Kweli kupata kazi ni kazi

Kweli kupata kazi ni kazi

Plot Agent

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
311
Reaction score
20
Huu ni mwaka wangu wa pili niko mtaani. Nahisi kukata tamaa na kuendelea kutafuta ajira maana nimeshatuma CV zaidi elfu 5 hadi sasa lakini nimeitwa kwenye interview mara mbili tu.

Ebu tazama inavyokatisha tamaa, kweli kupata kazi ni kazi na chezea kazi uone ilivyo kazi kupata kazi. Wana jamvi tusaidiane,mimi sichagui kazi ilimradi tu iwe halali. Pia nipo tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa muda wa miezi 6.

Napatika kupitia namba 0752953860
 
Ni vizuri ungeonyesha una elimu ya kiwango gani, ujuzi ulio nao na aina ya kazi unayotaka kufanya.
 
umeona eeeh,siyo wew tu wapo wengim zaid yako,ila usife moyo we endelea kutum ipo siku utapata,lakn kwan una ujuz wowte ule ili upate hat wazo la kuanzia make nil cv yoyte ile itakua mgum kidogo mkuu
 
usife moyo............. tafuta hata shule ujitolee. Huko utajenga kitu kinaitwa 'network, itakusaidia. Utachangamana na walimu tofauti, wengine wana miradi yao au taasisi binafsi, watakusaidia.
 
umekaa siku 760 unalalamika! hii tized bana ukijitolea jiandae kuwakaribisha wafanyakazi wapya hapo hapo ofisini kwako. fanya kazi yoyote hii mambo ya halali na sio halali utasubiri sana....jifunze kutokuogopa kwenda jela
 
Ni vizuri ungeonyesha una elimu ya kiwango gani, ujuzi ulio nao na aina ya kazi unayotaka kufanya.

Nina shahada ya IT,mkuu Mimi Niko tayari kufanya kazi yoyote ata kufundisha naweza
 
ila tunapokaa mda bila kupata ajira tunakuwa na adabu sana tena na utii hata wa kuithamini kazi ..........unaona mtu anasema niko tayari kfanya kazi yeyote ile ? vizuri sana hakuna kurembesha chapa kazi aaaaaahahahahahahahaha kazi bwana mpaka raha
 
Kupambana Mpaka zamu yetu Itafika hakuna kukata tamaa daima jaribu kupeleka cv kila kona hata ambako hawajatangaza ajira
 
Hapana. Sio kiviiile. Mbona kazi tayari unayo. Hiyo ya kitafuta kazi ni kazi tosha.
Shida ipo kwenye kupata ajira. Hapo sasa.
 
Kaka pole sana kwa sasa IT ni janga la kitaifa coz watu wengi wanapata tabu jaribu kutafuta kutafuta shule za private ukapige pindi la physics na Math shule nyingi zina upungufu wa hao waalimu bro kuna jamaa yangu alisoma computer science naye alifanya hivyo mkuu naye alisota sana ila kwa ss keshapata kitengo wizara ya ujenzi vumilia tu bro
 
kaka pole sana wala haupo peke yako me pia kama ww tu nimeamua nianzishw genge langu hapa atleast nisogeze sku hz kaz zkpatkana bas tutashukuru pia
 
duu pole mi kuna kaka nafahamiana naye yuko mbeya ana kampuni yake ngoja nijaribu kuwailiana naye kusaidiana ni bora zaidi kuliko kuwa mbinafsi
 
Hizo gharama za kazi ya kujitolea si bora uanzishe mtadi? Ama unaonaje? Kujitolea ujue hulipwi chochote
 
Back
Top Bottom