Siwezi kukupa Advantage za Advance ila nitakupa advantage za DIT kwani mimi ndiko nilikopatia FTC yangu kabla sijatunukiwa shahada pale MECHE Coet
Advantage za DIT
- Unaanza maisha ya chuo mapema so matatizo ya elimu ya juu utayazoea mapema
- Unaanza kula bumu la Industrial Training (IT) UD wanaiita PT mapema so utaanza kufaidi mapema
- Waalimu wanaokufundisha wengi wana masters so exposure yao ni kubwa tofauti na Advance
- Hakuna Tuition tofauti na advance
- Msosi wao si mchezo kila siku usiku na siku za jumapili mnagonga rice, asubuhi chai maziwa na mkate, jumapili mnapiga chai na mayai NB kama ratiba ya msosi haijabadilika kwani mimi nimeondoka huko takribani miaka saba iliyopita
- Kama ukichemka unaendelea na ujuzi wako kama kawaida
- Vile vile nafasi ya kwenda chuo kikuu ipo pale pale kwani hata mimi nilikuwa na wasiwasi lakini mungu akasaidia nikapasua na kufanikiwa kwenda mlimani.
- Siku hizi wanatoa Diploma tena mfumo wa sasa ni rahisi zaidi kwani wanasoma kwa semister so kama wewe ni kichwa ni virahisi kufauru tofauti na enzi zangu kwani kulikuwa na pepa la mwisho kutoka NECTA
Mkuu nikushauri kama upo serious DIT ni bora kuliko huko unakokufikiria, kuna jamaa walichomoa kujiunga DIT eti wakaenda Advance then at the end walipochemka advance wakaomba St Joseph ambapo wanafundisha Engineering hiyohiyo
Thanks for further information ni PM