Kweli Magufuli aliubariki uamuzi wa Nape?

maonomakuu

JF-Expert Member
Jul 24, 2015
2,516
1,198
Nimewaza na kutafakari kwa kina kuwa Magufuli kama mwenyekiti wa baraza la mawaziri alikubali wazo la NAPE na kulibariki kuwa ni nzuri.Katibu mkuu kiongozi ambaye ni katibu wa baraza la mawaziri naye kanyoosha mkono juu akisema ndiyo mikutano ionyeshwe muhimu tu?
Bajeti ya TBC 2015/2016 ilishapitishwa na bunge leo unaambiwa gharama ni kubwa.Apana Magufuli maandamano yanaanza mapema mno kama hujaangalia kwa jicho la pili.
 
Kama mpaka jioni ya leo,Nape akiwa bado ni Waziri wa Habari,basi nitajua kwamba katika wanafiki JPM ni number moja,anachokisema sicho anachokifuata,kwa maana kwamba anakubali BUNGE kuwa kibogoyo na ndiyo sababu akatupa yule mama kilaza asiyejua hata sheria inayomfanya yeye asitakiwe kugombea nafasi za siasa
 
Nape atafukuzwa ila anafanya kazi maalum kwanza aliyopewa na Magufuli
 
Ivi kuna mtu aliamini kuna jipya chini ya huyu wanaemwita magufuli???

Sina iman nae ila alipomchagua nape kuwa waziri ndio nikapoteza imani kabisa!!!
 
Nape aliongea kama waziri wa serikali ya Magufuli, hakuongea kama mwana CCM bali waziri anayefikisha ujumbe wa maamuzi ya baraza la mawaziri.
 
hivi mnaodhani kuwa hilo jambo halina baraka za KUFULI basi poleni kwann asijitokeze kuzuia amependa sana na udicteta wake
 
Serikali ya Magufuli imeadhimia kupunguza gharama zisizo za lazima na alichokifanya Nape kina mwelekeo huo huo,so kwa mtu mwenye akili timamu tayari jibu la swali lako ameshalipata.
 
Bado naililia sana ile katiba ya wananchi,tutashuhudia madudu mengi kuanzia yale ya ukiukwaji katiba kule Zanzibar mpaka haya yanayoendelea sasa ndani ya Bunge,Uhuru wa vyombo vya habari uko wapi ?ule muswada wa kuondoa sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari sijui kama utapita chini ya huyu waziri wa sasa NAPE, nauona udikteta kwa jicho la tatu chini ya mwamvuli wa kukuza demokrasia hadaa mbele ya umma wa Watanzania ni aibu kusema tumerudi hatua kadhaa nyuma, Sanduku la Kura halipewi nafasi kufanya maamuzi ya watu hata kwa chaguzi ndogo kama za Umeya na Wenyeviti wa Halmashauri zetu,Mamlaka husika lazima zitambue Watanzania wameamka sana kuhusu haya mambo ata wakitumia Mkono wa Chuma kunyamazisha hisia mpya lakini wakumbuke hakuna dola iliyosimama milele.
 
Nape hana uwezo wa kuamua chocho,alitumwa asome kama walivyo mwandikia,msimlaumu,jilaumuni wenyewe,mliambiwa ni ile ile na mtaisoma .......
 
Serikali ya Magufuli imeadhimia kupunguza gharama zisizo za lazima na alichokifanya Nape kina mwelekeo huo huo,so kwa mtu mwenye akili timamu tayari jibu la swali lako ameshalipata.
Kama issue ni gharama then wawaachie private TV stations wafanye hiyo kazi, why monopolizing what you can't afford?
 
Mnajipa mioyo kama kawaida yenu,waziri mkuu ameshaweka msisitizo
Huwezi kuwazuia wananchi wafuatilie bunge lao mkuu,saa nne usiku ni majanga hata waulize madaktari masaa ya kulala ni mingapi,atakujibu.Ila acheni unyumbu yaani serikali ni kubwa lazima wakosea ili wakosolewa.Umri wako wote unaitetea chama hata wakijamba unavuta vumbi tu
 
Back
Top Bottom