Kwenye hili CUF wanalo la kujifunza

Kwenye hili CUF wanalo la kujifunza

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
1,154
Reaction score
118
Juzi nchini Uingereza ulifanyika uchaguzi wa kuchagua councillors na wawakilishi wengine. Uchaguzi ule kwangu mie unaweza kuwa ni mfano wa ndoa kati ya CUF na CCM kule Zenji ingawa kwa huko Uingereza ni ndoa kati ya Conservative na Liberal democrats.
Katika uchaguzi ule, chama cha liberal D kimefanya vibaya saana na hii inaaminika ni kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na torries na hivyo kufanya kinyume na yale ambayo wanachama wake walitarajia. Wengine wanasema kimekuwa ni kama light conservative na wengine wanasema kujiunga kule kumefanywa kimezwe na kisionekane kabisa.
Kama ilivyo hapa Tanzania, uamuzi wa CUF kuwa na CCM ulikuwa ni wa msingi kwasababu ya kuondoa uezekano wa uvunjifu wa amani. Lakini basi, ufike wakati tuheshimu kukubali matokeo na kuwapa haki walioshinda hata kama hatupendi hivyo. Maana hii tabia ya serikali za umoja zinaondoa changamoto kwa serikali na hatimaye wananchi wanakosa uwakilishi waliokuwa wanahitaji.
Pia CUF kuna haja ya kuiangalia hiyo ndoa maana ni ndoa ambayo haiaminiki na inakifuta chama hicho taratibu kwa upande wa Bara.
 
Usitie shaka, ndoa ni ya wawili na wawili hao wanasema wanaaminiana. Tuwape muda; atayeshindwa atatafuta mlango wa kutokea.
Natumai wamekusoma
 
Changamoto haziletwi na CUF peke yake kwani naona imekataa tamaa. Tunahitaji vyama vyenye uvumilivu na kusimamia malengo yake milele. Kwa hiyo usihofu, chama cha kuleta changamoto za kweli kipo tu na wala si CUF.
 
Juzi nchini Uingereza ulifanyika uchaguzi wa kuchagua councillors na wawakilishi wengine. Uchaguzi ule kwangu mie unaweza kuwa ni mfano wa ndoa kati ya CUF na CCM kule Zenji ingawa kwa huko Uingereza ni ndoa kati ya Conservative na Liberal democrats.
Katika uchaguzi ule, chama cha liberal D kimefanya vibaya saana na hii inaaminika ni kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na torries na hivyo kufanya kinyume na yale ambayo wanachama wake walitarajia. Wengine wanasema kimekuwa ni kama light conservative na wengine wanasema kujiunga kule kumefanywa kimezwe na kisionekane kabisa.
Kama ilivyo hapa Tanzania, uamuzi wa CUF kuwa na CCM ulikuwa ni wa msingi kwasababu ya kuondoa uezekano wa uvunjifu wa amani. Lakini basi, ufike wakati tuheshimu kukubali matokeo na kuwapa haki walioshinda hata kama hatupendi hivyo. Maana hii tabia ya serikali za umoja zinaondoa changamoto kwa serikali na hatimaye wananchi wanakosa uwakilishi waliokuwa wanahitaji.
Pia CUF kuna haja ya kuiangalia hiyo ndoa maana ni ndoa ambayo haiaminiki na inakifuta chama hicho taratibu kwa upande wa Bara.
Mkuu umezungumza mambo ya msingi sana ila naona kama umechelewa, nafikiri walishauriwa mapema hatari iliyoko mbele yao nao wakaiona hii ndio njia bora matokeo ndio haya. Binafsi siwezi kuja kuiamini tena CUF, kwa sababu isitegemee support ya wananchi wakati wao ni wabia wa wanaoiendesha nchi. Tutatofautishaje kati ya chama tawala na Cuf hivi sasa, kama ulivyosema kwa huku bara kazi wanayo hasa wanavyozidi kuwasakama wapinzani wenzeo ndio kwetu tunaona ni watawala wenza kweli.
 
Tuendelee kusema na tusichoke kusema huenda ikasaidia. Wahakikishe ndoa ile inaukomo. Yaani lazima iwe na ya mkataba na lazima wajipambanue na yale mambo wasiyoyakubali. Wakiendelea na mchezo wa kukubali kitu, hali yao itakuwa hoi zaidi. Maana sasa hivi wanaonekana kama rubber stamp. Lazima ifike wakati wawakilishe hoja zenye kuipinga serikali pale inapofanya hivyo na si kuhofia serikali ya kule Zenji. Wakati ni sasa, watafute strategies na wajitofautishe vinginevyo waombe tu bila haya kuwa chama kiondolewe kwenye usajili.
 
Well said!

Kwenye hii marriage hakuna chochote Conservative walicho compromise in terms of election manifesto policies.Lib Dems become a lame duck kwenye hii marriage kila policy wamefuata za Tory-tution fee , spending cuts,AV systems e.t.c?

Je, Cuf supporters watakumbuka siku ya kupiga kura,their leaders decided to do it for themselves?

Kuna wapiga kura wengi hata hapa jukwaani ukiwauliza sera za uchaguzi za vyama vyao sasa hivi hawakumbuki,kwa sababu wapo busy na 2015 to repeat the same mistake.
 
