Kwenye makampuni kuna CSR, kwenye vyama kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye makampuni kuna CSR, kwenye vyama kuna nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjenda Chilo, Jun 11, 2012.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Corporate Social Responsibility (CSR) I
  limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa makampuni ili kulipa fadhila kwa wananchi baada ya kutengeneza faida, hata kama ni kidogo lkn tumeshuhudia vodacom wakigawa madawati, airtel wakigawa vitabu, barrick wakijenga shule nk. Tunajua lengo la vyama ni kushika dola na hatimae kutuongoza tukitegemea watuletee maendeleo huku tukijua wazi washika madaraka wananufaika kwa vyeo na marupurupu kibao manono. Swali langu ni je kuna umuhimu gani kwa chama tawala ambacho kinatakiwa kutuonyesha tangible outputs kipoteze mahela mengi kwa kukodi mabasi kwenda kuwaambia watu wamefanya nini ni kupoteza muda na kutokuwa na vision au ni kutapatapa tu? hayo mambo wawaachie upinzani bwana. Imagine wangefanya kaproject kakujenga hata shule ya chama nzuri wakakusanya watoto maskini kila kona wakawapa elimu ya bure wale wanufaika hata kama ni wachache hebu angalia impact yake, watu wa masoko wanaita a good word of mouth(WOM). Huu usanii wanaofanya watu wanaujua na wanaohudhuria ni wale tu wanaonufaika na viposho, mbaya zaidi ambacho hawakijui wanafanya uchaguzi wanawapa nafasi vijana ambao wanajua lazima watapiga hela due to current state of politics bila kujua vijana hao moyoni ni CDM. Ccm na vichwa vyao vyote wameshindwa kuteua idara ya uenezi competent na yenye vision ktk kipindi muhimu sana kwao. Tusubiri tuone!
   
Loading...