Kweli nchi sasa imeoza!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli nchi sasa imeoza!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maarifa, Oct 28, 2008.

 1. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,873
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Samahania sana kama mtakuwa tayari mmeanza kuichangia article hiyo niliyodesa kutoka IPPMEDIA. Baada ya kuisoma hadi mwisho nilibakia na maswali mengi yasiyo na majibu. Ingawa mahitimisho yangu ni kuwa sasa si ufisadi tu bali sasa nchi imeoza kwa maana all systems zimekufa.

  Kashfa ya mwaka Baraza la Mitihani

  2008-10-27 13:57:26
  Na Waandishi Wetu


  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limesambaza vyeti bandia vya matokeo ya kidato cha nne mwaka jana, (result slip) katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

  Wanafunzi walioathirika na hatua hiyo, ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka jana, na baadhi yao wameanza kupata misukosuko, ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa madai ya kughushi.

  Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Magomeni, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Rehema Mlata, alisema mtoto wake, Alexander Gundula (22), hivi sasa yupo mahabusu mjini Mbeya, kwa kosa lililofanywa na NECTA, kusambaza vyeti hivyo.

  Alexander alikuwa miongoni mwa askari wanafunzi katika Chuo cha Magereza Kiwira, mkoani Mbeya.

  Mlata, alisema Alexander alisoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari Azania, mkoani Dar es Salaam kati ya mwaka 2004 hadi 2007.

  Uongozi wa Azania, kupitia waraka wake wa Oktoba 3, mwaka huu kwa Mkuu wa Mafunzo, Chuo cha Magereza Kiwira, umethibitisha mwanafunzi huyo kusoma katika shule hiyo.

  Mlata alisema Alexander alichukua result slip shuleni hapo Februari mwaka huu, kwa ajili ya kujiunga na Magereza, na kwamba alifanikiwa kuanza mafunzo chuoni hapo.

  Alisema Septemba mwaka huu, Alexander alikamatwa mjini Mbeya na kufikishwa mahakamani, akidaiwa kughushi result slip yenye namba S0101/0032, aliyopewa na uongozi wa Azania.

  Ilidaiwa kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Magereza kuthibitishiwa na NECTA, kuwa cheti hicho kilikuwa na kasoro zilizokifanya kisifanane na vingine vilivyotolewa mwaka jana, hivyo kuamua kwamba kilikuwa cha kughushi.

  Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Magereza, ilimwandikia barua Alexander, yenye namba HQC.58/X1/287, ikielezea kuachishwa mafunzo kutokana na kosa la kughushi cheti hicho, na hivyo kukosa sifa ya kuajiriwa.

  Kufuatia uhakiki wa ajira uliofanywa na kamati ya uhakiki kutoka Makao Makuu ya Magereza kuanzia tarehe 31 Agosti mwaka 2008 hadi Septemba mwaka huu, imedhihirika kuwa cheti cha kufuzu masomo ni cha kughushi hivyo moja kwa moja unapoteza sifa za kuajiriwa kama askari Magereza, ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza, E.M. Nkuku.

  Mlata alisema alikwenda kuonana na uongozi wa Magereza jijini Dar es Salaam, na kujibiwa kwamba uthibitisho kwamba cheti hicho kilikuwa cha kughushi, ulitolewa na NECTA.

  Mzazi huyo alifanikiwa kupata nyaraka kadhaa zinazothibitisha kuwa result slip hiyo, ilitolewa katika Shule ya Sekondari Azania.

  Kwa upande wake, uongozi wa Azania uliandika barua tofauti, ikiwemo namba AZ/BMT/19, kwenda NECTA, ikieleza kuwa Alexander ni mwanafunzi halali wa shule hiyo na result slip husika ilikuwa halali na ilitolewa shuleni hapo.

  Lakini Magereza waliendelea na msimamo wao kwamba wamethibitishiwa na Baraza la Mitihani kuwa result slip hiyo ni feki, alisema.

  Mlata alionyesha barua ya Baraza kwenda Magereza inayotaka Alexander achukuliwe hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa wengine wenye kawaida ya kughushi.

  Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Azania, Benard Ngoze, alilithibitishia gazeti hili kuwa Alexander alikuwa mwanafunzi halali wa shule hiyo, na kwamba result slip iliyotolewa shuleni hapo ilitoka NECTA na si ya kughushi.

  Alisema vyeti hivyo vilipelekwa shuleni hapo na NECTA mwaka jana, na kwamba vijana wengi wanaokutwa navyo hivi sasa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

  ``Zile result slip walileta wenywe Baraza kwa dispatch na tukazipokea, wanafunzi walikuwa wakija kila mtu kwa wakati wake, wanalipia Sh. 5,000 na kuchukua, sasa wanaziruka wakati zimetoka kwao?`` alihoji.

  Alisema alishaandika barua mara kadhaa kwa uongozi wa Baraza la Mitihani na Magereza kuthibitisha kuwa result slip ya Alexander ilipatikana kihalali shuleni hapo, lakini inashangaza kuona bado wahusika wanaendelea kumtia msukosuko kijana huyo.

  Baada ya kugundua kuwa ni kweli hizo result slip zimetoka kwao, Baraza walichukua nyingine 17 zilizobaki hapa shuleni na walisema wanaenda kuwashughulikia watu wa idara ya uchapaji, kwamba walihusika na udanganyifu huo, alisema.

  Alisema inawezekana watu wa idara hiyo katika Baraza, waliuza result slips halisi na kisha kuchapisha za kughushi na kusambaza katika shule mbalimbali nchini.

  Walipokuja hapa tuliwaambia watu wa Baraza kuwa wanastahili kushtakiwa kwa kutengeneza vyeti bandia hata sisi tumeanza kuogopa, kama taasisi nyeti kama hii inafanya vitu vya ajabu kama hivi nani tutakayewaamini, alihoji Mwalimu Ngoze.

  Baraza hilo limekiri kutokea kosa hilo katika barua yake ya Oktoba 13, mwaka huu, ikiwa na kumbukumbu namba MTS.2/14/Vol.L.IV/65, ya kumwomba radhi Alexander kwa kosa lililofanyika.

  Uchunguzi katika kumbukumbu za Baraza la Mitihani Tanzania umeonyesha kuwa result slip ya Alexander Gundula ni sahihi.

  Tayari tumemwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza kumjulisha kuhusu uhalali wa result slip hiyo ambayo pia imerudishwa kwake tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, ilisema barua hiyo iliyosainiwa na Kaputa kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako.

  Ingawa Baraza hilo halikukiri moja kwa moja katika barua yake kuwa result slip hizo zilitolewa na Baraza hilo, maofisa wake waliokwenda shule ya Azania, walikiri kuwa zilitolewa na taasisi hiyo yenye jukumu la kuandaa mitihani nchini.

  Msemaji wa Magereza, Omari Mtiga, alisema uhakiki wa vyeti vya askari wanafunzi, ni mchakato wa kawaida unaofanywa na jeshi hilo.

  Mtiga aliyeahidi kulifutilia suala hilo kwa undani, alisema utaalamu wa kubaini ikiwa vyeti vilivyowasilishwa na wanafunzi ni sahihi ama vimeghushiwa, unafanywa na NECTA.

  Wakituambia kwamba cheti fulani kimeghushiwa, sisi tunaamini hivyo na hatua inayofuata ni kumfikisha mhusika katika vyombo vya sheria, alisema.

  Hata hivyo, Mtiga alionyesha kushangazwa na tukio hilo alilolifananisha na mchezo wa kuigiza, na kusema taarifa zaidi itatolewa leo.

  ``Njoo Jumatatu, mimi nitakuwa nimesafiri, lakini taarifa zaidi utazipata kwa huyu Kaziulaya, ni mmoja wa wasaidizi wangu,`` alisema.

  Kwa upande wake, Dk. Ndalichako hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, kwa madai kuwa halijui.

  ``Kuna maamuzi yanayofikiwa na wasaidizi wangu, naomba tuwasiliane kesho, nitakuwa nimelifuatilia na kukupa jibu, nipigie simu kabla hujaja ofisini kwangu,`` alisema.