Juzi nchini Uingereza ulifanyika uchaguzi wa kuchagua councillors na wawakilishi wengine. Uchaguzi ule kwangu mie unaweza kuwa ni mfano wa ndoa kati ya CUF na CCM kule Zenji ingawa kwa huko Uingereza ni ndoa kati ya Conservative na Liberal democrats.
Katika uchaguzi ule, chama cha liberal D kimefanya vibaya saana na hii inaaminika ni kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na torries na hivyo kufanya kinyume na yale ambayo wanachama wake walitarajia. Wengine wanasema kimekuwa ni kama light conservative na wengine wanasema kujiunga kule kumefanywa kimezwe na kisionekane kabisa.
Kama ilivyo hapa Tanzania, uamuzi wa CUF kuwa na CCM ulikuwa ni wa msingi kwasababu ya kuondoa uezekano wa uvunjifu wa amani. Lakini basi, ufike wakati tuheshimu kukubali matokeo na kuwapa haki walioshinda hata kama hatupendi hivyo. Maana hii tabia ya serikali za umoja zinaondoa changamoto kwa serikali na hatimaye wananchi wanakosa uwakilishi waliokuwa wanahitaji.
Pia CUF kuna haja ya kuiangalia hiyo ndoa maana ni ndoa ambayo haiaminiki na inakifuta chama hicho taratibu kwa upande wa Bara.

Mkuu haya ni maneno ya kuzingatiwa sana katika harakati za siasa Tanzania. Mkuu hii imekaa vyema, big up!!!!!
 
Tehetehe .... Nimefurahia maoni ya wachangiaji humu. Na naamini ni mawazo mgando haya ya humu kijiweni viongozi wa CDM waliyachukua na kufanya sera rasmi za chama! Inaelelekea maelewano ya CUF na CCM Zanzibar yanawakera sana!Lakini mbona US issue ikiwa na bipartisan agreement ndio inakuwa best? kwa nini hapa mnataka kusiwe na concesus juu ya swala lolote? Matokeo yake wale wenye misimamo ya kihuni na vurugu ndani ya CDM sasa ndio wanakuwa flag bearers! Wale wenye maono ya mbali na ukomavu wa kisiasa wanaonekana wasaliti! CDM is nearing its demise!
 
Juzi nchini Uingereza ulifanyika uchaguzi wa kuchagua councillors na wawakilishi wengine. Uchaguzi ule kwangu mie unaweza kuwa ni mfano wa ndoa kati ya CUF na CCM kule Zenji ingawa kwa huko Uingereza ni ndoa kati ya Conservative na Liberal democrats.
Katika uchaguzi ule, chama cha liberal D kimefanya vibaya saana na hii inaaminika ni kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na torries na hivyo kufanya kinyume na yale ambayo wanachama wake walitarajia. Wengine wanasema kimekuwa ni kama light conservative na wengine wanasema kujiunga kule kumefanywa kimezwe na kisionekane kabisa.
Kama ilivyo hapa Tanzania, uamuzi wa CUF kuwa na CCM ulikuwa ni wa msingi kwasababu ya kuondoa uezekano wa uvunjifu wa amani. Lakini basi, ufike wakati tuheshimu kukubali matokeo na kuwapa haki walioshinda hata kama hatupendi hivyo. Maana hii tabia ya serikali za umoja zinaondoa changamoto kwa serikali na hatimaye wananchi wanakosa uwakilishi waliokuwa wanahitaji.
Pia CUF kuna haja ya kuiangalia hiyo ndoa maana ni ndoa ambayo haiaminiki na inakifuta chama hicho taratibu kwa upande wa Bara.

Kweli mkuu tofauti ninayoiona kwa huku kwetu ni uwelewa wa wapiga kura lakini mwenye macho ya kurunzi cuf bara wamepoteza natabiri kifo chao baada ya next 2015 election.
 
Tehetehe .... Nimefurahia maoni ya wachangiaji humu. Na naamini ni mawazo mgando haya ya humu kijiweni viongozi wa CDM waliyachukua na kufanya sera rasmi za chama! Inaelelekea maelewano ya CUF na CCM Zanzibar yanawakera sana!Lakini mbona US issue ikiwa na bipartisan agreement ndio inakuwa best? kwa nini hapa mnataka kusiwe na concesus juu ya swala lolote? Matokeo yake wale wenye misimamo ya kihuni na vurugu ndani ya CDM sasa ndio wanakuwa flag bearers! Wale wenye maono ya mbali na ukomavu wa kisiasa wanaonekana wasaliti! CDM is nearing its demise!
Hapa haiongelewi CDM bali ni facts. Labda tukupe mfano mdogo huenda ukakusaidia. CUF wakati wanagombea walikuwa na election manifesto yao ambayo ilikuwa inawaelekeza nini watafanya endapo watashinda katika uchaguzi ule. Sasa hawakushinda, na walishinda CCM wao wakaingia kwenye ule mseto wenye lengo la kutekeleza sera za CCM maana CCM ndio washindi. Kwa mantiki hiyo CUF wanaendelea kusimamia sera za CCM tena kwa lazima wakubali hata kama hawataki maana wapo pia serikalini. Hali kama hii lazima ilete tafsiri kwa wapiga kura. Maana wamefifishwa CUF. Hawawezi kuongea tena hasa huko visiwani kama wapinzani. Wakati Bara wanaCUF wapo kwenye bumbuazi maana chama kimesahau kuwa nao wanawahitaji. Tena basi wapo kimya hawasikiki wanafanya nini zaidi ya kuonekana kwenye dhifa za Kitaifa. Unadhani bado kuna uhai hapo.
 
