Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,112
- 24,642
Hivi karibuni EWURA walitangaza kupandisha bei ya umeme kwa 8.5% ghafla waziri akapinga kupandishwa kwa bei hizo, sasa prezdaa anamshukuru huyu waziri eti kwa kupinga kupanda kwa hizo bei!
Sasa hapa tutaona jinsi gani tunavyochezewa akili zetu na hawa watu!
Ni hivi wakati EWURA wanaanza mchakato wa kupandisha bei ya umeme huyu waziri alisema umeme hautapanda bei, lakini ukakasi unakuja hapa ni nani huyu aliyebariki ongezeko lililotangazwa na EWURA la 8.5%, je hadi hawa ewura wanatangaza je waziri hakuwa na taarifa??
Vipi naye prezdaa hakuwa na taarifa..??
Ina maana michakato ya kupandisha bei ya nishati huwa inafanyika pasipo wizara husika kushirikishwa..?
Na je hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kutundanganya eti mnashusha bei ya umeme wakati ule angali ile ilikuwa ni gia ya kuingilia huku mnakotaka nyie EWURA..?
Tamko la waziri linatia shaka weledi wake, ninaamini hili ni baada ya wananchi kupiga kelele ndipo hili tamko likatolewa!