  Hata hivyo, Nipashe ilipowasiliana naye kwa mujibu wa ahadi yake, Dk. Ndalichako alidai yupo kwenye mkutano, na baadaye alipopigiwa mara kadhaa, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila kupokewa.
  Taarifa nyingine zilizopatikana hivi punde, zilidai kuwa, Magereza imeagiza Alexander kuripoti chuoni hapo na kuendelea na mafunzo, baada ya barua ya NECTA kuthibitisha kuwa result slip aliyonayo imetolewa na Baraza hilo.

  Imeandaliwa na Mashaka Mgeta na Joseph Mwendapole

  SOURCE: Nipashe


  Je mpaka leo hii Huyu Dr Ndalichako bado anapata pay slip?
  Je mpaka leo hii hakuna aliyefikishwa mahamani?
  Huyu maskini kijana anaombwa radhi na kuambiwa arudi mafunzoni je hiyo tu inatosha? to what extent damage waliofanya katika maisha ya huyu kijana. NO ACCOUNTABILITY NOR RESPONSIBILITY JE TUTAFIKA JAMANI?
   
 2. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibu limeshapatikana baraza zima limeoza.....au wewe unaonaje?
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ni kwamba tumelogwa na mchawi wetu kafariki......when i'm thinking about this damn country i get sick......All i am thinking all the time is leaving this fu**** country its better to be somalian rather that Tanzanian......i'm pissed off folks iam soooooooooo fu**** tired of sikialing these BullShit!
   
 4. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,873
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana kuona vihiyo wanapeta na ili hali watu waliosotea credit wananyanyaswa. Hivi waziri mhusika na baraza la mitihani yuko wapi? mpaka leo hii hakuna tamko lolote la mitihani ku leak na at the same time vyeti sahihi vinaitwa bandia na bandia vinakuwa sahihi. Nina uhakika hata wizi wa mitihani Dr Ndalichako anahusika. Je mpaka leo hii karne ya 21 still data base ya sehemu nyeti kama barasa bado wafanyakazi wao wa IT ni vihiyo nanma hiyo? still trip kila leo!! Hata wabunge nao kimya!!! wot are they doing?
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  This is serious maana we are creating an ignorant state full of fools and when we realize it it is going to be too late to say we wish we knew!They govt should take measures to address this issue!
   
 6. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #6
  Oct 28, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dr. Ndalichako anahujumiwa jamani. Unajua hii nchi ukiwa strict sana,watu uliowakuta wanaanza kuharibu makusudi ili wakukomoe na uonekane hufanyi kazi.Tumsaidie huyu mama kuwafichua mafisadi waliopo pale baraza.
  Nikitolea mfano,kuna shule fulani iko Tabata,mkurugenzi wake ana mtu wake pale baraza.Huyo jamaa kila mwaka anapata mitihani na shule yake inafungiwa lakini bado inaendelea kuwepo.Tumsaidie huyu mama jamani,ana nia njema kabisa ila pale hana watu waaminifu.
   
 7. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,873
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Kwa namna nyingine ninaweza kukbaliana nawe. Lakini still Kama kweli ana nia ya kuweka mambo sawa then anasubiri nini ku act? Sometimes she has to be radical kama kweli anataka kunusuru hali ya 'uhiyo' Tanzania. Wanaotenda Uozo wako chini yake. whay can't she make them accountable? Sasa atasaidiwa vipi ana katika level gani more than yaliyotolewa hapo juu? Au mpaka aunde tume? Au anaogopa aliowakuta wamejikita na bagamoyo au ni mafisadi wa kutisha au wan mkono wa baraka toka juu(hawashikiki). Kama anaona ni vigumu ajiuzulu ili ampishe mtu mwenye unavu wa kusafisha baraza. kwani NECTA needs kusafishwa tena kwa DETO!!!! IT STINKS!! PUhhhhhh
   
 8. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima Mbele wakuu.... Yaani unajua hii issue ni mbaya na imekuwa inaendelea kutokea mwaka hadi mwaka... Mkuu MyTa.... umesema maneno ambayo ukiangalia kwa undani ni ugonjwa sugu hapa nyumbani, hii inatokana na kukitokea tatizo mahali tunabadilisha kichwa na kuacha mabega yaleyale (change the top cadre and leave the middle management) ambapo kufanyiwa shutuma kwa mtu mpya ni kawaida sana.... Zaidi ya hapo ni hili swala la kujuana (madaraka kwa kupeana) pia recycling ya baadhi ya watendaji/viongozi wetu...