Tehetehe .... Nimefurahia maoni ya wachangiaji humu. Na naamini ni mawazo mgando haya ya humu kijiweni viongozi wa CDM waliyachukua na kufanya sera rasmi za chama! Inaelelekea maelewano ya CUF na CCM Zanzibar yanawakera sana!Lakini mbona US issue ikiwa na bipartisan agreement ndio inakuwa best? kwa nini hapa mnataka kusiwe na concesus juu ya swala lolote? Matokeo yake wale wenye misimamo ya kihuni na vurugu ndani ya CDM sasa ndio wanakuwa flag bearers! Wale wenye maono ya mbali na ukomavu wa kisiasa wanaonekana wasaliti! CDM is nearing its demise![/QUOTE]

Mkuu mbona unaongea kinyume chake. CUF ndio inayo karibia kufa!. Mwaka 2010 na 1995 Seif Shariff Hamad alishinda uchaguzi lakini hakupewa haki yake. Consensus ambayo ni one sided sio consensus, kama unakumbuka mwaka jana wakati CCM inahitimisha kampeni zake pale Jangwani Mkapa alisema katika utawala wake watu walikuwa wanamshutumu kwamba hataki serikali ya mseto Zanzibar, akasema sio kwamba alikuwa hataki bali alikuwa yupo tayari tu kuona serikali ya mseto inaongozwa na CCM na sio CUF. Sasa hapo kuna consensus kweli? Definately hapo hakuna Consensus ila CUF inaburuzwa. Pamoja na wanachama wao kukataa, viongozi wa CUF walikubali serikali ya umoja hatakama walishinda kwasababu ya uchu wao wa madaraka na hicho ndio kifo chao!. Viongozi wa CUF wamewasaliti wanachama wao na gharama za maisha ya watu waliuwawa January 26 2001 haziwezi kuwa justified na mwafaka huu wa upande mmoja.
 
CUF wamejipaka kinyesi cha CCM, kwa kukubali kuunda serikari ya mseto na chama ambacho tunasubili kukizika soon, hivyo CUF will definetly go down with ccm hamna jinsi, ndo maana wanatumia nguvu kubwa sana ndani ya bunge na nje ya bunge kuhakikisha wanawatetea na kusafisha kinyesi cha wanandoa wenzao, ni hiyo ndo wananchi wamewastukia kuwa hawa CUF ni watu wa maslahi tu! hilo jiti halichomoki, vyama vya siasa vilivyokomaa husubiri kwani subira huvuta kheri lakini maalimu Seif alitaka afaidi matunda ya kuwa makamo wa raisi asiekuwa na kazi wala mamlaka yoyote na kuwasaliti mashujaa waliopoteza maisha yao kupambana kuindoa ccm madarakani ili watoto wao wasifungwe nira na huyu mkoloni mweusi. Mshahara wa wasaliti ni mauti, hivyo CCM will pull down CUF to the grave haihitaji darubini kali kuling'amua hilo.
 
Tehetehe .... Nimefurahia maoni ya wachangiaji humu. Na naamini ni mawazo mgando haya ya humu kijiweni viongozi wa CDM waliyachukua na kufanya sera rasmi za chama! Inaelelekea maelewano ya CUF na CCM Zanzibar yanawakera sana!Lakini mbona US issue ikiwa na bipartisan agreement ndio inakuwa best? kwa nini hapa mnataka kusiwe na concesus juu ya swala lolote? Matokeo yake wale wenye misimamo ya kihuni na vurugu ndani ya CDM sasa ndio wanakuwa flag bearers! Wale wenye maono ya mbali na ukomavu wa kisiasa wanaonekana wasaliti! CDM is nearing its demise![/QUOTE]

Mkuu mbona unaongea kinyume chake. CUF ndio inayo karibia kufa!. Mwaka 2010 na 1995 Seif Shariff Hamad alishinda uchaguzi lakini hakupewa haki yake. Consensus ambayo ni one sided sio consensus, kama unakumbuka mwaka jana wakati CCM inahitimisha kampeni zake pale Jangwani Mkapa alisema katika utawala wake watu walikuwa wanamshutumu kwamba hataki serikali ya mseto Zanzibar, akasema sio kwamba alikuwa hataki bali alikuwa yupo tayari tu kuona serikali ya mseto inaongozwa na CCM na sio CUF. Sasa hapo kuna consensus kweli? Definately hapo hakuna Consensus ila CUF inaburuzwa. Pamoja na wanachama wao kukataa, viongozi wa CUF walikubali serikali ya umoja hatakama walishinda kwasababu ya uchu wao wa madaraka na hicho ndio kifo chao!. Viongozi wa CUF wamewasaliti wanachama wao na gharama za maisha ya watu waliuwawa January 26 2001 haziwezi kuwa justified na mwafaka huu wa upande mmoja.

Hapa Wakuu kidogo mmenichanganya na sijui namjibu nani kwa kweli. CUF imeshinda Chaguzi zote tangu 1995 na huu wa juzi ndio ilikuwa landslide mpaka jopo zima la Wakuu wa Serikali, JWTZ na Usalama wa Taifa wakateremka Zanzibar kufanya "mapinduzi" na kuinyima CUF ushindi wake halali. Hii ni open sectret. Viongozi wa CUF walikubali kuingia katika kile kilichokuja kujulikana kama "maridhiano" kwa kutaka kusalimisha roho za watu wake, jambo ambalo kwa hawa watawala wetu hawaoni kuwa ni jambo kubwa.

