Kweli Tanzania Shamba la BIBI

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
OFISA wa Wanyamapori Ufilipino anatuhumiwa kuiba pembe za ndovu zinazosadikiwa kuwa sehemu ya nyara zilizoingizwa nchini humo kwa magendo kutoka Tanzania, ambazo zinaendelea kuhifadhiwa huku Serikali nchini ikiwa katika maandalizi ya huko kufanya uchunguzi.

Taarifa kuhusu wizi huo, zilitolewa jana katika baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zikitaja kwamba jumla ya kilo 794 za pembe zenye thamani ya dola 80,000 za Marekani zimeibwa katika ghala zilikohifadhiwa.

Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) lilimkariri Mkuu wa Idara ya Wanyamapori wa Ufilipino, Josie de Leon, akisema wafanyakazi wenzake na ofisa huyo anayetuhumiwa kuiba pembe za ndovu, walimhisi kutokana na matumizi yake kuwa makubwa.

Taarifa zilisema baada ya wafanyakazi wenzake kuchunguza pembe zilizohifadhiwa ndani ya ghala la serikali, waligundua kwamba kilo 794 zimepungua. Vyombo hivyo vya nje vilikwenda mbali kwa kusema ujumbe wa Tanzania uko mbioni kwenda Manila, wiki ijayo kukagua pembe hizo na kubaini kama ni za Tanzania kwa lengo la kuzirejesha nchini.

Hata hivyo, akizungumza na HabariLeo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Tarimo Erasmus, alisema Tanzania ilianza kushughulikia taratibu za kwenda si tu Ufilipino, bali pia Vietnam tangu mwaka jana, kuchunguza pembe hizo.

Alisema si kwamba wanakwenda kutokana na taarifa hizo za Ofisa wa Ufilipino kuiba pembe. Erasmus ambaye hata hivyo alisisitiza kwamba pembe zilizokamatwa na kuendelea kuhifadhiwa Ufilipino na Vietnam, inawezekana zilipitia nchini na si kwamba ziliibwa kwenye ghala la Tanzania, alisema tangu Aprili mwaka jana, walikuwa katika maandalizi ya kwenda huko, lakini taratibu hazijakamilika. “Bado hawajaondoka na tiketi hazijakamilika,” alisema.

“Hatujapoteza meno yoyote kwenye stoo zetu. Inasemekana yamepitia Tanzania si kwamba yameibwa kwenye stoo zetu,” alisema Mkurugenzi huyo na kutaja baadhi ya nchi ambazo meno hayo inawezekana kutoka kuwa ni Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.

Alisema kikosi kinachotarajiwa kwenda kufanya uchunguzi kinahusisha maofisa kutoka ofisi yake, Polisi wa Kimataifa (Interpol), ofisi ya Mwanasheria Mkuu na mwakilishi chini ya Mkataba wa Lusaka.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Machi mwaka jana, nchini Vietnam zilikamatwa pembe kilo 6,232 na Ufilipino zilikamatwa kilo 3,346. Wakati huohuo, Aprili mwaka jana, Ufilipino zilikamatwa kilo 1,483 na Vietnam kilo 3,000 ambazo inasadikiwa, ndizo sehemu yake imeibwa na Ofisa wa Ufilipino aliyetoweka Februari 26 mwaka huu baada ya kugundulika.

Anaendelea kusakwa na vyombo vya Dola nchini kwake. Kwa mujibu wa AFP, pembe zilizoibwa, ni sehemu ya pembe zilizokamatwa Juni mwaka jana, bandarini Manila.

Wataalamu wa masuala ya wanyamapori wanasema takribani tembo 38,000 katika Afrika huuawa kila mwaka kwa lengo la kujipatia pembe. Hao ni sehemu ya tembo 500,000 wanaokadiriwa kuwapo.

Pembe za ndovu ni nyara ambazo zinatajwa kuwa na matumizi mengi ikiwamo kutengeneza urembo, vinyago na vigae hususan Asia.

Julai mwaka jana, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela (CCM) alifikisha bungeni suala la wizi wa pembe za ndovu zilizosafirishwa kama taka rejeshwa za plastiki, akitaka uchunguzi ufanyike dhidi ya kontena mbili zilizosafirishwa kwenda nchi hizo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, alitolea ufafanuzi akisema upelelezi unafanywa na timu ya wataalamu yenye ujuzi wa kutosha. Mwangunga alikiri kuwa kati ya Machi na Mei mwaka jana, wizara yake ilipokea taarifa kupitia Interpol-NCB-Dar es Salaam, kuwa kontena hizo zilikutwa na meno ya tembo zikitokea Dar es Salaam na zilikamatwa Ufilipino na Vietnam
 
Mkuu nilishaitoa hii tarehe 2nd Dec, watu wakasema nithibitishe- nafikiri wakisoma ulichoandika tutawasaidia.



" Tanzania ni shamba la bibi
ELNIN0
user_online.gif
2nd December 2009, 11:28 AM
Imefikia hatua Tanzania yetu nchi yenye mali nyingi na vivutio vya kitalii inaitwa shamba la bibi, cha kujiuliza kweli tumeamua kuiita hivyo? je unavyoimba wimbo wetu wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wotee ni unafiki tu? mimi binafsi naumia sana nikisikia kauli hii ila huwa sina pa kwenda kushitaki.
__________________
 
Back
Top Bottom