Kweli Ndugai umelewa madaraka

Kweli Ndugai umelewa madaraka

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,150
Jamani kweli huyu naibu spika Jon Ndugai kwa kauli zake leo amelewa madaraka, mapema baada ya kipindi cha maswali na majibu, akiwa katika kutangaza matangazo mbalimbali, amewalaumu wapinzani pamoja na mambo mengine anasema wamekuwa wakilalamika kuwa kiti cha spika kinaupendeleo wakati si kweli.

Anasema robo 3 ya wabunge wote ni wa CCM na robo tu ni wa upinzani lakini kwenye kipindi cha maswli na majibu utaona kabisa kuwa wapinzani ni wengi kuliko wale wa CCM, na anasema anaweza amshawishi spika wabadili utaratibu ili kila wabunge 4 wanaouliza maswali 1 tu atoke upinzani. Binafsi nadhani Ndungai anataka kuzima hoja, hoja ya wapinzani na wananchi kwa ujumla, ni kwamba maamuzi ya spika yanakuwa yanapendela upande mmoja na sio uwiano anaousema wa kuuliza maswli.

Pili ndugai afahamu kuwa watanzania tunajua wabunge wa CCM walio wengi hawaibani serikali bali kuisupport serikali kwa kila kitu hvyo huwezi ukawaona wakiuliza maswali kama wapinzani.

Vilevile Ndugai amewaponda waandishi wa habari, kuwa wanatakiwa wariport habari zao kwa ufasaha, anasema unaposema wabunge wametoka nje ya bunge wakati wabunge wametoka nje ya ukumbi tu na wapo maeneo ya bunge(hawajatoka kwenye geti la bunge0 na ameendea kwa kusema mbunge mmoja anaweza toka, wabunge kwa makundi nk. Wasiwasi wangu ni kwamba kama na wenyewe huu ni utaratibu basi ni wa kipumbavu, kwamba wabunge wanaweza wakatoka nje ya ukumbi provided kwamba hawajatoka nje ya geti!

Je, Ndunngai, anaweza akawa nje ya darasa chuoni halafu mw. alete quiz aseme alikuwepo darasani kwa kuwa hakuwa nje ya geti la chuo?
 
Kama wanakusudia hivyo, believe me bunge litakosa kipindi cha maswali na majibu? The BIG question ambayo Ndugai angejiuliza pamoja na WABUNGE wa UPINZANI kuwa ROBO, kwanini wao ndiyo wanauliza/wanaleta maswali mengi kuliko wenzao wa CCM ambao wako ROBO TATU?

Hizi akili za mbuni kuzika kichwa mchangani ilihali mwili wote ukiwa nje, zitawafikisha wapi CCM? BTW, Ndugai akumbushwe kuwa sasa hivi tuko kwenye mchakato wa katiba mpya. Inaelekea bado yuko kwenye usingizi wa PONO.
 
Kilaza kweli huyo Job, wenye hyo robo tatu anahesabu na Mawaziri na manaibu waziri, pamoja na maspika? Pia maCCM yanayolala.. Komba et,

Naona Job leo ndio kakiri rasm kuwa uwezo wa mbunge mmoja wa upinzani, ni sana na mabunge ya maCCM manne... Well done Job
 
Dr si unajua athari za kutegemea akili za waganga wa lienyeji ni kama kuwa na kijeti kwenye chumba cha mtihani,hua akili inalala nasikitika sana viongozi wa Tz kuendelea kudanganya na waganga wa kienyeji hawana akili walizoumbiwa tena,na tafadhali fatilia hata masuala yao nyumbani lazima yatakuwa ovyo,ujinga wa shetani,ushauri wangu kwa kuwa bado wako madarakani tuwaombee kwa Mungu wapone kwa sababu maamuzi ya kishetani ni kututesa sisi na ndio yanayoendelea,....
 
Anamaanisha Wabunge a upinzani japo kuwa wapo robo ndio wanafanya kazi kubwa kuliko wa CCM? Ndugai na Makinda mwisho wao utafika tu
 
Ndugai amekiri kuwa mbunge 1 wa upinzani(sio cuf)ni sawa na wabunge 1oo wa nyinyiem.juzi mbatia kawashinda nyinyiem wote
 
Ndiyo tatizo kubwa tulilonalo TZ ya kuwa na watu kama hao katika ngazi mbalimbali zilizo nyeti serikalini, bunge nk.
 
Ajue vyote hivyo vina mwisho na akijakufikiri kwa kina atajizarau
 
Ajue vyote hivyo vina mwisho na akijakufikiri kwa kina atajizarau

Ndugai anatakiwa anatakiwa achague moja, ama awaruhusu wabunge waongee bungeni Dodoma, au wabunge hao waongee huku mtaani kwa wapiga kura. Na kwa speed ya sasa toka kwa Ngudai iko siku watu watatembezwa mitaani kama vikojozi sugu!
 
Job ndugai, amezeeka kabla ya uzee halisi, ukimlinganisha na kingunge kwa uzee, afadhali ya mzee kingunge.
 
Mburula, anahitaji matiba kwenye ile hospitali hapo dodoma, nafikiri inaitwa milabwe.
 
Hii nizaidi ya ulevi, hizi ni tabia za kishirikina ambazo unaweza kumuangamiza mwezako kwasababu anajituma na ana maendeleo wakati na wewe fursa unazo lakini uvivu umekujaa. Mnyika kaja na hoja kwa wakazi wote wa DSM, Ndungai anatumia nguvu kuipinga hizi ni tabia za kishirikina.
 
Ndugu yangu bado unapoteza muda na hawa watu??acha waendelee kufanya chochote watakacho ila mi nimeshaweka kadi yangu ya kupigia kura karibu sana na mapema kwa ajili ya kuadhibu hawa watu 2015.Ndiyo maana nasema hata chadema iwe na sera mbovu kiasi gani siwezi kuiacha coz sioni chama kingine zaidi yake,,,kushabikia ccm ni bora hata ukajiunge na PPT MAENDELEO vyama visivyojulikana
 
Back
Top Bottom