Maulid!
Kuna ndugu yangu kweli yanayomkuta mpaka nami yananipa wasiwasi ya kuingia kwenye mahusiano.
Huyu ndugu alikuwa kwenye mahusiano ya ke na me kwa muda mrefu mpaka mungu akawasaidia kuwapatioa mtoto mzuri wa kiume.
Baada ya hapo wakakaa kama miaka zaidi ibirisi wa ufarakano ukaingia kwenye mahusiano yao na likafanikiwa.
Sasa kinachomkera huyo ndugu ni kuwa mwanamke huyo amekuwa akimsema vibaya tu mzazi mwenza kila mara yaani hakuna zuri hata moja linalosemwa juu yake na huyo mwanamke.
Sasa hii kweli ni ungwana jamani.