fulani ni fisadi?
 
Vibaraka wa wazungu huwa hawaishi kuanzai ma chief mpaka leo wapo wanawatetea japokuwa wanahamisha rasilimali za nchi. Hata kama ni silver, iron au hata core kwa nini wasifanyie extraction hapa nchini? kipi rahisi kubaba furushi la makontena ya michanga kusaririsha au kuleta kontena moja tuu la mshine kuja kuifanyia kazi hiyo hapa nchini? waache kutudanganya !!!! tumechoka na hatudanganyiki tena
 
Wanachimba mchanga na kupeleka nje lakini wanadai hawapati faida, ni kwa hasara. Sasa Rais anakataza wanasema wanapata hasara.

Wakifanya hasara, wakiacha hasara. Huu ni utapeli.

Cha msingi sana ni hivi: kama Rais amekataza kusafirisha mchanga nje basi unaacha mara moja hata kama hakuna dhahabu.

Tumedharauliwa vya kutosha, tumenyonywa vya kutosha, ila sasa tuna Magufuli. Kitaeleweka tu.
 
Amesema ana uhakika 90% ya kilichopo kwenye mchanga kuna dhahabu,na sio ana uhakika 90% ya mchanga ni dhahabu
Lakini kuwepo kwa dhahabu kwenye huo mchanga hakuna anayekataa (hata hao accacia wenyewe). Suala ni dhahabu kiasi gani? Kwa hivyo hiyo asilimia 90 kama ilikusudiwa probability ya mchanga kuwa na dhahabu then sio relevant kwa sababu mabishano sio uwezekano wa mchanga kuwa na dhahabu bali ni kiwango cha dhahabu kilichomo kwenye huo mchanga.
 
Ikiwa yule dg wa bandari amempotesha raisi na asilimia 90 zake anazolazmisha naomba ashtakiwe kwa uhujumu uchumi maana atatia taifa hasara nyingi sana. Ila ngoja tuone
Nauliza kama lay person, huyu jamaa wa bandarini ana kifaa kweli cha ku determine sample za madini yote yanayokuwa kwenye mchanga au amelishwa maneno. Kama kuna findings why do they not put them on the sheets when they are transporting the sand? Hapa ni biashara siyo kuiba na kama container zinapita mchana kwa nini huyo aliyesema 90% asiamliwe afanye moderation ili tuone kweli alisema ukweli. Ukweli utatuweka huru daima. Tumeliwa sana na mikataba ya kiunyonyaji sawa ila kama wakubwa waliridhia basi hata mchanga nao tuone ukweli ila siyo kusingizia. Mungu nirehemu kuzaliwa nchi ambayo kila mtu ni mwanasiasa, Askari na judge isipokuwa waganga wapo wachache kama mbunge wa Tanga wapi sijui
 
Sasa bila kuwepo dhahabu kwanini wakachuje?

Wataalam wanasema ipo kwa kiwango kilichotajwa hapo juu kwenye post namba moja.
Kwenye thread za kitaalamu hapo ndipo ninapokuelewaga huwa unasimamia misingi ya kitaaluma na kuweka mbali mihemko ya kisiasa na ukada.

Ningefurahi sana kama watanzania wengi wangeiga mfano wako kwa kusimamia uchambuzi wa kitaalamu na kukipiga kikumbo propaganda za ukada.

Hii ni Tanzania yetu sote, na ukweli lazima usemwe, na ushauri makini lazima usemwe ili kujenga na kuliinua taifa.

Mimi binafsi naogopa sana kuchangia mada hii kwa sababu inahitaji mtu anayejua kweli biashara hii ya dhahabu kama mleta mada alivyofafanua. Lakini wengi wa makada wa chama cha mapinduzi wametawaliwa na propaga na undumila kuwili katika hili swala mpaka kupotosha maana nzima.

Nasubiri takwimu za kitaalamu wazilete, na pia nitalinganosha na nìnachostudy kwa sasa ili nisiropoke tu kama mwenda wazimu kuwa tunaibiwa kumbe hakuna chochote.
 
Tatizo mikataba inawaruhusu, na kuivunja itabidi awalipe maradufuvya thamani ya mchanga.

Biashara kichaa.

