Kweli nimeamini kuna wanawake wagumu

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Siamini kilichotokoea jana, kuna mwanamke amenizungusha sana mwezi wa3 huu, nikaona labda nitumie Nguvu ya Shilingi ya Kitanzania mambo yatakaa sawa, nikamualika Lunch akakubali, nikaona nisiongee sana, nikaziachia chips mayai na kuku ziongee, nikaiachia Saint Anna wine iongee, Nikayaachia maji ya Kilimanjaro ya Baridi yaongee.

Sikutaka kuongea kabisa siku hiyo maana nilishaongea sana bila mafanikio, Nikaamua niiachie pesa ya kitanzania iongee, baada ya kula tukiwa tunapiga story nikaweka Laki5 mezani nikamwabia hiyo itamsaidia kimatumizi.

Cha ajabu nayo alikataa, nikajua labda anaona aibu nikachukua pochi yake nimuwekee ndio akawa mkaliii "HUWEZI KUNIRUBUNI NISHAKWAMBIA SIPO TAYARII! " akaita bodaboda akaondoka zake na laki5 akaiacha.

Kuna wanawake wa ajabu sana.
 
hii stori yako uminikumbusha kuna majamaa walikuwa na USD nyingi sana walipata ajali kijiji flani.zile dola wanakijiji wakaziokota na kwenda kuzibandika ukutani magetoni kwao.ilikuwa karibu dola laki 3
 
Back
Top Bottom