Kwenu Tanzania Revenue Authority (TRA) na mfumo wenu mpya wa eFilling.

babayao255

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
11,121
27,212
Kwanini mnalazimisha wafanyabiashara kutumia huu mfumo mpya wa eFilling system kutuma VAT za kila mwezi huku mkijua kabisa huu mfumo bado una changamoto na haujakaa sawa bado?

Nimeona pia mfumo wa zamani tayari mmeshaufunga!
Hizi haraka haraka ni za nini?

Juzi kuna semina yenu mlifanya hapa Dar Es Salaam kupitia Smart ERP, hamuoni kuwa ile semina haitoshi na inawapasa kufanya semina zingine zaidi?

Huu mfumo mnaolazimisha wafanyabiashara wautumie una changamoto na unasumbua.

Unaweza kuwa ni mfumo mzuri lakini embu rekebisheni kwanza malalamiko mnayopewa.
 
KwA kweli ni changamoto.
Mambo yanarudi kinyumenyume yani.
Kwanza system yao inachosha kweli kweli.
Seminar moja haitoshi na uhakika haijawafikia walengwa wote.
Bora wafungulie tuu hiyo ya mwanzo wakiwa wanajipanga vizuri
 
Wana haraka sijui wanakimbilia wapi!
Au labda kuna 10 percent wanapiga!
 
Hehehehe..ila leo nimejaribu kuingia mfumo wa zamani,imekubali kuingia. Inawezekana wamekubali iendelee kutumika wakisort matatizo yao.
 
Hehehehe..ila leo nimejaribu kuingia mfumo wa zamani,imekubali kuingia. Inawezekana wamekubali iendelee kutumika wakisort matatizo yao.

Wa zamani wamefungua kwa ajili ya wale ambao hawakuwasilisha return za mwezi wa tatu.
Wewe komaa na mfumo mpya tu wa zamani haukuhusu.
 
Kwanini wabongo mnapenda deadline??
Ndo ukome andaa 250,000.mimi ni marufuku muhasibu wangu kuvuka tar 15 .
Wewe naee,umejibu kimazoea.
Kuna changamoto chungu nzima za mfumo mpya wa VAT Return. Ukiachana na hilo siku za mwanzo hakukua na access kabisa mtandaoni.
Most of the time mlio juu ya wafanyakazi mnaishia kuhukumu wa chini yenu bila kujali sababu msingi.
 
asante kwa kumpa za uso
 
Kwanini wabongo mnapenda deadline??
Ndo ukome andaa 250,000.mimi ni marufuku muhasibu wangu kuvuka tar 15 .

Huu mfumo mpya hakuna cha kuwahi wala sijui nini.Huu mfumo unakataa receipts 10 unakubali receipts 2 ?.

TRA mnamkwamisha Mama na haya maujanja yenu ya 10%.
 
Huu mfumo mpya hakuna cha kuwahi wala sijui nini.Huu mfumo unakataa receipts 10 unakubali receipts 2 ?.

TRA mnamkwamisha Mama na haya maujanja yenu ya 10%.
Yaani mwenyewe yamenikuta unascan risiti kuhakiki ila inatemwa vilevile
 
mfumo wa e felling 2.0 ulibidi ubaki kwenye pilot study ya upto 6 months ili kuwe na option ya kufile kwa mfumo huu au wa awali wakati bado unastudy changamoto za mfumo mpya.. mmh mfumo una balaa huuu.. sio tarehe 1 wala tarehe 20..muda wote unasumbua..
 
Inachosha kweli hii i say.
Kilasiku kujifunza vitu vipya.
No settling yani.
 
Back
Top Bottom