Viongozi kadhaa akiwamo BM na JK na JN kabla yao wamekuwa wakisema waziwazi kuwa watayalinda Mapinduzi kwa hali yoyote ile. Sisi wananchi, tunajua fika kuwa CCM, hawako tayari ku relinquish wala ku share power lakini kwa wakati ule hawakuwa na option nyengine. Mtakumbuka kuwa CUF walikuja kukataa kile kilichokuja kujulikana kama Azimio la Butiama kutokana na haya ambayo kwa sasa ilionekana kuwa ndio the only way out.

Walikuwa wapi CDM, tulipokuwa tunapigwa, tuna najisiwa watoto, wake, mama na dada zetu? Walikuwa wapi CDM tulipokuwa tunakimbia majumba yetu na kulala misituni na baadae kukimbilia Shimoni? Nadhani CDM waliiona joto ya jiwe kule Arusha. Hio ndio CCM, Chama Dola king'ang'anizi kinachotawala bila rihaa za wananchi.

Wananchi tunajua hasara ya hii GNU na ndio maana mpaka sasa Serikali ni kama iko liikizo. Kubwa walofanya ni kuteua Mawaziri 8 kutoka CUF na Watendaji 180 wenye Presidential appointment na bado wengine kama Wakuu wa Mikoa, Wilaya na wengine kadhaa hawajateuliwa. Hao waliokwisha kuteuliwa tu, wanatumia 1/3 ya wage bill.

Hali si nzuri bado lakini kwa mara ya kwanza, Uchaguzi huu hakufa mtu.CUF pia inajua kuwa katika politics, hakuna permanent friend wala permanent enemy lakini kuna permanent interest. CUF walichagua kusalimisha wananchi na mauaji ya kimbari ambayo hufanyika wakati na baada ya Uchaguzi tokea 1995.

Kwa hivyo pale mnapolaumu hii mnayoiita "ndoa", ni lazima mujue mazingira ya tukio hilo. Hapa chini nakutumia makala, ukipata nafasi someni. Pia nakuwekea picha chache uone namna CCM/SMZ/SMT inavyoshinda Uchaguzi na kuimarisha "muungano"

Hizi ni ID za raia wa Msumbiji alopewa kwao na akapewa na ya Zanzibar ili apige kura:

View attachment 29553

View attachment 29555

Hivi ndivyo Mapinduzi na Muungano unavyolindwa na CCM/SMZ/SMT:

View attachment 29556

View attachment 29557

Haya makala jisomee kwa wakati wako:

Na Mohammed Khelef Ghassany

Akiwa mjini Zanzibar tarehe 25 Januari mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa akiapa kwamba hatamvumilia yeyote anayeyachezea Mapinduzi. Kwa hakika hakikuwa kiapo tu, bali pia kilikuwa ni kitisho: "Kama mtu hajipendi, achezee Mapinduzi aone." Ilikuwa kauli nzito, lakini si ngeni kutoka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), hasa wanaotokea Tanganyika, na hilo ndilo shughuliko kuu la makala hii. Ninahoji kwa nini viongozi wa Tanganyika wawe wakali ‘kuyalinda' Mapinduzi ya Zanzibar!

Mimi ni kijana wa Kizanzibari na Mapinduzi yanayoapiwa kulindwa hapa ni yale ya Januari 12, 1964 ambayo yaliiondosha madarakani serikali ya mseto wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP). Zaidi ya asilimia 60 ya sisi Wazanzibari wa leo hatukuyaona Mapinduzi hayo. Sasa ninajiuliza, ikiwa Mapinduzi yenyewe ni hayo, kwa nini yamfanye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ale kiapo hicho cha ‘kuyalinda' dhidi ya ‘atakayeyachezea'? Au kuna Mapinduzi mengine? Au kuna maana zaidi ya Mapinduzi ambayo haijasemwa hapa?
Ninapotafuta majibu ya masuali kama hayo, ndipo ninapojikuta kulazimika kuziangalia nadharia zilizopo kuhusu Mapinduzi yenyewe. Nagundua kuwa kuna haja ya kwanza kujibu suali: Nini hasa kilitokezea tarehe 11 Januari, 1964?

Nadharia zipo tatu: mbili zimezoeleka, moja ngeni. Ya kwanza inasema kuwa siku hiyo kundi la vijana wa tabaka la chini lilipandwa na hasira kutokana na kuendelea kwa hali ngumu ya maisha, huku wakiwa hawaoni dalili yoyote ya mabadiliko yoyote ya kiuchumi na kisiasa yanayoweza kuwanufaisha. Wakaamua kuelekeza hasira zao kwa tabaka la juu na tabaka la kati, waliyoamini kuwa yanafaidi uchumi wa Zanzibar peke yao. Na kwa kuwa Mji Mkongwe ulikuwa kitovu cha matabaka hayo, vijana wa tabaka la chini wakaamua kuuteketeza kwa moto.

Kwa bahati kundi jengine la vijana wa chama cha Umma, kilichokuwa kikiongozwa na Abdirahman Babu, likaingilia kati mpango huo na ‘kuupa sura ya kimapinduzi' badala ya uasi tu wa kijamii. Matokeo yake ndiyo kupinduliwa kwa serikali ya ZNP/ZPPP na kuingia madarakani kwa serikali ya Afro Shirazi Party/Umma Party (ASP/UP).
Kwa hivyo, Mapinduzi lilikuwa tukio la kushtukizia tu, ambalo lilikuwa halikupangwa kitaalamu na ambalo, kama si uingiliaji kati wa vijana hao wa Umma, ambao wengi wao walikuwa ni wa tabaka la kati wakiwa na elimu nzuri na mafunzo ya kijeshi kutoka nchi za iliyokuwa Kambi ya Mashariki, basi pengine ungelikuwa uasi mdogo ambao ungelidhibitiwa na askari wachache wa serikali.

