Jamani wana JF ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, Ile siku mkuu alipokuwa anazindua ile barabara ya kutoka mwenge kwenda tegeta ya kilometa 13, kuna watu walimchomekea kwamba eti pale jangwani pameuzwa, na mkuu kama kawaida yake, bila kufanya utafiti akaongea moja kwa moja, namnukuu. " nimepita pale jangwani nimeona kuna mtu amejenga uzio pale na nimeambiwa ameuziwa, sasa nawaagiza wale waliomuuzia wamrudishie pesa zake na ule uzio ubomolewe mara moja"mwisho wa kumnukuu. UKWELI WA MAMBO PALE JANGWANI. Kama kawaida yangu mimi ni mtafiti makini pengine kuliko yeyote. Pale kuna mradi wa kituo cha mabasi yanayokwenda kwa kasi, ambao uko chini ya TANROAD. na kampuni ya Kichina ya CCECC Ndiyo walioshinda ile tenda, na fedha za mradi tayari zilishatolewa. na pia siyo jangwani pote kama alivyosema mkuu, mradi unahusu kisehemu kidogo cha pale jangwani, SWALI. Kama kweli mkuu wa nchi hawasiliani na wizara zake na mawaziri wake ili kujua juu ya miradi ya serikali ili apate ukweli na badala yake anawasiliana na wapambe wake ambao hawajui lolote linaloendelea zaidi ya kutafuta majungu na kuyapeleka kwa msikiliza majungu ili wajifurahishe na kutafuta umaarufu, Kweli tutafika?