  NECTA ndiyo inategemewa kututolea watendaji wa kesho, sasa kama mambo ni mpeni atese then we are in for a major trouble!! Waziri naona amesema kuna a major reform coming, swala ni kwamba atazingatia yaliyotajwa huko nyuma na wenzangu nami kuwekea msisitizo??

  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!
   
 9. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,959
  Likes Received: 20,296
  Trophy Points: 280
  Kwa mbali unaweza kuona ni hujuma, eti mama Ndalichako anahujumiwa! La, hapa pana kitu zaidi ya hujuma, kuna uoza. Kuna watu walibadilishwa pale baraza na tukajua kuwa hawa ndo wanafanya hujuma lakini kwa suala la hii taarifa ya matokeo nadhani mheshimiwa huyu anapaswa apate ulimi wa kusema.


  IPO SIKU BUBU WATASEMA, VIPOFU WATAONGEA NA HAKI ITAPATIKANA
   
 10. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...kama wewe ni kiongozi wa eneo fulani na unaona kuwa unahujumiwa, kuna mambo mawili unaweza kufanya. Ama una-fight within na kuwashinda wanaokuhujumu, ama unaachia ngazi kulinda heshima yako. Usipofanya either of the two, nawe utaishia kuonekana ni mmoja wapo wa UOZO uliopo ndani ya eneo hilo na utasababisha akina MyTanzania walaumiwe bure kuwa wanakutetea!! Take Action!
   
 11. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh, kaaz kweli kweli.... nami nilikuwa mmoja kati ya wale tuliokuwa tunadhani Dr Ndalichako wanafanyia fitina lakini kwa hili liliondikwa humu kwenye Nipashe la leo, duh I need a glass of water manake ni madudu matuuuupuuuuuuuu

  hivi wajemeni Tz tunapoelekea ni wapi?? kwema kweli huko?? tunafikafikaje, kwa heri au shari??

  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!!!

  Baraza la Mitihani lapeleka vyeti halisi Azania

  2008-10-29 12:29:08
  Na Joseph Mwendapole na Mashaka Mgeta


  Baada ya kusambaza vyeti feki katika shule mbalimbali nchini, Baraza la Mitihani Nchini (NECTA), limeanza kusambaza upya vyeti halisi kwenye baadhi ya shule, huku likisitisha kutoa vyeti hivyo kwa wanafunzi wanaokwenda kuvichukua.

  Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Sekondari ya Azania, Benard Ngoze, alisema.

  Baraza lilipeleka vyeti 17 kufidia vile walivyochukua ambavyo vilibainika kuwa ni vya kughushi.

  ``Walikuja juzi (Jumatatu) wakatukabidhi vyeti halisi 17 kufidia vile walivyochukua vilivyobainika kuwa ni vya kughushi,`` alisema na kuhoji itakuwaje kwa vile vya kughushi ambavyo vilishachukuliwa na wanafunzi.

  Ngoze alisema alifurahi kwa kuwa walikiri kuwa vyeti vile vya kughushi vilitoka ofisini kwao.
  Kwa mujibu wa Ngoze maofisa wa Baraza waliofika shuleni hapo walijitetea kuwa kosa lilitokea idara ya uchapaji na kwamba watashughulikiwa wote waliohusika na udanganyifu huo.
  Hata hivyo, alisema kuna vyeti vingi feki kama cha Alexander ambavyo wanafunzi walishachukua bila kujua na kuendelea navyo katika shughuli mbalimbali.

  Mwalimu Ngoze alisema wanafunzi hao wanaweza kupata matatizo makubwa kama aliyopata Alexander bila kuwa na hatia.

  ``Ni aibu kubwa sana kwa taasisi nyeti kama hii kufanya vitu vya ovyo kama hivi, sasa kama hawa wanafanya hivi tumwamini nani,`` alisema.