Hii ndiyo nadharia inayozungumzwa sana na kundi la wachambuzi wa Ki-marx na Ki-Lenin ambao kwao wao mabadiliko yoyote katika jamii ni matokeo ya msuguano wa kitabaka (class struggle). Hapana shaka, Babu na wafuasi wake (kwa sababu zao wenyewe) waliipigia sana chapuo nadharia hii hata imekuwa ni sehemu ya kumbukumbu za kimaandishi (literature) zilizopo kuhusu tukio hilo lililobadilisha mstatili wa mambo Zanzibar.

Nadharia ya pili inasema kwamba, kilichotokezea siku hiyo kilikuwa ni matokeo ya maandalizi ya ASP ya muda mrefu. Waafrika wenye uchungu na waliovunjwa moyo na matokeo ya kura katika chaguzi zote – kuanzia ule wa 1961 hadi wa 1963 – sasa waliamua kujitolea muhanga, wakasuka mipango ikasukika, na siku hiyo wakachukua mapanga na mashoka na kuivamia serikali kibaraka iliyokuwa chini ya usultani wa Kiarabu wa Jamshid bin Abdullah Busaidy na kuipindua.
Kwa mtazamo huu, yale yalikuwa Mapinduzi yaliyofanywa na Waafrika walio wengi dhidi ya utawala wa Waarabu wachache. Kiongozi wa Mapinduzi hayo alikuwa ni Abeid Amani Karume na kikundi cha watu 14 (Committee of Fourteen) ndicho kilichokuwa dhamana wa tukio zima.

Nadharia hii inayaangalia Mapinduzi kama tukio la kikabila na kama matokeo ya kawaida pale wachache wanapowatawala wengi bila ya ridhaa yao. Waafrika wengi dhidi ya Waarabu wachache. Muasisi wa nadharia hii, kwa hakika hasa, ni Julius Nyerere na propaganda yake ilienezwa vyema kupitia Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) kwa kushirikiana vyema na aliyekuwa mkoloni, Dola ya Uingereza. Hii ndiyo nadharia inayotumiwa na wachambuzi wengi wa Tanganyika hadi leo.

Nadharia ya tatu, na ambayo inaweza kuwa ngeni, inasema kwamba kilichotokezea siku hiyo ni majeshi ya dola ya kigeni, na hapa inakusudiwa Tanganyika, kuivamia nchi ya Zanzibar, kuiangusha serikali katika usiku wa tarehe 11 Januari, na kisha majeshi hayo yakarudi Tanganyika alfajiri yakiwacha nyuma waasi waliokuwa wametayarishwa kitambo kuendelea na mauaji na kukamilisha zoezi la kuunda serikali nyingine.

Nadharia hii inayaangalia Mapinduzi yale kama mavamizi ya dola moja dhidi ya nyengine katika mifano inayofanana na kile Indonesia ilichokifanya wakati Ureno alipoondoka Timori ya Mashariki na au Morocco ilichokifanya baada ya Hispania kuondoka Sahara. Nadharia hii inakwenda mbele kusema kwamba ni baada ya kujaribu Zanzibar na kufanikiwa, ndipo Nyerere ‘akatamukiwa' na akawa anapeleka majeshi yake katika nchi nyengine za jirani kusaidia kile kilichoitwa wakati huo "Mstari wa Mbele Katika Ukombozi wa Afrika."

Kuna simulizi zinazosema kuwa wakati Mfalme Jamshid alipowasili Portsmouth, Uingereza, kwa hifadhi ya kisiasa, alisema kwamba yeye hakupinduliwa na Wazanzibari, bali majeshi ya kigeni (Tanganyika) ndiyo yaliyoivamia nchi yake (Zanzibar). Inasemekana Nyerere na Baraza la Mapinduzi waliipata kauli hiyo na iliwatetemesha, kwani ilikuwa ikijenga hoja katika sheria za kimataifa dhidi ya ‘utakatifu' wa Nyerere na Mapinduzi ‘yake.' Hima ukapitishwa mkakati wa ‘kuisahaulisha' kabisa kauli hii; na kama ni kweli, basi mkakati huo ulifanikiwa maana hadi unasoma makala hii huenda ikawa ni mara yako ya mwanzo kusoma au kusikia haya.
Baada ya kuziangalia nadharia hizi tatu, sasa nikaona kuwa ni rahisi kujibu maswali ambayo nimeyauliza hapo juu. Kwa mfano, unapoipiganisha nadharia ya tatu kwa ya pili chini ya kivuli cha kauli kama hizi za akina Kikwete (za kulinda Mapinduzi dhidi ya anayeyachezea), unapata mwangaza wa jawabu nyengine nyingi hata kwa maswali ambayo hukuwahi kujiuliza mwanzoni. Nitafafanua.

Nadharia ya tatu inasema hivi: tarehe 11 Januari 1964, Amiri Jeshi Mkuu wa Tanganyika anaamuru kikosi maalum cha jeshi lake kwenda Zanzibar usiku na kuipindua serikali changa ya mwezi mmoja. Baada ya wiki moja, nadharia ya pili inasema, Amiri Jeshi huyu ambaye pia ndiye Rais wa Tanganyika, anazungumza na maafisa wa kibalozi na baadhi ya waandishi na kuyaelezea Mapinduzi ya Zanzibar kama tukio lililokuwa la lazima kuwapa nguvu Waafrika waliokuwa wengi dhidi ya utawala wa Waarabu wachache. Kwa nini Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanganyika anakuja na tafsiri hii? Anahusika?

