Kwenu CHADEMA, nimegundua kila kinachofanyika na Serikali kipo kwenye Ilani yenu

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Naandika Mimi Rashda Zunde

Nimepitia Ilani ya Chama chenu kwa makini sana na kugundua kitu kimoja kwamba KILA KINACHOFANYIKA NA SERIKALI NDICHO KILICHOPO KWENYE ILANI YENU NA MNAUMIA KUONA YAKIFANYIKA VIZURI SABABU SIO NYINYI NDO MNAFANYA.

Mlidhani kwamba Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita kufanya mambo makubwa yenye tija kwenye nchi hii tena ndani ya muda mfupi. Ndani ya mwaka wake mmoja tu dunia ilishatambua kwamba sasa Tanzania mama anafanikisha maendeleo endelevu.

Turudi kwenye mada sasa; Ilani ya Chama chenu CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye kiambatanisho hapo chini ni kwamba mliahidi sekta binafsi zishirikishwe kwenye uwekezaji na kuvutia mashirika makubwa ya meli. Sasa niwaulize kwani DP WORLD ni shirika dogo ? Kwani Serikali inavyohakikisha kwamba inazingatia sheria na taratibu zote za ulinzi katika kuhakikisha mwekezaji anapatikana ni kosa?

Mbona mnakua na roho ya kwanini jamani, ilani zote zinataka TANZANIA ipate maendeleo endelevu na kuhakikisha bandari zetu zinakuwa na ufanisi maana hata nyie mngekua madarakani mngeichukua tu DP WORLD kwahiyo acheni huo upotoshaji wenu kisa tu sio nyie mlioko madarakani.

Serikali ya awamu ya Sita haiwezi kuweka usalama wa nchi matatani, hatua za uwekezaji kwa kuzingatia sheria zimefuatwa na zinaendelea kufuatwa ili bandari zetu ziweze kuwa na tija na kuleta manufaa.

Sisi sote ni wamoja na wote tunataka maendeleo, DP WORLD ikifanikisha ufanisi bandarini maisha ya watanzania yanaenda kuwa bora bila kuzingatia huyu katoka chama gani. Upotoshaji mnaofanya unania mbaya ya kuligawa taifa na si jambo zuri kabisa.

Tanzania ni huru na kuna uhuru wa kutoa maoni lakini sio kupotosha kama mfanyavyo.

Kama Ilani yenu inasema hivi na nyie sasa hivi mnasema hivi mnafanya wanachama wenu wawe na mashaka na maamuzi yenu, je mtaweza kutimiza ahadi zenu pindi mkipewa nchi kuiongoza? Hivyo basi kuweni na msimamo tuungane na serikali katika kuhakikisha nchi inasonga mbele.

Serikali imeweka wazi kwamba inapokea maoni katika suala hili la bandari hivyo basi toeni maoni na ushauri la sio MATUSI na dhihaka kama anavyofanya TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU.

1690793782413.png
 
Back
Top Bottom