Kweli usije ukamjaribu mtu ktk kitu kinachoitwa pesa

fizo talent

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
2,257
3,882
Naam wakuu habari za weekend,

Ktk maisha hususani haya ya kibongo ukiamua kutumia pesa km kipimio cha kumpimia mtu,hasa ukitaka kujua yupi ni mwaminifu na yupi si mwaminifu haki ya nani kwenye watu mia unaweza ukampata mmoja ama usimpate kabisa.

Habari ipo hivi ktk eneo nililopo nafanya biashara fulani hunikutanisha na watu tofauti tofauti,ambao kwa mazoea tu ya kuja ofisini unakuta mmeshazoeana na muda mwingine mnapiga stori mbili tatu za kubadilishana mitazamo ya kimawazo na kimaisha.Bila kusahau zile stori za kusogeza masaa kiba na mondi mkali nani,mo na bakhresa mwenye mkwanja nani,messi na ronaldo ili mradi masaa yaende mwisho wa siku kila mtu anaenda kwao.

Niliambiwa na watu walioniwahi kufanya biashara kabla yangu kua epuka kukopesha mtu hela ambayo unajua km asipokulipa itakuyumbisha ktk biashara yako hivyo nami nililizingatia.Hivyo ikawa mwisho wangu wa kumkopesha au kumuamini mtu achukue bidhaa yangu halafu ataleta baadae ulikua hauzidi elf kumi.Hapa nilipoteza watu maana mwingine anahama kabisa kisa buku tatu ama elf kumi mwingine hata buku.


Baada ya kipindi fulani nami nikaanza kuwajaribu unaowajua hawa ni watu wako wa karibu kabisa na unawaona kwa upeo wa macho ni watu smart.Siku ya kwanza jamaa mmoja mtu smart sana hata kwa ushauri anaokupa nikamzidishia chenji kwa maksudi kabisa alitoa elf tano kwa kitu cha elf tatu badala nimrudishie elf mbili nikamrudishia buku saba, baada ya kumrudishia jamaa akazuga km dakika tano akijifanya anapiga stori mara huyo kaondoka zake hakurudisha.

Mwingine huyu ni mshkaji wangu sana sometimes hata akikwama huwa namuungia siku hiyo kuna mtu alimtuma kitu akaja ofisini alipewa elf kumi kwa kitu cha elf tisa hapo aliniuliza na bei kabla tena nakiuzaga elf kumi baada ya kulialia nikamuuzia kwa buku tisa,nae nikajifanya nimejichanganya badala ya kumrudishia elfu moja nikampa elf tisa na ile bidhaa ha ha ha huwezi amini jamaa alisepa mazima,ile siku hakuja tena ofisini basi siku ya pili nakaamua nimwambie jana nilijichanganya nilikupa elf tisa huwezi amini jamaa alikataa kabisa na uswahiba ukaisha siku ile kwa kuniona mimi snitch eti simuamini hela ndogo km ile itampeleka wapi.Nikimkumbuka mpaka wa leo huwa naishia kusema achana na kitu kinachoitwa pesa na nimefanya hivyo kwa watu takribani watano lakini sikubahatika kurudishiwa hata mara moja mwingine hata buku anaichikichia.Sometimes nawaza ndio vyuma vya Jiwe vimekaza namna hii ila wamenifundisha kua kwenye pesa usimuamini mtu.Ila lengo la kufanya hili ni kujipa tahadhari kabla maana unaweza kua na mtu na kusema unamuamini akakueleza tatizo na wabongo tulivyo unaweza ukamuamini tu na unaweza ukamkopesha mtu hela ndefu halafu mtu akatembea mazima.Nilichogundua kuaminiana hakupo ktk kitu kinachoitwa pesa na sio km sikopeshi ila mambo inabidi yawe kisheria na sio kishkaji.
Weekend njema.
 
Inabidi ujitathimini mwenyewe, waswahili wana mseme wao " ndege wafananao huruka pamoja". Ukiona marafiki/watu unao waamini wana chembe za kutokuwa wa aminifu kwenye pesa jiangalie sana na wewe yawezekana uko hivo hivo.

Wapo watu wengi tu waaminifu kwenye pesa, sasa kwasababu haujakutana nao haimaanishi hawapo.
 
Inabidi ujitathimini mwenyewe, waswahili wana mseme wao " ndege wafananao huruka pamoja". Ukiona marafiki/watu unao waamini wana chembe za kutokuwa wa aminifu kwenye pesa jiangalie sana na wewe yawezekana uko hivo hivo.

Wapo watu wengi tu waaminifu kwenye pesa, sasa kwasababu haujakutana nao haimaanishi hawapo.
fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom