Kwenda kuonja vitoweo halisi vya Sichuan katika mji maarufu wa Chengdu wenye vyakula vya kuvutia

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Hivi karibuni, mji wa Chengdu, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Sichuan uliidhinishwa kujiunga na mfumo wa miji yenye wazo la uvumbuzi wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni wa Umoja wa Mataifa, na kupewa sifa ya "mji maarufu wenye vyakula vya kuvutia", na kuwa mji wa kwanza wenye sifa hiyo barani Asia. Nchini China watu husema, "vyakula vizuri vya kuvutia viko nchini China, na vyakula vyenye ladha nzuri zaidi viko mkoani Sichuan", vitoweo vya Sichuan vimekuwa na historia ya miaka mingi, sifa za vyakula vya Chengdu zinajulikana nchini na katika nchi za nje.
Sichuan inachukuliwa na wachina kuwa ni mahali penye vyakula vizuri vya kuvutia, vitoweo vya Sichuan vikiwa moja kati ya makundi manne ya vitoweo vya nchini China, vinajulikana sana nchini China hata katika nchi za nje kutokana na mapishi yake ya kipekee na yenye umaalumu wa Sichuan. Vitu vingi vinaweza kutumiwa wakati wa kupika vitoweo vya Sichuan, hivyo vitoweo vina ladha za aina mbalimbali, wakazi wa Sichuan wanapenda zaidi ladha za mwasho za Huajiao na pilipili, hata wakati watu wanapoongea kuhusu vitoweo vya Sichuan, wanafikiria ladha za mwasho za Huajiao na pilipili, utamu na harufu nzuri za vitoweo vya Sichuan. Kwa kuwa Sichuan iko kwenye sehemu ya bondeni, hewa ya huko ni yenye unyevunyevu, Huajiao na pilipili zina uwezo wa kutembeza damu kwa haraka na kuondoa baridi mwilini, hivyo ladha za mwasho mkali zinapendwa na watu wa Sichuan kizazi baada ya kizazi.

Kutokana na takwimu zisizokamilika, vitoweo vya Sichuan viko vya aina zaidi ya 4,000, na vitoweo maarufu zaidi ni pamoja na nyama ya kuku ya Gongbao, nyama ya bata iliyofukizwa moshi wa mbao ya camphor na kupikwa pamoja na majani ya chai, nyama ya nguruwe iliyopikwa mara mbili na nyama ya nguruwe yenye ladha ya samaki, vitoweo hivyo vinajali sana rangi, harufu, ladha na muonekano wake. Ofisa wa mkahawa wa Hongxing, ambao ni mmoja kati ya mikahawa maarufu sana yenye vitoweo vya Sichuan mjini Chengdu, Bw Li Wei alisema,

"Vitoweo vyenye umaalum zaidi vya Sichuan ni nyama ya nguruwe iliyopikwa mara mbili, Mapo Tofu na nyama ya kuku ya Gongbao, wakazi wa sehemu nyingine waliofika Sichuan wengi wanapenda vitoweo hivyo."

Vyakula vinavyotumbukizwa katika maji moto kwa muda mchache na kuliwa vya Sichuan ni maarufu sana sawasawa na nyama ya kuku ya Gongbao. Watu wengi wanasema, watu waliofika Sichuan bila kula vyakula vilivyotumbukizwa katika maji moto kwa muda mchache na kuliwa ni sawa na watu wasiofika Sichuan. Wenyeji wa Sichuan wanapenda sana vyakula vinavyotumbukizwa katika maji moto kwa muda mchache na kuliwa, watu kadhaa wanaketi wakizunguka sufuria kubwa yenye maji moto, ndani ya sufuria yamewekwa maji yalitiwa viungo mbalimbali, vyakula vinatumbukizwa katika maji moto kwa dakika chache hadi kuiva, kisha vinatolewa na kuliwa pamoja na pilipili, huajiao, chumvi na ufuta. Mfanyakazi wa mkahawa maarufu wa vyakula vya aina hiyo dada Wanglilin alisema,