Kwa nini hakukataa mikataba hii awali? Alikuwepo serikalini ilipopitishwa
Wale walioserikalini kwasasa wanachangia nini kwenye mipango kazi?
 
Swala hapo ni kwamba tunaibiwa. Maana HAKUNA hata container moja lililotoka wakaja sema tume pata kiasi hiki baada ya kuchambua. Kwani coper, silver, na gold inayo kutwa umo siyo PESA. Tusitete ujinga tushaibiwa sana makontena mangapi yaisha pelekwa njee mpakaleo. Kama wameweza leta mitambo ya kuchimbia kwa nini wasilete mitambo ya kusafisha MCHANGA.
mkuu kama hujui vitu uliza,...data zote kuhusu huo mchanga unaosafirishwa nje na results zake huko china na japan vinapatikana wizara ya madini,no fact no right to speak
 
Watanzania bwana....huwezi ukasafirisha mawe ya dhahabu barabarani.

Mwaka 2007 mwanzoni kuliibuka wizi wa huo mchanga wa dhahabu, madereva wa kampuni iliyopewa tenda ya kuuleta Dar walicheza dili na wafanyabiashara wa huko Kahama na kuanza kuuiba huku wakiweka mchanga wa kawaida kwenye nafasi ya ule wa dhahabu (makinikia).

Walikamatwa madereva wote baada ya polisi wa bulyanhulu kuja pale MOFED na kuyafungua baadhi ya makontena. Lakini kesi ile ilizimwa nadhani kwa maombi ya matajiri wenyewe huko nje.

Tunapenda sana kuongopeana na uongo unakuwa ndio ukweli, huwezi kusafirisha mawe ya dhahabu kwa trucks, ikiwa huu mchanga watu waliweza kuchora mchoro wa kuuiba sembuse mawe ambayo ni bei mbaya sana!.

Tumepigwa kwa miaka mingi, lakini kama wasemavyo wataalam wa madini, uwezo wetu wa kufaidika moja kwa moja na utajiri huu sio suala la mijadala kama ile ya udaku, tunatakiwa kujipanga katika hali ya umakini wa hali ya juu.
 
Kwa hili upo sahihi. Ila viwango vya madini mengine, bado siwezi kuamini
Mimi nilicheki kupitia XRF zipo chini mfano ambapo ukiwa wewe target yako ni gold, inabidi upoteze AS,F,Bi,S etc[/QUOTE]
Tatizo raisi anakurupukaga kabla hajafanya uchunguzi...eti sasa hivi ndio kaunda tume zifanye uchunguzi..haya ngoja tuone natumaini hautanyongwa.

Hapo kwenye BOLD si kweli, kuna clip kabla hata hajagombea uraisi alisikika akilaani wizi huu na mwenzie akamtania kuwa kachukue fomu, yeye alisema hawezi kuchukua kwani watu watalimia meno, ilishawahi kuletwa hapa siku za nyuma.

Baada ya kuchaguliwa amekaa zaidi ya mwaka ndo ametoa agizo, lakini pia nilimwangalia wakati anafungua kiwanda cha marumaru (tiles) kule mkuranga baada ya kuambiwa kuwa wananyeyusha machanga/ mawe hadi centigrade 1000 kama sikosei ndipo aliposema amekuwa anaambiwa kuwa TZ hawawezi achieve hilo na ndipo akasema hakuna kusafirisha mchanga tena.
Hivyo tutoe "comment" zetu tukiwa tumeishafanya utafiti kidogo, hapa hakukurupuka kuna kitu.
 
Dhahabu ni nzito kuliko kopa,dhahabu ingekuwepo kwa asilimia hizo ingekuwa ngumu kuweza kuzisafirisha ikiwa imejaa kwenye kontena.
Kwanza inatia kinyaa unapomsikia mtu anayesema amesoma halafu anasema ndani ya container kuna 90% dhahabu. Huyu ina maana hana hata elementary chemistry ya periodic table! Anajua specific gravity ya gold? Almost 10 times water. Container liwe 90% gold anajua uzito wake utakuwa ni kiasi gani? Ni lorry gani la kubeba uzito wa namna hiyo?

Ningekuwa Rais, halafu mtu anasema hayo, ni wa kufukuza mara moja maana inaonekana hana elimu, ni mjinga wa kudumu na hana reasoning.
 
Back
Top Bottom