Kweli haya ni maajabu ya mlima kilimanjaro! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli haya ni maajabu ya mlima kilimanjaro!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by msani, Nov 3, 2011.

 1. msani

  msani JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wana jf
  kwanza poleni kwa umiza kichwa ya kila siku na nchi yetu hii ya tz.
  Tumesikia kampeni za kuupigia kura mlima kilimanjaro ili uingie kwenye maajabu saba mapya ya dunia na nimesikia tangazo kwenye redio na baadaye wakasema ili kuupigia kura tuma meseji lakni huduma hii ni kwa wateja wa 'zantel na airtel pekee' au utumie website yao ya New7Wonders of Nature

  maswali yaliyonichanganya:
  1.Idadi ya wateja wa airtel na zantel pekee na kuwabagua wateja wa vodacom na tigo
  2.kampeni kuzinduliwa juzi zikiwa zimebakia siku 10
  3.idadi ya watz wenye uwezo na matumizi ya kompyuta
  4.je tunaweza kweli kushindana na afrika kusini ambao tunashindana nao hapa afrika ukizingatia ni nchi mbili tu afrika ndo zimepata hiyo nafasi na afrika kusini walizindua kampeni zao kwa mbwembwe na matangazo mengi barabarani na redio na tz na matamasha lukuki mwezi mmoja uliopita
  halafu mi nikaona isiwe shida basi ngoja niende kwenye website,nilipofungua tu zilikuja documents kibao ambazo nahitaji ku-download kama hata haijafungua,nikajaribu documents kama 2 mwishowe nikakata tamaa kwani MB zangu zilikuwa zinaisha tu bila kujua kama nitafanikiwa kuupigia kura mlima wetu wa kilimanjaro
  au hayo ndo maajabu yenyewe,hebu jaribu muone!!!!!!!!!!!!!!

  kazi tunayo jamani
   
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Huku labda kampeni za uchaguzi ndio utaoni mauzinduzi.. Mlima huu ukifanikiwa ni mapesa na ajira mingi mingi kwa Watanzania. Lakini who cares? Wao wanatangazia bidhaa zao hata ikibidi kumuomba mkuu ashiriki kwa Tangazo lao
   
 3. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Sio kweli kwamba ni kwa wateja wa Airtel na Zantel
  Pia wale wa Tigo na Voda wanaweza kupiga kura na namba ya kupiga kura ni 15771. Ni kweli kampeni zimechelewa kuanza,na inaonekana kuna uzembe fulani. Ila hilo lisikupe tabu. Naomba uchukue hatua ukapige kura yako. Mimi nimeshapiga.
   
 4. msani

  msani JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wewe umefanya jitihada za kujua kuwa kuna vodacom na tigo wameruhusiwa kupiga kura ila mpaka sasa matangazo yanatangaza airtel na zantel tu
  hakuna anayejali kuhusu umuhimu wa huu mlima kuingia kwenye maajabu 7 mapya ya dunia na faida yake kwa watz
   
 5. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwani kuna maajabu gani pale mbona mimi siyaoni?
   
 6. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Kwani usipopigiwa kura hautakuwa mlima mrefu kupita yote africa?
  Kwani usiposhinda hao watalii hawatakuja kuupanda?

  nini faida ya moja kwa moja kwa mwananchi wa hali ya chini kama mlima huo utashinda?

  Mbona tuna madini kama tanzanite ambayo hayapatikani sehemu yoyote hapa duniani zaidi ya tanzania, lakini hatunifaiki nayo?

  Mbuga ya Serengeti ipo katika urithi wa dunia, mwananchi wakawida ananufaika na nini katika hilo?
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,084
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama ulikuwepo kwenye kichwa changu. Faida ya moja kwa moja kwa mwananchi mnyonge ni ipi? Well, walalahoi (ambao ndio wengi) tutapiga kura pengine mlima utashinda, then? Ukisikia ufisadi wa kutisha unaoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu zikiwepo mbuga na hifadhi zetu (TANAPA) na jinsi kulivyo na upendeleo wa ajabu hainiingii akilini kuthubutu kupiga kura.

  Ukisikia ufisadi wa kutisha uliofanyika pale TCRA eti wafanyakazi watatu (3) walipelekwa masomoni Ulaya kwa gharama ya T.Shs. bilioni 2.2/- huku watoto wa walalahoi wakikosa mkopo kiduchu kwa ajili ya masomo yao pale UDSM, SUA, n.k. siwezi hata kuwaza "kuupigia kura" Ml. Kilimanjaro kwa faida ya wachache! Non-sense!

  Hebu leteni hoja za kumkwamua mnyonge na haki ionekane kweli inatendeka muone mtakavyoungwa mkono na walio wengi. Vinginevyo hayo mawazo waachieni hao hao (wazungu) walioyaanzisha wahangaike nayo.
   
 8. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mimi ni mtanzania MBUMBUMBU ambaye kwaujumla sijajua maajabu ya mlima huu zaidi ya kuwa na barafu wakati wote wa kipindi cha miezi 12, kuna yeyote anajua maajabu zaidi ya mlima huu? naomba msaada tafadharli maana kila nikiulizwa na wenzangu juu ya maajabu ya mlima huu najua hilo tu. Nitashukuru kama nitapewa maajabu mengine ya mlima huu....
  Natanguliza shukurani,
   
 9. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu nimekusoma sana uko sahihi kabisa.
   
 10. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pamoja sana mkuu uko sahihi, tujiulize zile pesa BIL.2.2 kusomeshea watu 3 ndo mpango wa makusanyo ya pesa zetu? yaani kipato kipande halafu mgao uongezeke!!!
   
Loading...