kweli mume ni kichwa cha nyumba..hadi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kweli mume ni kichwa cha nyumba..hadi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Dec 11, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,547
  Likes Received: 5,756
  Trophy Points: 280
  Ashushiwa Kipigo na Mumewe Baada ya Kushinda Uchaguzi


  Tuesday, December 08, 2009 10:59 AM
  MWANAMKE Salma Musa mkazi wa Kiloleni Mkoani Tabora, amelazwa katika hospitali ya Mkoa huo baada ya kupigwa na mumewe hadi kupoteza fahamu baada ya kushinda uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa kwa tiketi ya CCM na kumshinda mumewe aliyegombea kwa tiketi ya CUF.
  Mwanamke huyo alipigwa baada ya kumpiku mumewe huyo katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini kote ambapo yeye aligombania kiti hicho kwa tiketi ya CCM na mumewe huyo kugombania kiti hicho kwa tiketi ya CUF.

  Akielezea mkasa huo kwa waandishi wa habari kwa shida, huku akiwa kitandani katika hospitali hiyo, baada ya kupata fahamu kidogo Salma alisema kuwa sababu iliyomfanya apigwe na mume wake huyo kukerwa na kitendo cha yeye kushinda uchaguzi huo kwa tiketi ya CCM.

  Alieleza kuwa mume wake huyo alikuwa akimkorofisha kwa muda mrefu na kukerwa na kitendo cha yeye kumpiku katika uchaguzi huo na kusema kuwa yeye alitoa rushwa kwa wasimamizi wa uchaguzi na maneno mengi kuashiria hakushinda kwa halali kwenye uchaguzi huo lazima atakuwa ametoa rushwa ya ngono kwa wasimamizi.

  Alisema mara kwa mara alikuwa akimpiga lakini alimsihi kuwa aachane na tabia hiyo lakini aliendela na vitendo vya kumpiga mara kwa mara na mara ya mwisho alimwamia kuwa akimpiga atakimbilia polisi kutoa taarifa.

  Alisema baada ya kumwambia hivyo ndipo alimpiga hadi kupelekea kupoteza fahamu na majirani kukimblia polisi kutoa taarifa kufuatia tukio hilo.

  Mkuuu wa Wilaya ya Tabora Mussa Chang’a amesema kuwa mume wa dada huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia ukatili huo alioufanya kwa mke wake huyo.

  Na Salma anaendelea na matibabu hospitalini.
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu mwanaume ni mjinga kuliko wanaume wote duniani!
   
 3. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kweli aisee ,siasa ni kupingana na si kupigana,yeye haoni Makamba na Warioba,wanapingana ila Hawapigani!!!na kwenye Send-off wako pamoja...sasa yeye angekubali kushindwa na warudi nyumbani ili aendelee kula matamu ya Ndoa.
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Angalia jinsi huyu baba alivyo na ufinyu wa kufikiria, haamini kama mkewe ameshinda uchaguzi. Kakosa bomu tu angelipua familia yote wafe.

  Angekuwa mkristo hapa mapenzi ni mototomoto, sherehe na nderemo mke kashinda. Lakini kwa kuwa ni haowa wenzetu,
  mmhhhh!!! Poleni sana Salma,

  Akina dada mlioko huko nawasihi tokeni, huko hakuna uhuru wa maisha ya kiumbe mwanamke!!!! Zindukaaaa mtoto wa kike nenda shule acha kufungiwa ndani, acha kujifunika minguo mweusi, angalau basi uvae nyeupe. Mbona wanaume wamejivalisha nyeupe, nyie hata jua la utosi lichome vipi ni minguo mweusii tiii.

  Salma, nakutakia upone haraka, mwache huyo baba na ondoka njoo kwa Yesu maisha ni raha na salamaaaa.
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Jamani huyo mwanaume amekosa imani kaona ufisadi mpaka uvunguni mwa kitanda chake kwa nini asifyatuke? ebu imagine una mke chama tawala kashinda uchaguzi na anafweza zaidi yako wewe! Lazma utahamaki unaibiwa penzi kha halaaaa! Wtakubebea!
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hizo ndio tabia za CUF
   
 7. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The lowest thinking I have ever seen in my life!
   
Loading...