Kweli sasa nimeamini, mkuu anaendesha nchi kwa majungu na siyo utashi

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Jamani wana JF ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, Ile siku mkuu alipokuwa anazindua ile barabara ya kutoka mwenge kwenda tegeta ya kilometa 13, kuna watu walimchomekea kwamba eti pale jangwani pameuzwa, na mkuu kama kawaida yake, bila kufanya utafiti akaongea moja kwa moja, namnukuu. " nimepita pale jangwani nimeona kuna mtu amejenga uzio pale na nimeambiwa ameuziwa, sasa nawaagiza wale waliomuuzia wamrudishie pesa zake na ule uzio ubomolewe mara moja"mwisho wa kumnukuu. UKWELI WA MAMBO PALE JANGWANI. Kama kawaida yangu mimi ni mtafiti makini pengine kuliko yeyote. Pale kuna mradi wa kituo cha mabasi yanayokwenda kwa kasi, ambao uko chini ya TANROAD. na kampuni ya Kichina ya CCECC Ndiyo walioshinda ile tenda, na fedha za mradi tayari zilishatolewa. na pia siyo jangwani pote kama alivyosema mkuu, mradi unahusu kisehemu kidogo cha pale jangwani, SWALI. Kama kweli mkuu wa nchi hawasiliani na wizara zake na mawaziri wake ili kujua juu ya miradi ya serikali ili apate ukweli na badala yake anawasiliana na wapambe wake ambao hawajui lolote linaloendelea zaidi ya kutafuta majungu na kuyapeleka kwa msikiliza majungu ili wajifurahishe na kutafuta umaarufu, Kweli tutafika?
 
wewe ndio huna data na ndio unaleta majungu, kaa kimya kama hunachakuandika.
 
Duuh ndugu hyo kali na inasikitisha kuona aina ya mkuu wa taifa letu!hapo ndo utajiuliza hao wazee wa intelejinsia na usalama wa taifa wanafanya kazi gani?wkt huohuo wana bajeti kubwa tena ambazo hazihojiwi hata bungeni,tunahitaji nguvu ya umma ifanye kazi kweli kweli
 
JK mwenyewe ndo bingwa wa majungu sasa atakuwaje hafanyi kazi kwa majungu???
 
JK mwenyewe ndo bingwa wa majungu sasa atakuwaje hafanyi kazi kwa majungu???

Yaani wizara nzima wameshangaa jinsi jamaa anavyoendesha mambo nyeti ya nchi kimajungu badala ya utendaji. kila mtua anatamani kuacha kazi
 
Rais amedanganywa UKWELI ni kuwa pale hapajauzwa mkandarasi amepewa kibali na manispaa ya Ilala kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi. alieleta post yupo sawa. Ndio maana uzio bado upo.
 
Yaani wizara nzima wameshangaa jinsi jamaa anavyoendesha mambo nyeti ya nchi kimajungu badala ya utendaji. kila mtua anatamani kuacha kazi

Poleni. hata hivyo kwa vile hatukumchagua bali alituchakachulia kura zetu, tutasubiri hadi nguvu ya umma itakapomwondoa.
 
Rais amedanganywa UKWELI ni kuwa pale hapajauzwa mkandarasi amepewa kibali na manispaa ya Ilala kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi. alieleta post yupo sawa. Ndio maana uzio bado upo.

sasa ndugu yangu ebu fikiri tu ktk hali ya kawaida, hiyo inatoa picha gani kwa jamii au kwa wizara inayohusika, lengo lake ilikuwa kumharibia magufuli ili ionekane machoni mwa watu kuwa hayuko makini. nachukia utawala wa namna hii daima
 
Hivi gov't haina means nzuri za escalations na upatikanaji wa apropriate reports mpk kutegemea wapambe? Hivi hawana internal briefings mpk kupayuka hadharani na kujishushia hadhi? If ths z true...thn poor Tanzania.
 
sasa hivi ktk utafiti wangu hakuna wizara hata moja inayomzungumzia vizuri, kwa kweli amepoteza umaarufu, yaani kila mtu mpaka yule mfagiaji wa ofisi anakwambia waziwazi kuwa jamaa nchi imemshinda
 
utafiti mwingine unaonyesha pia tangu hii nchi izaliwe haijawahi kumpata waziri mkuu zoba kama tuliye naye sasa maana ameshindwa kabisa kumsaidia JK
 
Tatizo JK hapapendi Jangwani kabisa.......maana alipiga mwereka mara mbili 2005 na 2010...wakati wa kampeni
 
Tatizo JK hapapendi Jangwani kabisa.......maana alipiga mwereka mara mbili 2005 na 2010...wakati wa kampeni

yeye anadai pale ni kwa ajili ya viwanja vya michezo, lakini kwa mtu anayepajua jangwani pale ni nyumbani pa mazalia ya mbu wa DSM.Kama kweli alikuwa na nia ya kupafanya pawe viwanja vya michezo, alitakiwa apatengeneze, lakini siyo ktk muonekano wa sasa. hii ni aibu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom