Kweli hali hii inatokea kwenye biashara ya Korosho mwaka huu.....imekaaje huko bondeni...?

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
DuB7INhW0AAL89e.jpg

Nimekuwa nasikia hili mitaani hapa Dar kwenye vijiwe mbalimbali kuwa kama huna una korosha za kuuza na huna shamba basi korosho zako zinataifishwa na mamlaka iliyopewa kununua korosho huko Mtwazra na Lindi hivi kweli hali iko hivyo huko mikoa ya kusini?

Pia nasikia kuna wengine wamekuwa wanakimbia mizigo yao ya korosho kwasbabu tu hana shamba hivi kweli mambo hayo huko bondeni?

Na wengine sasa wanaona kabisa maisha yao yako hatarini kwa kufungwa kuonekana ni walanguzi wa korosho ..hasa hali halisi ikoje huko....

N aleo naona Kipanya ametoa hii katuni kuonesha kuna jambo hilo huko bondeni ni kweli hali iko hivyo

Vipi wale waliozoea kununua korosho nchi jirani na kuleta hapa kwetu kibiashara huko nyuma ilikuwa inaruhusiwa kihalali au walikuwa wanafanya isivyohalali?

Na sasa ikoje kuhusu biashara ya korosho kutoka nchi jirani je ni halali kununua na kuuza hapa nchini je kuna utaratibu upo kibiashara kufanya hivyo au korosho ya nchi jirani hapa kwetu ni marufuku kabisa kuonekana?

Kama kuna wadau wanaujua haya basi watujuze ili kuondoa maneno maneno ambayo yamekuwa yanaleta mkanganyiko huku vijiweni.
 
Sijua hiii akili ya wapi wao waliwaacha wakulima kangomba ikawaokoa nashangaaa wanakuja kudhulumu watu
 
Back
Top Bottom