Ndiyo, anahusika. Mimi nakubaliana na nadharia ya tatu, yaani kilichofanyika tarehe 11 Januari 1964, ulikuwa ni uvamizi wa dola moja dhidi ya nyengine, kwa maana ya kwamba serikali ya Tanganyika ilituma majeshi yake kuivamia Zanzibar na kuiondosha serikali madarakani, kwa mfano ule ule iliokuja kuufanya miaka kumi baadaye kwa kutuma majeshi yake kwenda kumuondoa rais wa Uganda, japo kwa sababu na malengo tafauti.

Kwa hivyo, leo hii unapomsikia kiongozi wa Muungano (ambaye kwa bahati ndiye pia kiongozi mkuu wa Tanganyika na Amiri Jeshi Mkuu) anaapa kuyalinda Mapinduzi, ana sababu za kufanya hivyo. Anayalinda kwa kuwa Mapinduzi haya ni yake katika kiwango na namna ile ile yalivyokuwa pale mwaka 1964. Yalifanywa na nchi yake dhidi ya nchi nyengine na ana kila wajibu wa kuhakikisha kuwa yanadumu.

Lakini kufika hapa nikajiuliza, hivi kwa nini Tanganyika iliipindua Zanzibar? Nikapata nadharia nyengine tatu. Moja ni woga wa Tanganyika kwamba, kuwa na jirani ambaye alikuwa anapiga hatua za kimaendeleo kwa kasi (kwa kiwango cha wakati ule) kungelikuwa na athari mbaya za kisiasa kwake, kwani wananchi wa Tanganyika wangekuja kuinuka na kudai maendeleo kama waliyokuwa wanayapata Wazanzibari kutoka kwa serikali yao. Hapa inakumbushwa kwamba hadi yanafanyika Mapinduzi, Zanzibar ilikuwa inajitegemea kiuchumi na inatoa misaada kwa nchi nyengine, ina wataalamu wa kutosha wa kizalendo na ina akiba ya kutosha kwa uwekezaji wa ndani katika hazina yake.

Nadharia ya pili ni kwamba, Zanzibar ilikuwa dhaifu kijeshi na kiulinzi na, kwa hivyo, ingeliweza kirahisi kutumiliwa na maadui wa Tanganyika kuishambulia hasa katika msuguano wa Vita Baridi. Inakumbushwa hapa kuwa Uingereza, pamoja na kuwa ilikuwa imekubali kutoa ulinzi kwa nchi nyengine za Afrika Mashariki zilizokuwa makoloni yake (Tanganyika, Uganda, Kenya na Yemen), ilikuwa imekataa kufanya hivyo kwa Zanzibar, na hivyo kwa makusudi kabisa kuiwachia iwe rahisi kuvamiwa, kushambuliwa na kudhuriwa.

Na nadharia ya tatu, ambayo ndiyo ninayokubaliana nayo, ni kuwa Nyerere alikuwa na ndoto za kujenga himaya kubwa ya utawala. Kwa hakika, hata jina la Tanzania, ambalo ulikuja kupewa mchanganyiko wa nchi hizi mbili (Tanganyika na Zanzibar), halikuwa limetokana na Tanganyika na Zanzibar kama inavyosemwa na baadhi ya watu. Jina hili linatokana na Tanganyika na Azania, na Azania ni upwa wote wa Afrika Mashariki, vikiwemo visiwa vya Komoro, Ushelisheli na Bukini.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba Tanganyika iliivamia Zanzibar na kuikalia na msamiati wa tendo hilo ukaitwa ‘Mapinduzi.' Sasa kuchezea Mapinduzi, kwa hivyo, ni kuchezea azma, dhamira na mbinu za Tanganyika dhidi ya Zanzibar. Vivyo, kulinda Mapinduzi ni kudumisha azma, dhamira na kuendeleza mbinu za Tanganyika dhidi ya Zanzibar.
Kadiri nilivyokuwa ninapata majibu ya maswali yangu ya mwanzoni, ndivyo nilivyopata hamu ya kujiuliza maswali mengine ya ziada. Kwa mfano, baada ya kauli ya Kikwete na kwa kuhusisha na kauli kama hiyo ya mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, pale mwaka 2005 kule Micheweni aliposema kwamba ameapa kuyalinda Mapinduzi, na matendo yake ya kumwaga vikosi vya kivita kwenye uchaguzi wa 2000, mauaji ya Januari 2001, na luteka la kijeshi la 2005 nchini Zanzibar, ni nani ‘mchezeaji wa Mapinduzi' hapa Zanzibar leo hii? Nirudi kwenye mgogoro wa kisiasa wa 1995, 2000 na 2005? Hapana, huko ni mbali sana.

Afanaalek! Si kuanzia katikati ya mwaka jana, Wazanzibari wamekuwa wakijikusanya pamoja kutetea mamlaka zaidi kwa nchi yao ndani ya Muungano? Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), pamoja na udhaifu mwingi ilionao, kwa mfano, ilimwambia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar ni nchi, yeye aliposema si nchi. Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamuhuna alifikia umbali wa kujitolea muhanga kwa lolote litakalokuwa, lakini alinde dhamira ya Zanzibar kuwa nchi. Waziri mwengine, Hamza Juma, amefikia umbali wa kusema kuwa Zanzibar itajiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC) kivyake ikiwa Serikali ya Muungano inakokota mguu. Waziri anayehusika na nishati, Mansoor Yussuf Himidi, ameshasema si mara moja wala mbili kuwa mafuta ni mali ya Wazanzibari na hilo ni vyema likaeleweka na kuheshimika hivyo tu.

