Kweli vs halisi!

Kweli vs halisi!

Joined
Mar 23, 2025
Posts
16
Reaction score
8
Ulimwengu! Umeacha wanadamu wenye macho hafifu ya ndani waendelea kuishi uhalisia badala ya ukweli!
Hivyo maisha yamekuwa ni kama bahati nasibu!aliyesifika Leo kwa kutafuta heshima Mali na fedha ndiye anayetajiwa kesho kuwa marehemu! Yaani baada ya juhudi zote muda unabakia kuwa mwamuzi wa nani abaki nani aondoke!

Hapa ukaidi,na jeuri vinawekwa pembeni kwani fumbo hili la kifo halina fundi wala mjuzi wote ni kama bendera kumfuata upepo. Kama Plato, Aristotle, Karl Max, na wengi walio uchunguza uhalisia wasifikie kujua ukweli.
Leo tuna fundi mfano Elon Musk ajabu naye ana maswali anawaza atamuuliza nani? Ni muda? Au Kuna nguvu kubwa mbali ya Muda.

Ukiondoa ujinga,uliosawasawa na upumbavu.usiku ukiwa nje peke Yako utakatazama angani utajua kuwa vitu hivi havikutokea kwa ujinga wa nadharia ya big bang!

Unauliza je sayansi ni uchawi au uchawi ni sayansi.Twende CERN(mpakani mwa uswisi na ufaransa) wanasayansi Hawa magwiji wanateketeza matrilion ya pesa ambazo zingesaidia wasiosadiwa yaani wakazi wote wa Dunia.

Mbele ya kituo hiki cha kustaabisha unakaribishwa na sanamu ya Shiva Mungu wa kihindi ambaye ni kazi yake ni kuharibu. Ujinga ulio mwingi sana hauwezi kuwa ni upumbavu.unawezaje kutumia nguvu nyingi kumharibu usiokijua kwa kina kwa Nia ya kuitengeneza tena. Ni ajabu. kumbe tunaishi halisi sio Kweli.
 
Back
Top Bottom