Kweli chaja unaifahamu au unaitumia tu?

Kweli chaja unaifahamu au unaitumia tu?

chilali

Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
52
Reaction score
22
CHAJA hiki ni kifaa unachokitumia kujaza kifaa chako cha umeme baada ya nguvu ya betri kupungua.Vifaa vya umeme vitumiavyo chaja viko vingi vifuatavyo ni baadhi tu mfano;simu ya mkononi, tablets (kishkwambi), computer.
MAMBO YA KUZINGATIA UNUNUAPO CHAJA
Unawezashangaa hasa Kwa hawa vijana wa kishua na akajiuliza kununua tena wakati simu,tablets,camera huja na chaja zake hapana nazungumzia baada ya kupotea au kuharibika.Japo Kwa wenzangu na Mimi hatushangai simu unanua ya kitaa unapata simu baadae betri hatua ya mwisho chaja,japo manunuzi ya chaja hayawi ya haraka kivile huchukua muda tena wa kutosha tu jirani akibainika anayo aaaaha inatosha sana cha ziada hapo ni unyenyekevu tu Allah akitia wepesi ndo unaimiliki upo hapo?
a-Uwiano auliosawa kati ya betri na chaja.
hapa tunazungumzia uwiano wa kiuwezo mfano utakuta mtu anauziwa chaja ambayo inauwezo wa 3.7 wakati uwezo wa betri ni 5.7 ndugu yangu simu hiyo utaichaji mpaka uchoke kama itajaa muda utaotumika zaidi ya masaa 10 kweli utaliwahi Bus la asubuhi pale Mbezi Kwa Magu?
b-Idadi ya miguu
vichwa vya chaja/plug vimepewa majina mengi sana na wagunduzi mbali mbali wa vifaaa vyaumeme kwa kuzingatia mambo mbalimbali kama vile umbo,idadi ya miguu.Acha tujikite hapa hapa kwenye miguu kuokoa muda. Hizi zipo za miguu miwili bapa na duara miguu miwili bapa matumizi yake yako chini mno ukilinganisha na miguu miwili duara rafiki ukiuziwa ya miguu miwili bapa utahahaa kupata kebo au soketi itakayofiti kwakuwa maranyingi chaja hizi miguu yake hukaribiana sana inakuwa ni kazi tena kubwa kupata soketi au kebo ni seme tu sio nzuri.Pia Kuna hizi za miguu mitatu ambapo zinafaa Kwa soketi zote na tronic cables niseme tu ziko vizuri hizi chaja.
C-Malighafi iliyotumika kutengeneza
Hapa siwezi ongea chochote Kwakuwa wewe ndo mwamuzi unapokuwa dukani au na machinga kitaa utaangalia mvuto wa chaja rangi utasikia Mimi wa jangwani sio Simba sitaki nyekundu lakini pia umbile la chaja.
Baada ya kununua chaja yako zingatia yafuatayo Kwa lengo la kurefusha uhai wa chaja Yako.

*Epuka kukunja waya wa chaja yako,hii itapelekea kupata usumbufu wakati wa kuchaji kifaa chako utakuta sometimes Charger connected na muda huo huo charger removed kiashiria kwamba chaja haikosawa nyaya zimepata shida baada ya kukunjwa mara Kwa mara.

*Chaja ikae kwenye umeme pale tu itakapokuwa inatumika kinyume na hapo ni tatizo inaweza isidumu na ukalazimika kununua nyingine mwisho wa siku simu moja chaja 6 ndani ya mwaka mmoja ni hasara hii.

*Epuka kulamba chaja
Kuna baadhi ya watu hupima uwepo wa umeme,uzima wa chaja Kwa kulamba sio sahihi kabisa mate hupigisha shoti lakini pia mate huacha unyevu baadae asidi na kuua kabisa chaja.
Mwisho niwatakieni siku njema,Asante.
 
Duh,charger yangu ya s20 + niliikubali mno .imekufa baada ya kuitumia kuchaji powerbank
 
Back
Top Bottom