Huo ni upande mmoja: wa CCM Zanzibar na SMZ tu. Kuna upande wa pili ambao ndio hasa injini ya kusimamia hadhi na heshima ya Zanzibar kisiasa – Chama cha Wananchi (CUF). Si Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, amezifufua na kuzipa mwelekeo mpya jitihada za Wazanzibari kuitetea heshima yao ndani ya Muungano? Si viongozi wengine, kama Juma Duni, wameutangazia ulimwengu mzima kuwa Zanzibar haijawa huru chini ya himaya ya Tanganyika? Si Ismail Jussa amefikia umbali wa kuwaahidi viongozi wa SMZ uungwaji mkono wa asilimia mia moja katika kuitetea nchi yao, hata ikibidi kuwapa ngome ya binaadamu (human shield) kama wataletewa vifaru na mizinga vya Serikali ya Muungano? Si Soud Yussuf Mgeni ametamka wazi kwamba sasa kugawiwa kwa misingi ya vyama kumefikia mwisho? Kwamba Zanzibar kwanza, u-CCM na u-CUF baadaye?

Ikiwa hivi ndivyo, basi Wazanzibari hawa ndio wanaoyachezea ‘Mapinduzingwa Matukufu.' Na hawa – wawe CCM wawe CUF – ndio Amiri Jeshi Mkuu aliowalilia kiapo, maana wanachofanya ni kupingana na azma, dhamira na mkakati wa Tanganyika kwa Zanzibar.

Huo ndio ukweli wenyewe na khabari ndiyo hiyo. Ni bahati mbaya sana, ikiwa wana-CCM wa Zanzibar waliokuwepo Kibandamaiti siku ile ya tarehe 25 Januari, 2009 hawakumuelewa vyema mwenyekiti wa chama chao. Wao wakadhani kuwa kile kilikuwa ni kitisho dhidi ya Maalim Seif, Duni, Jussa, Bimani, Aboubakar Khamis na Dkt. Juma Muchi tu. Ukweli ni kuwa kile ni kitisho zaidi kwa akina Mansoor, Shamuhuna, Hamza na hata Karume na Shamsi wenyewe kuliko kilivyo kwa viongozi wa CUF.
Mwisho, baada ya maswali na majibu yote hayo, nikajiuliza la mwisho: hivi, ikiwa la ‘kuyachezea Mapinduzi' ndilo hilo nililoliona, kuna ladha gani zaidi kwa Mzanzibari zaidi ya mchezo huo? Mchezo uchezwao na watu kama Maalim Seif na Shamhuna, Jussa na Hamza, Aboubakar na Mansoor?

Wallahi, fakhari iliyoje kuwa sehemu ya mchezo huo! Mchezo wa kikubwa, mchezo wa kizalendo. Mchezo ambao hauna kupoteza. Maana ikiwa utamalizika kwa Kikwete kufanikiwa ‘kuwashughulikia' wanaoyachezea Mapinduzi, wachezaji hao watatoka uwanjani mashujaa mbele ya jamii ya Wazanzibari kama alivyokuwa Hayati Abeid Karume. Kwake tulisema: "Kilichozikwa ni kiwiwili chako, bali Roho na Mawazo yako bado ya hai." Na ukimalizika kwa wachezaji kufanikiwa kuondosha azma, dhamira na mkakati wa Tanganyika kwa Zanzibar, watavikwa nishani za dhahabu, za lulu na yakuti. Majina yao yataandikwa kwa wino wa ajabu kwenye vitabu vya historia ya nchi yao. Kuna mchezo bora zaidi ya huo?

Jibu langu likawa "La, Hakuna!" Na kwa sababu hiyo, nami najiunga nao. Najiunga nao nikizingatia msemo: "Ama unganikeni muwe wamoja, au gawanyikeni muchinjwe mmoja mmoja." Ni juu ya Amiri Jeshi Mkuu Kikwete kuamua kuanza ‘kunishughulikia' mcheza mie niyachezeaye Mapinduzi yake. Ila hata akija na vifaru na mizinga, atanikuta ndani ya ardhi ya nchi yangu ninamuimbia Mama yetu Mpendwa, Zanzibar:

Kwa jinalo wewe, neno natamka, na kulikariri
Hitaka ujuwe, ndiwe mtukuka, ndiwe wangu huri
Sina mwenginewe, wala hatazuka, wa kumkubali
Watwani ni wewe, kila kitu wewe, Mama Zinjibari!
Nanisemwe kwawe, sitaadhirika, wala sitajali
Hata nichukiwe, sitababaika, moyo haudhili
Nitakuwa nawe, sitakugeuka, hilo ni muhali
Mimi ni kwa wewe, kwa myaka na kaka, Mama Zinjibari!
Nitukanwe kwawe, sitakukanuka, wala sitabali
Kwa vyovyote uwe, sitakugeuka, nitakukubali
Nimezawa nawe, kwako ‘meleleka, vipi nende mbali?
Mimi bila wewe, sina wa kushika, Mama Zinjibari!
Nipigwe kwa wewe, damu ‘tamwagika, kisha ‘tasubiri
Jela nifungiwe, niwe nadhikika, sitakughairi
Mateso nipewe, ita'wa baraka, na ladha nzuri
Kwa jinalo wewe, mimi nanonoka, Mama Zinjibari!
Wacha nife kwa'we, sitanung'unika, ‘tafurahi bali
Lolote naliwe, ewe mtajika, kwa wewe sijali
Nanilaumiwe, nitwikwe mashaka, na masilisili

