Kwaya ya CCM yahamia CHADEMA

Kwaya ya CCM yahamia CHADEMA

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Kwaya ijulikanayo kama Kwaya ya Ng'ombe ya Magu Mjini Mkoani Mwanza yenye watu 45 imejiengua CCM na kuhamia CHADEMA. Wanakwaya hao wamepokelewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu ndugu Katinde aliyeongozana na Katibu wa CHADEMA Jimbo la Magu mjini Bahati Simon.

Hii ilikuwa ni Kwaya ya waliyoitumia sana kwenye kampeni na kwenye kila matukio yao na vifaa vyao vyote vya muziki vilitunzwa kwenye ofisi za CCM wilaya ya Magu. Siku mbili kabla ya kuhamia CHADEMA walitafuta kambi ya muda na wakatunga nyimbo za kumsifia Dr. Slaa ambaye atafanya ziara hivi karibuni wilayani Magu.

 
Duuuh,mda wote nilikuwa sitaki ku-log in, ila hii imenileta mpaka ndani, ni kali na haijawahi kutokea. Mfungo wa Lema sio wa kawaida, Chuma Ulete ya CHADEMA ni international
 
Naona hawajajua effect ya huu mwendo wa sasa wa kisiasa mpaka baadae 2016.
 
Kesho utasikia na kuona bendi ya ccm ile ya Komba yahamia chadema, mara filikunjombe na mwisho lowasa na jk wahamia chadema! Pipoooooooooooooooz!...
 
mpaka sasa tutegemee kuskia makubwa zaidi ya haya
 
mmh,kwaya tena?
Si ndo yale yale ya kuanza kuchezewa ngoma kabla ya hotuba
au kukagua maendeleo?

Waingie kama wana chama tu,kucheza ngoma na kuimba imba
kwaya za ajabu hakuna mda sasa,time is money.
 
hahahahahahahahahah.......

Nachelea kusema bunge likiahirishwa wabunge wa magamba hawaendi Dar, watatoka nduki sana hapo Dodoma!!
 
Safi sana na Tunasubiria kusikia Dkt Limbu akiachia ubunge maana miaka 10 hakuna alichofanya cha maana jimboni kwake
 
Aiseeee, it is so amazing kwa kweli... NAPE why haya yanatokea, wewe si unapokea mshahara wa kutosha kwaajili ya kuhakikisha chama kinajozolea wafuasi na wakereketwa wa kutosha? Hii tafsiri yake ni kwamba kazi imekushinda hivyo unapokea mshahara-pesa usizozitolea jasho(UFISADI), Ikiwa ndivyo basi na wewe ni unatakiwa ujivue gamba!!
 
Back
Top Bottom