ARGAN MARA
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 1,135
- 2,940
ENZI ZA UTOTO TULIAMINI KWAMBA...
Kwa Wahenga tu si Kwa KIzazi cha Video Game
1. Ukiweka SINDANO kwenye RELI (aidha ya kirungu au ya kushonea) Basi TRENI ikipita itapinduka...
2. Ukila TUNDA lenye mbegu mfano chungwa, Bungo au Ubuyu, tulijitahidi tusimeze MBEGU, maana tukiamini kuwa ukimeza mbegu Mti wa ilo tunda utaota kichwani.
3. Tukiamni kuwa ukinyooshea kidole KABURI, basi kidole chako KITAOZA.
4. Ukiona Kuku wakipigana UKICHOMEKA KISU chini ardhini watapigana mpaka mmoja afe.
5. Mtu mwenye KIGUGUMIZI akiongea UKAFUNIKA KIFUU basi hataweza kuongea na atabakia anagugumia mpaka ukifunue.
6. Ukikutana na ALBINO temea mate KIFUANI/KITOVUNI kwako usipofanya hivyo nawe utakuja KUZAA kama huyo.
7. Tuliamini pia Albino HAWAFI, bali wanapotea tu Kimiujiza.
8. Ukihadithia HADITHI MCHANA basi utaota MKIA
9. Siku JUA likiwaka na MVUA kunyeesha basi sikuo hiyo SIMBA jike porini anazaa!
Na kama kuna mpira siku hiyo na Yanga anacheza basi matokeo yatakuwa sare.
10. Siku UKING'OA JINO tupa juu ya PAA la nyumba KUNGURU akilichukua jino lako ndio litaota jingine.
11. Watoto wote WANANUNULIWA hospitali au Wanaokotwa BAHARINI.
12. KONDOO ukimfunga kitambaa chekundu anapigana na radio iliyokua karibu yake.
13. Tuliamini kuwa wagonjwa wote wa akili (Vichaa na wendawazimu) kabla ya kuugua walikuwa ni WASOMI WAKUBWA SANA.
14. Ukiwa unanyonyoa KUKU/BATA usizungumze, ukizungumza tu MANYOYA yanarudi upya.
15. Tukiamini kuwa MAJAMBAZI ni Watu wenye sura ZINAZOTISHA, kama sura haitishi, basi sio Jambazi.
16. Ukitaka KUPIGANA na mwenzio ili kupata uhakika, unachora MSTARI na kumwambia ...KAMA WEWE MWAMBA VUKA HUO MSTARI, kitendo cha yeye kuvuka tu, ni ndundi tu, hakuna kuuliza mara ya pili.
Kama pembeni kuna mashabiki wapambe, watachota mchanga mkononi na kukwambia kama kweli unataka kupigana puta mchanga huu, kisha aliyekupa mchanga atakunja ngumi na kukwambia tia kidole hapa (Katikati ya kiganja chake), kitendo hicho tulikichukulia kama tusi kubwa sana na mtu kama kama kafanya hivyo basi kweli kadhamiria ugomvi na mtazipiga tu.
17. Kama unaangalia mpira na ukaona timu yako inataka kufungwa au ni pira wa penati, basi tuliamini UKIZIBANA SEHEMU ZAKO BINAFSI yule mpigaji penati atakosa na kupiga nje au juu au kipa atadaka.
18. Kama umekaa na UMENYOOSHA MIGUU, ikatokea mtu AMEKURUKA, basi atatakiwa arudi na kukuruka tena, hasipo fanya hivyo atasababisha yule aliyerukwa kutokukua yaani hato ongezeka kimo atabakia kuwa andunje.
19. kama mmekaa na mmoja wenu KASIMAMA, tuliokaa wote tuliamini yule aliyekaa atakuwa ANATUNYONYA DAMU.
Utasikia tu mtu analalamika, ebu kaa chini usitunyonye damu.
20. Watoto wa Kike walikuwa wanaweka mdudu (Fukufuku) kwenye manyonyo yao, wakiamini kuwa yatakuwa makubwa... Yule mdudu ilikuwa ukimuimbia, sikumbuki vizuri ule wimbo, ila ulikuwa kama hivi... Fukufuku toka nitakupa maji ya sukari... au Fukufuku toka baba yako kaja... (Na ajabu wale wadudu ukiwaimbia walikuwa wanatoka).
21. Kuna ndege wa Pwani, tukiwajua kwa jina la Yangeyange (Bata Maji) walikuwa weupe, wakiruka tukiwaimbia... Yangeyange tupe kucha nyeupe... Tukiamini kuwa kwa kuimba uko tutakuwa na kucha Nyeupe.
Ongeza Mengine Unayo Yakumbuka...