Februari 2, 2009
 
Maoni yangu ni kwamba, Watanzania waishio nje ya Tanzania ni vizuri wakachangia mawazo katika kurekebisha na kuendeleza nchi kupitia vyama, makundi au mtu binafsi kwa mawazo, vitendo na mengineyo, lakini sikubaliani na suala la kuanzisha vyama nje ya nchi, au kufungua matawi ya vyama nje ya nchi. Maana watu hawa wanakuwa kwenye nchi nyingine inayotawaliwa na sheria tofauti kabisa, kwa hiyo huko ni ugenini na si mahala safi pa kufanyia shughuli za kisiasa kivyama, ila kiujumla ni sawa kabisa.
 
Dah wapemba kiboko, mmeshabadili maudhui ya thread hii kuwa "kero za muungano" siyo?
 
Kwetu sisi hakuna kero za "muungano", "muungano" wenyewe ndio kero.

Angalia nilikuwa najibu nini kabla hujaingiza mambo ya kitoto.

Mimi nazungumzia hizi kelele za CDM dhidi ya CUF lakini ni ukweli mtupu kuwa yote haya yanayotufika yanatokana na huu "muungano" wenu bomu
 
Nilijua ati kuwa hapo ndo target-kazi mnayo kwelikweli, ya nini kuja na mbinu za kizamani za kupigania uhuru zinazoamini kupandikiza majina kibao kwa wakoloni [wavamizi, mabeberu, nk] wakati uwezo mnaooo! Ukweli ni huu-maadamu nyote mnashabikia simba na yanga kwa timu za tanzania nyie ni sehemu tu ya Tanganyika, nasema Tanganyika siyo tanzania huu mpaka kiyama! (Tafakari). Mtoa mada ametoa point za msingi sana na ukweli mtupu tuko wengi ambao hatukuelewa logic ya ndoa ya cuf upande mmoja na 'nyumba ndogo' upande mwingine zo tukajitoa CUF. Pia ndoa ya cuf na ccm imedhihirisha kuwa vuguvugu la kisiasa la zanzibar siyo kutaka maendeleo au maisha mazuri kwa wazanzibari bali ni kutaka kundi flani la watu waingie madarakani ili kuendeleza ufisadi na unyonyaji. Kwani maisha yamezidi kuwa ya ovyo zanzibar, mapembe yangali yanamiminika, serikali imekuwa kubwa mno, tabaka baina ya wafanyakazi limeshaundwa zanzibar kama tanganyika ilivyo(prove me if am wrong), wazanzibari wanatafutiwa mchawi wao kama ilivyo tabia ya viongozi wa zanzibar- mwanzo ilikuwa cuf ndo kikwazo, sasaivi tanganyika ndo kikwazo, then sjui atafuata nani? ndugu zetu wa visiwani tulisoma nanyi huku Tanganika na mlikuwa na ufahamu mzuri tu. Je mnaoupeleka wapi ufahamu huu tunapojadili masuala haya?
 
Nilijua ati kuwa hapo ndo target-kazi mnayo kwelikweli, ya nini kuja na mbinu za kizamani za kupigania uhuru zinazoamini kupandikiza majina kibao kwa wakoloni [wavamizi, mabeberu, nk] wakati uwezo mnaooo! Ukweli ni huu-maadamu nyote mnashabikia simba na yanga kwa timu za tanzania nyie ni sehemu tu ya muungano huu mpaka kiyama! (Tafakari)

Kwa sababu kiama hatujui ni lini, tuko tayari kusubiri.

Roman Empire, Ottoman Empire, British Empire na hata Songhai Empire, ulipofika wakati wake zilianguka. Kuna tafauti gani na Tanganyika Empire?

Keep watching this page, we are not turning back.

*"Ule wakati wetu na Nyerere tulikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hawakubali, Bw. Sitta, ITS OVER" - Hassan Nassor Moyo, former SMZ/SMT Minister and ASP/CCM Veteran

"Its now or Never" - Mansour Yusuf Himid, SMZ Minister and Member of CCM NEC

View attachment 29570

View attachment 29571
 
Ndiyo maana nilimaliza na neno tafakari-hebu tafakari bac!
 
Hapa haiongelewi CDM bali ni facts. Labda tukupe mfano mdogo huenda ukakusaidia. CUF wakati wanagombea walikuwa na election manifesto yao ambayo ilikuwa inawaelekeza nini watafanya endapo watashinda katika uchaguzi ule. Sasa hawakushinda, na walishinda CCM wao wakaingia kwenye ule mseto wenye lengo la kutekeleza sera za CCM maana CCM ndio washindi. Kwa mantiki hiyo CUF wanaendelea kusimamia sera za CCM tena kwa lazima wakubali hata kama hawataki maana wapo pia serikalini. Hali kama hii lazima ilete tafsiri kwa wapiga kura. Maana wamefifishwa CUF. Hawawezi kuongea tena hasa huko visiwani kama wapinzani. Wakati Bara wanaCUF wapo kwenye bumbuazi maana chama kimesahau kuwa nao wanawahitaji. Tena basi wapo kimya hawasikiki wanafanya nini zaidi ya kuonekana kwenye dhifa za Kitaifa. Unadhani bado kuna uhai hapo.

Ahsante sana mkuu,naona hajaisoma vizuri thread,yuko ki siasa zaidi.
 
Back
Top Bottom