Umesema
"1. Yanga ya Manqoba ina xG kubwa kuliko Yanga yoyote ya misimu 3 iliyopita. Maana yake tunatengeneza nafasi nyingi zaidi, goli linakuja tu." Hili nakataa
Kwa mechi za mwanzoni mwa msimu ilikuwa hivyo, Ila kadri siku zinavyoenda ndipo tunaona timu inacheza mpira wa hovyo na magoli yanakuwa ya jitihada za wachezaji ama makosa ya timu pinzani.
"2. Pressing yake ndio bora NBC. Hakuna timu inayowin mipira mingi final third kama Yanga. Hiyo ndio mpira wa Ulaya." Hili pia nakataa
Narudia tena laiti kama hatukuona mechi ya Geita, Gaborone na Simba basi tungekubali unachosema kuhusu hiyo pressing. Mechi na Simba ndio aibu tupu yaani Yanga ndio iliyokuwa inafanyiwa pressing na muda wote wanashambuliwa tu, wakipata mpira hata haichukui dakika wamepoteza.
3. Anacheza na mfumo, sio na majina. Leo Pacôme hayupo? System inabaki ile ile. Hapo ndipo unajua kocha ni bora. Hili pia sio kweli.
Kwa mtu anayeangalia mpira ni ngumu kukubaliana na haya maelezo yako, ingekuwa anacheza na mfumo basi tungekuwa tunaona kwenye sub timu inakuwa imara zaidi. Ila kila akifanya sub timu ndio inaelemewa zaidi, maanake hajui hata anachopaswa kukifanya. Tuliona kwa watangulizi wake kama Nabi, Gamondi na Miloud kuwa Yanga kipindi cha pili wanakuwa bora zaidi kwanzia kimbinu, kiufundi na kiutimamu wa mwili na hadi wapinzani walikuwa wanajua hili. Lakini chini ya kocha, Yanga kipindi cha pili ndio inakuwa hovyo zaidi na kutepeta. Ukibisha ninaweza kukupa stats za vipindi vya pili uone Yanga ya huyu Manqoba ilivyokuwa unga kipindi cha pili.
Klabu bingwa kuna timu zenye ubora na viwango kuizidi Simba, Gaborone na Geita Gold sasa kama hizo timu za kawaida zimemtoa jasho huko makundi si atapuyanga?