Kweli napendwa!

Kweli napendwa!

maharage ya ukweni

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
1,416
Reaction score
3,236
Asalaam aleykum!
Kutokana imani yangu ya kua ni muislamu ninaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja,basi siku moja baada ya kumaliza kula na mke wangu tukawa tunapiga stori mbili tatu.Baadae mke wangu akaniuliza "hivi mme wangu unapenda kuoa mke wa pili?

Mimi nikamjibu kwa maisha ya sasa yalivyo siwezi kuoa mke wa pili lakini mambo yakiwa mazuri naweza kuoa mke wa pili.Nilivyomjibu hivyo basi akaniangaliiiiiiia halafu akanitamkia maneno yafuatayo;

"kama hivyo basi bora tuishi maisha ya chini lakini niwe peke yangu"
Haya maneno nikiyakumbuka hua yaninipa faraja sana na kuamini kweli wanawake wanaopenda wanaume kwa dhati wapo.

Hii ndio sababu pekee ambayo nikitaka kuoa mke wa pili nitaweka vipengele vigumu vya kimkataba ambavyo vitamlinda mke wangu wa kwanza.Jamani kupendwa raha sana isitoshe mwanamke mwenyewe ni mzuri wa tabia,umbo na sura yaani my wife ni shombe shombe rangi rangi,nywele nywele na sauti ndio daah!Mashaalah.

NB;Inabidi kumuomba sana mungu ili kuweza kuvishinda vishawishi maana mke wako hata akiwa mzuri lazima utatamani mwingine.
 
mimi nilikuwa na mpenzi wa dini tofauti, akakataa kata kata kubadili dini kunifata ila mimi nibadili. nikakubaliana nae huku nkimwambia "huku kwenu safi si tunaoa hadi wa 4"

hii ilikuwa tiketi ya kuachana maana alinambia katika dini yao najua hilo tu na si mengine.
 
Ulimuumba mwenyewe ??
kama sio kuwa makini na ndoa yako
 
Polygamy hii, dini ina-encourgae hili suala kwa sababu za kitamaduni tu wala si kwadababu ya kiroho. Well, sasa ndugu unataka uoe mke wapili, halafu utaenda watatu, wanne... ili iweje wakati unasema bibi wako ni MZURI anakufaa kwa kila kitu? Unataka uone mwingine upate sifa na uwafurahishe wapendwa wako katika imani?

Mimi kwamtazamo wangu haya masuala kuoa wake wengi kwasababu eti dini inasema haiana mashiko yoyote spiritually. Hii mambo kazi yake nikutetea na kuimarisha MFUMO DUME.

Tuki-encourage mume kuoa zaidi ya mke mmoja si sawa tu wanawake nawao wakawa na mume zaidi ya mmoja na jamii ione sawa tu?
 
Hii polygamy wanawake huwa hawaipenda ila basi kulingana na imani fulan lkn moyoni huwa wanaikubali kwa shingo upande.

Kiukweli mm wake wawili hapana. 1 tu ananitosha hata km nikipew bure siwezi kuoa wake wawili.
 
Back
Top Bottom