KWENU WAPAMBANAJI, ULISHAWAI KUKUTANA NA HALI HII AU BADO UNAIPITIA, USIKATE TAMAA HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Sijui kama wewe ulishafika hii stage, lakini kuna muda kwenye maisha unaona kabisa kila mtu anakukataa. Wale washkaji zako wa dam dam wanakufungia vioo, ndugu zako wanakupotezea, majirani wanakuchukulia poa, uliosoma nao chuoni au shuleni wanakuona jau, wana wa kukutana nao kwenye hustling wanakukwepa. Ukigeuka nyuma, kushoto, kulia na mbele huoni mtu yoyote anaye kusapoti.

Mwenzangu hiki ndo kipindi kigumu sana kwa sisi wapambanaji (hustlers), lakinj pia ndo kipindi kizuri zaidi kwetu ma hustler. Wengi hua wanashindwa kutoboa hii hatua ya maisha na ukishindwa kuruka hiki kihunzi kuna uwezekano mkubwa maisha yako yatakua hohe hahe, ukifanikiwa kupenya hii hatua basi umemaliza mchezo.

Hiki ni kipindi unatakiwa uwe kivyako kwa asilimia kubwa (sio kujitenga), hiki ni kipindi cha kupiga mchujo wa kiwango cha lami, kupunguza ndugu na kublock marafiki zako wanafki. Sio kwamba una roho mbaya, una kisasi au una kiburi, hapana ni kwa ajili ya manufaa yako na manufaa ya wanao. Hiki ni kipindi ambacho mapambano yako yanakuhitaji wewe kwa asilimia kubwa, umakini na jitihada zako zako zinahitajika kuliko kipindi chochote. Watu wengi hua wanapotea kwasababu wanayeyusha umakini wao katika kipindi hiki kwenye vitu vingi vinavyowawekea vikwazo.

Utakuta muda mwingine unawaza maneno ya wajomba, kidogo umefungua WhatsApp mliosoma nao au mshkaji wako kapost status flani unahisi wewe ndo umesemwa, kidogo ukiingia kitaa unaona vijana wdogo chini ya 25 wanapiga misele na ndinga kali, umekaa kidogo unasikia dogo flan kahitimu chuo kashapata kazi hapo wewe una miaka mitano upo kitaa hujawahi kuitwa hata interview 1. Kimsingi huu utumbo wote unakufanya upoteze dira nzima. Maana yake umeyetusha umakini wako ambao ilibidi uupeleke kwenye mapambano yako.

Unajua nini kinasababisha usipige hatua? Ni mambo yaliyojaa negativity kama haya yana kandamiza juhudi zako zote na kukifanya wewe mwenyewe uanze kujiona boya. furaha yako na kujiamini kwako vyote vinapotea unaanza kujijengea sumu ya mashaka, chuki, wivu nk

badala ufocus na kujenga maisha yako unaanza kupambana na stress, wivu, chuki, kutokujiamini kwasababu tu umeelekeza umakini wako kwenye mambo ambayo hayakupigishi hata hatua moja.

Ndio maana nasema kupunguza watu fulani kwenye maisha yako si kosa, si dhambi, si kiburi ni kwa manufaa yako.

Credits: jamaa alieandika hii anaitwa sirfeff, yupo instagram
 
Mengine yote umeongea point za msingi sana ila umevuruga hapo uliposema kuhusu insta followers na likes
 
Nakazia🔨 ndio kipindi cha kujipanga napia wakubadilika,naku wa block wale wasio na faida naww
 
Watu wote hao hawawezi kukukataa with no reason jichunguze before uanze kulaumu watu
 
Kuna muda unapaswa kubaki na watu wachache na muhimu.unapoyumba kimaisha wakati mwingine ni kipimo cha kujua marafiki wa kweli na wachomaji.hata wenza pia hiki ndio kipimo kwani wenza ambao sio wavumilivu hukupa kisogo katika kipindi hiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom