kweli ya tatu na ya nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kweli ya tatu na ya nne

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Dec 9, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}

  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}
  Mwalimu wetu alisimama mbele ya lectern[jukwaa la kuzungumzia] tena,na kusema,''Saa tunayo Kweli Tukufu ya Tatu,ambayo ni kati ya rahisi na fupi katika hizi Kweli.
  ''Kama Gautama alivyofundisha,mtu akiacha kuwa na matamanio na kitu basi mtu ataacha kuwa na mateso yanayohusiana na kile kitu;mateso yanaisha kabisa kama matamanio yakiisha kabisa.
  ''Mtu ana matamanio kwa kawaida kwa vitu vya mtu mwingine,anavitamani-anatamani kile ambacho kinamilikiwa na mwingine,na kama hawezi kuvipata hivyo vitu hasira inaingia,na anamchukia yule anayevimilki vile vitu anavyovitamani.Hii inaleta kuakata tamaa,hasira na maumivu.
  ''Kama mtu anakitamani kitu ambacho hawezi kukipata,basi atakosa furaha. Matendo ambayo yanatokana na matamanio yanaleta kukosa furaha. Furaha inatokea ukiacha kuwa na matamanio,ukiyachukulia maisha kama yanavyokuja,mema na mabaya.'' Yule Mwalimu wa Kihindi aliyageuza makaratasi yake,akatingishika kidogo,halafu kasema,''Sasa tunakuja katika Kweli ya nne ya Kweli Nne Tukufu,lakini Kweli ya Nne ya Kweli Nne Tukufu imegawanyika katika sehemu nane ambazo zinaitwa Njia ya Nane Takatifu. Kuna hatua nane ambazo mtu anaweza kuzichukua kupata ukombozi kutokana na hamu za mwili,kupata ukombozi kutokana na matamanio yake. Tutazipitia. Ya kwanza ni.
  {1} Maoni Sahihi:

  Kama Gautama alivyofundisha,mtu lazima awe na maoni sahihi kuhusu kukosa furaha. Mtu ambaye hana furaha au ana huzuni lazima atafute kwa nini hasa hana huzuni au hana furaha,lazima ajichunguze na agundue ni nini chanzo ya yeye kukosa furaha,halafu huyo mtu ataweza kufanya jambo juu ya hilo kupata ukweli wa nne wa Kweli Nne Tukufu ambayo ni-Naweza vipi kupata furaha?
  ''Kabla ya kuendelea na safari ya maisha yetu na akili shwari na matumaini kwamba tutaishi maisha jinsi ambavyo tunapaswa kuishi maisha lazima tuyafahamu malengo yetu. Ambayo inatuleta kwenye hatua ya pili ya Njia ya Nane Takatifu.

  [2].Malengo Sahihi: Kila mtu 'anawania' kitu fulani,kinaweza kuwa cha kiakili,kimwili,au faida ya kiroho. Inaweza kuwa kuwasaidia wengine,inaweza kuwa kujisaidia wenyewe tu. Lakini,kwa bahati mbaya,binadamu wamechanganyikiwa sana, hawana uongozi,wamepotea,wanashindwa kufahamu kile ambacho wanapaswa kukifahamu. Lazima tuyabandue maadili yote ya uongo,maneno yote ya uongo,ili tuweze kuona vizuri ni kitu gani na kile ambachi tunatakiwa kuwa,na kile ambacho tuna hamu nacho. Lazima tuyaache maadili ya uongo ambayo ni dhahiri yanaleta kukosa furaha. Watu walio wengi wanafikiria tu''Mimi'',na ''changu'' na ''nafsi''. Watu walio wengi wanajifikiria wenyewe tu,hawajali kabisa kuhusu haki za wengine. Ni lazima tujitazame nafsi zetu kama kitu ambacho tunahitaji kujifunza,tujitazame kama tunavyomtazama mtu ambaye hatumfahamu:Unampenda mgeni? Ungependa awe rafiki yako wa karibu?Ungependa vipi kuishi naye kwa maisha yote,unakula pamoja naye,unavuta hewa pamoja naye,unalala pamoja naye? Unapaswa kuwa na malengo sahihi kabla hujaweza kupata mafanikio katika maisha,na kutokana na hii kuwa na malengo sahihi inafuatia kwamba lazima uwe na:

  {3} Maneno Sahihi:

  Hii ina maana kwamba mtu ni lazima ayamiliki maneno yake,asiongee maneno ya kukashifu,asizungumze maneno ya uvumi kama vile uvumi ni kweli. Na Maneno Sahihi ina maana kwamba wakati wote umpe mtu mwingine faida ya shaka[ benefit of the doubt],na jizuie kuzungumza kama maneno yanaweza kumdhuru mwingine,zungumza tu wakati maneno ni mazuri,wakati maneno yanaweza kusaidia. Maneno yanaweza kuwa na madhara kuliko upanga,maneno yanaweza kuwa na sumu kuliko sumu kali kuliko zote. Maneno yanaweza kuliangamiza Taifa. Kwa hiyo,lazima uwe na maneno sahihi,na maneno sahihi yanatokana na:

  {4}'' Tabia Sahihi:Kama ukiwa na tabia sahihi hautaongea katika njia ambayo siyo sahihi. Kwa hiyo,tabia sahihi inachangia mtu kuwa na maneno sahihi na malengo sahihi.' Tabia Sahihi maana yake mtu hasemi uongo,hatumii vilevi,haibi.

  ''Gautama alifindisha kwamba sisi ni matokeo ya mawazo yetu wenyewe. Tulivyo sasa ndivyo mawazo yetu yalivyotu sababisha tuwe tokea zamani. Kwa hiyo tukifikri kwa usahihi sasa,tukiwa na tabia nzuri sasa ,tutakuwa ''sawa'' katika wakati fulani mfupi ujao .[Yaani tukiwa sahihi sasa,tutakuwa sahihi,dakika tano kuaznia sasa]
  ''Gautama alisema kwamba ,''Chuki haiishi kwa chuki wakati wowote;chuki inaweza tu kushindwa na upendo'' Alisema pia,''Mtu aishinde hasira ya mwingine kwa upendo,aushinde uovu wa mwingine wa wema wake.'

  ''Kama nilivyofundishwa mara nyingi,mtu asitoe ushahidi kuhusu vipaji vya akili,mtu asiwashambulie wale wanaokushambulia,kwa sababu kufuatana na maneno ya Gautama mtu asiwashambulie wale wanaokushambulia na maneno ya matusi au na fimbo au mawe. Gautama alisema.''Kama mtu akikulaani,ikandamize hasira yote yote na udhamirie kwamba hakuna neno la hasira litakatiza midomo yako. Utabakia mpole na mwenye urafiki na bila nia ya kutaka kulipiza kisasi.'
  ''Imani yetu ya Kibudha ni ya Njia ya Katikati,kanuni ya kuishi,kanuni ya kuwatendea wengine tunavyotaka kutendewa wenyewe. Inayofuatia katika Njia ya Nane Takatifu:

  {5[ Riziki Sahihi: Kufuatana na Mafundisho ya Buddha kulikuwa na riziki fulani ambazo zilikuwa na madhara kwa mtu,riziki fulani ambazo hazikuweza kufuatwa na Mbuddha wa kweli. Kwa mfano Mbuddha wa kweli hakuweza kuwa muuza nyama au muuza sumu,pia hakuweza kuwa mfanya biashara ya watumwa au kumiliku watumwa. Mbuddha hakuweza kunywa au kusambaza vilevi. Mbuddha mzuri,wakati wa Gautama ,kwa kawaida alikuwa ni lazima awe mtu anayetangatanga peke yake au anaishi katika monasteri.

  {6} Juhudi Sahihi: Juhudi Sahihi ina maana maalum;ina maana kwamba lazima uende mbele kwa kasi ambayo inakufaa wewe mwenyewe katika Njia ya Nane Takatifu. Mtu anayetaka kuenddelea asiwe na papara na kutaka kwenda mbele mbio kabla hata hajajifunza yale anayotakiwa kujifunza Lakini tena,huyo mtafutaji,hatakiwi kujirudisha nyuma na soni za uongo au unyenyekevu wa uongo. Mtu anaweza tu kuendelea kwa kasi yake mwenyewe.

  {7} Akili Sahihi: Ni akili ya Mtu ndio inayoongoza matendo yake. Wazo ni baba ya tendo,na mawazo mengine hayafai kabisa. Hamu za mwili zinaweza kumpotosha mtu na kumletea madhara. Mtu anaweza kuwa na hamu ya kula chakula kingi sana au kinono sana;ile hamu haimletei mtu maumivu,lakini kula kupita kiasi kutamletea maumivu. Kukosa furaha na maumivu yanatokana na kula kupita kiasi,na kunafuatia hamu kubwa sana ya kula.

  Mbuddha lazima akumbuke kwamba hisia[ feelings]hazidumu muda mrefu ,zinakuja na kuondoka kama upepo ambao unabadilika kila wakati. Hisia[emotions] ni kitu ambacho siyo tulivu na haziwezi kutumainiwa. Mtu lazima ajifundishe ili awe na akili sahihi wakati wote bila kujali hamu zake za mpito.

  (8) Kutafakari Sahihi:Kama Gautama alivyojua yoga haikuwa kwa njia yoyote ile jawabu la kupata mafanikio ya kiroho. Yoga ilikuwa tu seti ya mazoezi ya kuiwezesha akili kuudhibiti mwili,imelengwa kuiwezesha aliki kuumilki mwili kwa amri ya akili. Haikulengwa kumsaidia mtu kirohoKatika Kutafakari Sahihi mtu lazima ayamiliki mawazo ambayo siyo muhimu ya akili,lazima ajue mahitaji yake mwenyewe. Kwa kuwa na Tafakari Sahihi unaweza kutafakari-kutafakuri-[contemplate]-ili bila hoja[without reasoning] unaweza kufikia hitimisho kwa intuition kuhusu jambo gani ni sahihi au jambo gani siyo sahihi kwako.''


  Sauti ya yule Mwalimu wa Kihindi ilisimama na akaonekana kama vile anazinduka na kurudia wakati wa sasa. Macho yake yakatutazama wote halafu yakatulia kwangu..''Wewe'',akasema,huku akinielekeza kidole chake.''Nataka maneno na wewe,njoo nje kwenye corridor. Polepole nikainuka na kuelekea kwenye mlango. Yule Mwalimu wa Kihindi alifuatia na kufunga mlango nyuma yake,halafu akaufungua tena,na kuchungulia ndani na kusema,''Nyinyi watoto,sitaki kusikia sauti yoyote kutoka kwenu,nitakuwa hapa nje tu.'' Akaufunga ule mlango tena na akasimama ameupa mgongo.'' Sasa mtoto,'akasema,ulienda kumuona Dalai Lama;amekuambia nini?'''' Mheshimiwa Mwalimu,''nikalalamika,''Siruhusiwi kusema lilitokea,kusema neno lolote liliotokea.'' Akanigeukia kwa ghadhabu na akapiga makelele,''Mimi ni Mwalimu wako,nakuamuru uniambie! Ulinitaja mimi?''
  ''Siwezi kukuambia,mzee,''nikasema. '' Naweza tu kurudia kwamba siruhusiwi kutoa maoni kuhusu yaliyotokea.''
  ''Nitakuripoti kwa uasi na kukosa heshima,na kwa kuwa,kwa ujumla mwanafunzi ambaye hafai kabisa.'' Baada ya kusema hivyo,akainama mbele na kunipiga kwa nguvu upande wa kushoto na upande wa kulia wa kichwa changu. Akageuka na kuingia darasani,uso wake umewaka kwa hasira. Nilimfuata na kurudi nilipokuwa nimekaa.

  Yule Mwalimu wa Kihindi alirudi katika lectern halafu akayachukua makaratasi yake. Alifungua mdomo wake wakati ulu ule ambapo lama aliingia ndani . ''Mheshimiwa Mwalimu,''yule lama alimwambia yule Mwalimu wa Kihindi,,''Ni lazima nikueleze kwamba unatakuwa uende kwa Aboti na nimeagizwa kuedelea na hii lecture. Tafadhali nieleze ulipoishia nami nitafurahi kuendelea.'' Kwa kuchukizwa kidogo yule Mwalimu akatoa muhtasari wa alipofikia,na akasema alikuwa anataka kuongea kuhusu Nrvana. Halafu akasema,''Inanipa furaha kubwa kwamba nitakuwa naondoka kutoka katika darasa lenu na natumaini furaha yangu itaongezeka kwa kutokurudi tena.'' Baada ya kusema hivyo akayukusanya makaratasi yake yote na kuyaweka katika mkoba wake wa ngozi,akaufunga kwa sauti kali,na akaonodka kutoka kwenye chumba na kumuacha lama akionekana kuwa amestaajabu kidogo kwa ajili ya hasira aliyoiona.


  Tulitabasamu kwa sababu tulijuwa kwamba sasa mambo yatakuwa afadhali zaidi,kwa sababu huyu lama mwenye umri mdogo kiasi,alikuwa kijana kiasi kuelewa hisia za watoto.''Nyinyi vijana -mmekuwa katika hii lecture kwa muda gani? Mmekula chakula chochote?'' aliuliza. ''Kuna yeyote kati yenu ambaye anataka kuondoka kwa muda mfupi?'' Wote tulitabasamu na kumhakikishia kwamba tulikuwa hatuna shauku ya kuondoka. Kwa hiyo akatingisha kichwa chake katika hali ya kuridhika wakati akienda kwenye dirisha na akatazama nje kwa muda mfupi.


   
 2. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  heshima yako mzee.

  angalia private messege zako. nimekutumia kitambo sijapata jibu, please respond

  thanks in advance
   
Loading...