"Umaalumu wa vyakula vinavyotumbukizwa katika maji moto kwa muda mchache na kuliwa ni mwasho wa huajiao, pilipili, utamu na harufu inayonukia vizuri, ambavyo vinavutia watu na kuamsha shauku ya watu ya kula. Mbali na hayo, mboga zinazotumiwa ni mbichi sana tena ziko aina nyingi. Maji yanayotiwa katika sufuria ambayo yana viungo mbalimbali pia yako ya aina nyingi, yakiwemo ya viyoga vinavyoota mlimani, chakula kitamu cha mlimani cha kiwango cha juu, ambacho kinajenga mwili sana. Licha ya hayo, kuna supu ya mifupa na dawa za miti-shamba, pia zinajenga mwili. Vyakula vinavyotumika ni pamoja na nyama ya ng'ombe na kondoo iliyokatwa kuwa vipande vyembamba sana, vyakula vingine vinavyotumika ni pamoja na utumbo, makoromeo ya ng'ombe, mkunga(eel) wanaoishi kwenye shamba lenye maji la mpunga na mboga. Mbali na vyakula hivyo vya kutumbukizwa katika maji moto, kuna supu ya samaki wadogo, ambayo ni tamu sana."

Chakula kingine kinaitwa "chuanchuanxiang", ambacho kiliendelezwa kutokana na vyakula vinavyotumbukizwa katika maji moto. Tofauti na vyakula vinavyotumbukizwa katika maji moto, chuanchuanxiang ni vyakula vinavyotungwa kwanza kwenye vijiti vya mwanzi, na kutiwa viungo mbalimbali kabla ya kutumbukizwa katika maji moto. Meneja wa tawi la mkahawa wa Yulin, ambao ni maarufu sana mjini Chengdu, Bw Feng Qingshu alisema, chuanchuanxiang ni chakula chepesi zaidi kuliko vyakula vile vinavyotumbukizwa katika maji moto, tena bei yake ni nafuu zaidi, hivyo inapendwa na watu wengi.


Chakula chepesi cha Chengdu vilevile ni aina moja maarufu kati ya vyakula vitamu vya Sichuan. Chakula chepesi ni pamoja na Laitangyuan, Longchaoshou, Zhongshuijiao, Dandanmian na Sandapao, ambavyo vinapendwa sana na watu.

Ukitafuta habari kuhusu chakula kitamu cha Sichuan ni rahisi sana kupata tovuti inayoitwa "Chuanweifang", tovuti hiyo ilianzishwa na kikundi cha vijana wanaopenda chakula cha kisichuan, wakitarajia vitoweo vya kisichuan vienezwe mbali zaidi kutokana na upendo wao wa makwao. Kiongozi wa tovuti hii Bw Hu Bin alisema,

"Tuliwatembelea watu wengi wanaopenda chakula kitamu cha kienyeji, vilevile tuliwatembelea wapishi binafsi, walisema, ladha ya chakula cha kienyeji cha Sichuan si katika vitoweo au vyakula vile vinavyotumbukiza katika maji moto tu, bali inatakiwa kuanza toka mwanzo, ikiwa ni pamoja na kuchaguliwa vyakula, maandalizi ya viungo vya chakula hadi vitoweo kuuzwa, katika upande huu kuna njia yake maalumu. Sisi vijana tunajiamini, tutaweza kueneza vitu vingi vizuri vya kwetu, tena tunapenda chakula kitamu, hivyo tuliamua kuanzisha tovuti hiyo."

Kwenye tovuti hiyo, utaweza kufahamu vizuri vitoweo vya chakula kitamu cha Sichuan, hadithi yake na kufahamishwa mahali ilipo mikahawa ya vitoweo vya kisichuan, tena unaweza kuona utamaduni mkubwa unaohusu chakula kitamu. Bw Hu Bin alisema, toka zamani Sichuan ilijulikana sana kutokana na chakula chake kitamu, utamaduni wa starehe ni upande mmoja muhimu katika tabia ya Msichuan. Alisema,

"Wakati watu wanapopata nafasi ya kupumzika, hususan wazee, wanapenda sana kufanya utafiti kuhusu vitoweo, baada ya kufanikiwa wanaeneza kati ya jamaa na marafiki zao, kama vinapendwa na watu, wanavieneza zaidi."

Ladha za vyakula vya Sichuan zinaendelezwa na wenyeji, endapo unapata nafasi ya kufika Chengdu, bila shaka utapata kitoweo kinachokupendeza.
1.jpg
2.jpg
3.jpg
 
Back
Top Bottom