  Alisema uzembe wa Baraza umemsababishia Alexander usumbufu mkubwa katika maisha yake na wamemchafulia jina.

  Katika hatua nyingine yenye utata, NECTA limesitisha utoaji huduma ya vyeti (result slips) kwa wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne mwaka jana.

  Hatua hiyo imefikiwa kuanzia jana, huku NECTA ikituhumiwa kuhusika katika utaoji na usambazaji wa vyeti vya kughushi, vilivyopelekwa kwenye taasisi mbalimbali, ikiwemo Shule ya Sekondari Azania ya jijini Dar es Salaam.

  Wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari katika shule tofauti, walifika katika ofisi za NECTA jijini Dar es Salaam jana, na kukuta taarifa iliyohusu kusitishwa kwa utoaji wa vyeti hivyo vya matokeo ya mtihani.

  Uchunguzi uliofanywa na Nipashe, ulibaini kuwa idara ya utawala ya NECTA, ilitoa agizo hilo kwa kutumia kigezo cha kufanya marekebisho kwenye mfumo wa kompyuta zake.

  Waraka mmoja uliopatikana kwenye moja ya idara ya NECTA, ulisomeka: ``Kutokana na marekebisho ya mfumo wetu wa kompyuta, yanayofanyika leo na kesho, hatutakuwa na huduma za result slip na nyinginezo zinazohusiana na hizo.``

  Aidha, waraka huo uliandikwa: ``Huduma itarejeshwa tarehe 30/10/2008, tunaomba radhi kwa usumbufu, utawala.``

  Hata hivyo, hatua hiyo imelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa NECTA, wanafunzi, wazazi, walezi wa wanafunzi, waliofika katika ofisi hizo, ambao waliishia kuambiwa kuwa Baraza limesitisha utoaji wa vyeti hivyo.

  ``Hii ni ofisi ya umma, watu walitakiwa kuarifiwa mapema kwamba huduma hii inasitishwa, lakini wametoa tamko na kuliweka getini, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi,`` alisema mmoja wa watumishi ambaye hata hivyo hakutaka jina lake kutajwa gazetini.

  Nipashe ilishuhudia tamko la kusitishwa kutolewa kwa result slip hizo, likitolewa na mmoja wa walinzi katika geti kuu la kuingia ofisi za NECTA, ambaye hata hivyo jina lake halikupatikana.

  ``Huduma za utoaji result slips imesitishwa mpaka tarehe 30 mwezi wa 10,`` mlinzi huyo alisikika akiwatangazia wanafunzi na watu wengine waliofika kupata huduma hiyo.

  Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, kama kawaida yake jana hakupatikana ofisini kwake kuzungumzia suala hilo.

  Wafanyakazi waliokuwa eneo la mapokezi, waliiambia Nipashe kuwa, Dk Ndalichako yupo nje ya ofisi, na kwamba mahali alipokwenda hapakujulikana mara moja.

  ``Kuna waandishi wengi wamekuja hapa kumtafuta, lakini tumewaambia hayupo, wameondoka,`` alisema mmoja wa wafanyakazi hao ambaye pia jina lake halikupatikana.

  Wakati huohuo, habari zilizopatikana kutoka Jeshi la Magereza zimesema kuwa Alexander amerejeshwa mafunzoni katika chuo cha Magereza Kiwira mkoani Mbeya.

  Hatua ya Jeshi la Magereza kumrejesha mafunzoni inafuatia uthibitisho wa Baraza la Mitihani kwa maandishi kwa jeshi hilo kuwa Alexander hausiki na cheti cha kughushi kama ilivyokuwa imedhaniwa awali.

  Katika barua ya awali kwa Jeshi la Magereza, Baraza hilo lilisema kuwa kijana huyo ameghushi cheti na anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

  Barua hiyo ndiyo ilisababisha Jeshi hilo kumsimamisha mafunzo Alexander na kisha kumfikisha mahakamani mjini Mbeya akishtakiwa kwa kosa la kughushi.

