Kweli ndoa ndoano

'Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye MPUMBAVU huibomoa kwa mikono yake MWENYEWE'
 
dagaa pole my dear!
ila ngoja nikusaidie kitu,mi huwa ushauri wangu unakwenda na maswali!
1.mume wako ulikuruhusu kwenda picnic?
2.mume wako anajua kuwa hakuridhishi?
3.security ya mume wako kiuchumi iko vipi?
4.huwa mnasali kama wanandoa?
4.mtoto na umri gani?mlikubaliana kuacha kufanya tendo?
5.hebu ielelezee ndoa yako ykama nikiiweka kwenye makundi yafuatayo
A.NDOA YANGU NI NZURI NAIPENDA NA NIPO TAYARI KUIFANYA IWE BORA
B.NDOA YANGU YA KAWAIDA NA KILA KITU KIPO VILE NDOA INAPASWA KUWA
C.NDOA YANGU IPO KWA SABABU NINAPASWA KUOLEWA
D.SIIPENDI NDOA YANGU
 



sasa hapo brother anatuangusha wenzake
kama mali yake anaiendea kwa pupa na kuisusa alikua anafikiri mkewe afanye maamuz gani??
Af sasa jazba haisadii,kama anaona mkewe anabana hizo ni suala la kuongea tuh


pipi ya kijiti aifanyie check up iyo...
 
Aisee usije ukajaribu kumwambia kwamba hakuandai vizuri hapo ndio utaharibu kabisaa bora ukiwa ktk majombozi ndio umwambie bado kwanza usiingize mshedede tuendelee na foreplay...
MSHEDEDE? Teh teh teh teh !
 

we una matatizo!!, me mke wangu akinifanyia haya nampa taraka kesho yake!! mtoto wa 1.6 yrs unasema bado mdogo??? ha ha ha wachekesha kweli.. wakati huku kwetu uswahilini mtu ashazaa mwingine..!!!!! nahisi hukufanyiwa kitchen party
 
pole sana mdogo wangu hata cha kushauri sina ila busara unazo,ongeza maombi ili kuinusuru familia yako
 
Pole sana, ngoja nikuitie kina gfsonwin, snowhite, nyumba kubwa, Nyamayao, King'asti na wengine wakushauri.

Cha kwangu, ni mjenge tabia ya kusali pamoja kabla ya kulala. Pombe mpunguze ikiwezekana muache!

mhh, kazi kweli kweli, makubwa kwa madogo katika hii sector, anamyima unyumba kisa ananyonyesha? hata bwana but mambo ya kulia lia mbele ya mume/bf kisa mmekwaruzana ni ya kishamba, unakauka kwa wakati ule ukitoka hapo kajililie kivyako, mie msukuma anaonaga chozi langu kwenye matatizo tu...hastahili kunikera mpaka nilie, khaa kwani shs ngapi?
 
Kwanza wewe haujapigwa, toka mke wangu anibanie miezi sita eti sababu ya kuzaa, nshawatoa akili kabisi, tena kwa sababu za kijinga kabisa eti tutabemenda mtoto, tena wewe!! wewe!!
 
Leo nataka niwaulize wale wataaluma, na hata wana ndoa
Hivi kuna haja ya kuangalia/kuzingatia makabila wakati unaoa au kuolewa?. Je uwezo wa kifedha ni muhmu kuzingatiwa kabla ya kuoa au kuolewa? Je Elimu inaweza kuwa na nafasi kwenye ndoa? umaarufu na uzuri unanafasi gani kwenye ndoa? Haya maswali ni suluhisho kwenye hili tatizo maana chanzo ya kinaweza kuwa, Familia, kipato, uzuri/umarufu nk
wakatabahu!
 

Napenda vimaneno vyako vya kiinglish asante sana mfano eti GO WITH THE FLOW
 
.....................Mwanzo nilisisimka na kujua kwamba jamaa yako kawa chizi...... niliendelea kusoma kumbe hayo yote unayataka mwenyewe...... aidha kuna maelekezo mlitakiwa kupewa wakati wa ndoa yenu ... hamkupewa.... kwa nini unamnyima? kumnyima ni kosa kama haelewi maana ya kumbemenda mtoto yaani kumzalia mdogo wake wakati yeye bado mdogo sana....si vizuri ... lakini hili mlitakiwa kuelezwa mapema na waliowasindikiza katika harusi yenu, aidha mashangazi wa pande zote mbili walitakiwa kuwafunda... inatakiwa mpangie siku za kukutana kuzingatia dangerous day na safe day kwa kupata au kukwepa mimba zisizokuwa na mpangilio... mfuate shangazi yake mwambie kama wale ma best wa harusi yenu hawakuwaambia hilo.... haina haja ya kugombana wala kununiana... pole sana........
 

Dada nafikiri majibu yako ni hiki kipengere kidogo nilichokichukua kutoka kati ya yale mawazo yako, ila pakubwa jikite hapo kwenye RED.
 


Sijaelewa hapa naingiaje kwenye huu uzi
au ndo kusema umenimiss saana sio? lol
 

Aisee, kumbe ndo mnavyofikiria?? Basi kazi ipo.
Wanawake nasi tuna haki ya kufurahia tendo la ndoa, so isichukuliwe kuwa tunawanyima wanaume maana nasisi tunakosa pia. Dada Dagaa umeshauriwa vizuri tu humu ndani, kila la kheri kwenye ndoa yako.
 
Wewe unastahili kipigo mwaka 1 na miezi 7 bado unamnyima kwa kisingizio cha mtoto mdogo.Unachekesha wewe mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…