  Katika hali ya kushangaza, Baraza hilo liliandika barua nyingine ikipingana na ile ya kwanza iliyotaka Alexander ashitakiwe kwa kosa la kughushi cheti baada mzazi wa mwanafunzi huyo kulalamika na kuwasilisha uthibitisho kwamba mwanaye alikuwa amechukua cheti hicho shule aliyosoma vikiwa vimepelekwa hapo na Baraza.

  ``Uchunguzi katika kumbukumbu za Baraza la Mitihani Tanzania umebaini kuwa Result Slip ya Alexander Gundula ni sahihi.
  Tayari tumemwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza kumjulisha kuhusu uhalali wa Result Slip hiyo ambayo pia imerudishwa kwake hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu,`` ilisema sehemu ya barua ya pili ya Baraza kwenda kwa Magereza.

  Mama wa Alexander aliliambia gazeti hili jana kuwa anatafuta mwanasheria ili aweze kulifungulia Baraza kesi kutokana na usumbufu mkubwa aliopata mtoto wake.

  Alisema baadhi ya watumishi wa Baraza walikuwa wakimkejeli na kumkashifu kila alipokwenda kufuatilia kujua ukweli kuhusu cheti cha mtoto wake.

  Alisema hatua ya mtoto wake kufikishwa mahakamani tena kimakosa imemtia doa na imemwathiri kwa kiasi kikubwa kisaikolojia.


  SOURCE: Nipashe
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  huyu dogo kapata funzo kwamba akiwa askari magereza atambue kwamba si wafungwa wote wamepata adhabu hiyo kwa kutenda kosa wengine ni kwa kubambikiziwa kama ilivyokaribia kumtokea yeye.
   
 13. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huenda hata matokeo yote ya mitihani yakawa ni feki kwa mwaka 2007.Katika wale waliosit 2007 kwa mtiahni wa form VI kuna mmoja ambaye alikuwa so intelligent hivi kwamba alipopata matokeo kuwa alipata div IV karibu afe kwa kihoro.Kwneye ule wa IV alipata div 1.Maskini alitamani kuwa gaenacologist sasa kaolewa huko Gulf na nadhani ndiyo mwisho wa ndoto yake.

  Sasa baada ya kujua kuwa kuna uozo mkubwa ndani ya Braza la Mitihani,ni wakati muafaka wa Serikali kutake action.Tunaweza kujikuta tuna vihiyo nchi nzima wanatamba na wenye nazo wakiwa kama huyo msichana niliyetoa mfano wake halisi.Tunakwenda wapi??
   
 14. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,873
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Uozo wa baraza una sura nyingi.
  1. mitihani kuvuja- hiyo wafanyakazi huuza kwa ajili ya kuganga njaa na ama kusaidia jamaa na ndugu wa karibu.
  2 sura nyengine ni short cut. vyeti feki. Hivi hutolewa kwa mtahiniwa as afa as amejisajiri kufanya mtihani wa IV au VI. then Alama zinchongwa hukohuko Div ya nguvu. Sasa katika vyeti feki Hapa ndiyo UFISADI unaingia. walio juu credit na principle za nguvu. Sasa kuona kuwa zimezidi wanaamua kubuni alama na kuwawekea watahiniwa. Hata namba hubadilishwa. Haya yote yako wazi.

  AJABU- WHY Dr Ndalichako anakimbia media? maana hapo ndipo angetumia nafasi ya kutupooza na kutupa ana strategy gani za kukomesha hali hiyo lakini Jiiii. Au ana msemaji wake? I dont think kama ana cheti feki kama baraza lake linavyotoa. Hivyo she is capable of dealing with the issue. Tatizo wamo Manyangumi!!! na mapapa!!! Yataibuka mengi. Therefore anasubiri moto upoe na afanye consultation Juu. Kama kawaida ya Watanzania UKONDOO WETU TUTASAHAU!!! waliohusika wataendelea kupeta!!! watahiniwa wataendelea kuonewa, VIHIYO WATAZIDI KUZALIWA!! TENA WENGI TU KWA MAFUNGU. UOZO. HATA WAZIRI WA ELIMU KIMYAA!!!!!!!! WHY?
   
Loading...