Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 15,930
- 27,184
Poa poa Amna noma mzeeHamna kitu pale .
Mabondia tunaowaangalia kwa makini kwa sasa ni Dmitry Bivol,Usyk , Crawford nk
Bhebhe mwizukulu jilalaNilizaliwa na kulelewa katika Ukatoliki. Ujana nikaupitishia katika Usabato. Utu uzima niliokoka na kuwa mlokole pyua. Na sasa uzeeni (78) nimerudi tena kuumalizia mwendo katika Usabato.
Yote kwa yote Mungu ni yule yule ati!
Kwaresma njema! 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Hayaga nyanda.Bhebhe mwizukulu jilala
Mwezio kamfunga wewe unazumzia chaiushakunywa chai au bado?
Huyu anataka atuweke kwenye mashindano ya kufuturuHongera sana chief,pepo unayo mkononi kwa kujua kwako kufunga kwa imani yako but kama unadhani Mungu anapima kwa mzani mdogo kama huu wewe ndiye unayeshinda njaa.
Tunaomba mafundisho zaidView attachment 3259835
IFANYE KWARESMA 2025 KUWA YA TOFAUTI KIROHO
🟪🟪 Kwaresma ni kipindi maalum sana kiroho, ni safari ya kwenda nyikani na Bwana Yesu kwa muda siku 40.
🟪🟪 Kipokee kipindi hiki kama fursa ya Kiroho kwani ni kipindi cha kufunga, Kusali, Kutubu, na Kufanya matendo ya Huruma kwa wahitaji.
🟪🟪 Jiandae kiroho kwa kufanya toba halisi.
🟪🟪 Usiingie kwenye mfungo huu maalum ukiwa moyo wako una makwazo ama manung'uniko yeyote achilia kila jambo lililo gumu na ubaki huru.
🟪🟪 Weka nia maalum ya mfungo kwa kutenga na kumwambia Mungu akupe msaada hasa changamoto nzito na ngumu ambazo kwa upande wako unaziona huziwezi.
🟪🟪 Kama huna changamoto yeyote ya kiafya mfano kama si mjamzito ama husumbuliwi na ugonjwa wowote tafadhari jinyime kwa kutokula chakula.
🟪🟪 Usifunge kwa kujionyesha kwa watu kwamba na wewe umefunga, funga kwa kusudi ama nia uliyoikusudia ili Mungu akupe msaada wake.
🟪🟪 Kumbuka kipindi hiki hutokea mara moja tuu kwa mwaka hivyo ifanye kama fursa ya kiroho ambayo mara tuu baada ya kumaliza mfungo utavuna na kujiwekea akiba kubwa ya kiroho.
🟪🟪 Uwapo kwenye mfungo waombee na watu wengine kwani ukifanya hivyo Mungu atapokea maombi yako haraka na kwa urahisi.
🟪🟪 Saidia wahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha Kwaresma, watu wote Mungu amewaumba kwa mfano wake hivyo unavyowasaidia tambua kwamba unagusa mboni yake.
🟪🟪 Omba kwa imani na Mungu ataisikia sauti yako
🟪🟪 Omba kwa kumaanisha na Mungu ataenda kukutendea sawa sawa na mapenzi yake
🟪🟪 Safari hii ya siku 40 itakuwa ni historia kwenye maisha yako kwani ukifunga na kuomba kwa imani Mungu ataenda kuruhusu mambo makuu mnoo yatendeke maishani mwako.
🟪🟪 Nakutakia Mfungo mwema wa Kwaresma na Mungu akubariki sana 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Tubun na kuiamin injiliKesho mapema ibada ya majivu.
Tuombeane kwa Mungu azipokee toba zetu madhaifu na tabia mbovu tulizozoea kuziishi huko nyuma Kwaresma hii ikaziondoshe kwetu tubaki wasafi hata milele.
Kabisa mimi mwenyewe nataka nikaze kabisaMungu anipe rehema kwaresma hii nifunge niache vitu vya anasa.
Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU katika kristo YESU
Tumsifu YESU KRISTO. AMINA
Tumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo hasa kwa kumtuma mwanae aje atukomboe . AMINA
PASAKA ni nini pasaka ni kuteseka/mateso/ kifo/kufa/na kufufuka kwa YESU KRISTO
PASAKA ilianzia misiri lakini badae wana wa Israel MWENYEZI MUNGU aliwaagiza waadhimishe pasaka kama kumbukumbu la kwamba wao walikuwa watumwa wa mateso huko misiri
Hivyo wakristo kwa sasa huadhimisha pasaka kama kumbukumbu la kwamba TULIKUWA WATUMWA/ WAFUNGWA WA MINYORORO YA SHETANI mpaka pale BWANA wetu YESU KRISTO alipokuja kutukomboa kwa mateso yake makali pale msalani
Je kwaresma ni nini, kwaresma ni ibada ni ibada ambayo husindikizwa na mfungo wa siku 46 kutoa Dominika 6 hivyo siku hubaki 40
Kufunga kwaresma ni kufanya nini, kufunga ni kuyakalibisha mateso ya YESU KRISTO ambaye ni mfufua wa ulimwengu wote
Hivyo wewe uliyefunga unapaswa kuwapikia wengine ambao hawajafunga na kutoa pesa yako iliyopaswa kula ili uwalishe ndugu na watu Baki
Lakin ndugu zangu kufunga bila sala huko ni kushinda NJAA kabisa
Kufunga bila kunuia jambo flani huko nako ni kushinda NJAA kabisa
Lakin pia kwaresma huanza na jumatano ya MAJIVU
MAJIVU ni nini, MAJIVU hutukumbusha kwamba sisi wanadamu ni mavumbi na mavumbini hakika tutarudi
Masomo husika yoel 2:12-18
Injili husika mathayo 6:1-6,16-18
Moderate tafdhari nawaomba uzi huu msiuunganishe maana uzi utakuwa wa milele kwa update za kila siku juu ya neno la MUNGU la kipindi cha kwaresma
Basi nawakaribisha tufunge na tumuombe MUNGU wetu aliye mwema sana
SAYUNI BOY
Mambo ya Dunia ni mambo gani?!INaachana na mambo ya dunia namrudia Mungu wangu
Ndiyo zao hao jamaa.Huyu anataka atuweke kwenye mashindano ya kufuturu
Asante sana kwa swali zuriNaomba kuuliza kama ifuatavyo!:!.
1️⃣ Je kwaresma ipo kwa madhehebu yote ya kikristo / kikristu au ni special kwa wakatoliki peke yao?
2️⃣ Je makanisa au madhehebu yote yanayoadhimisha kwaresma ni lazima kujichora misalaba myeusi kwenye mapaji ya uso au hili ni kwa wakatoliki peke yao?
Nauliza hivi kwa sababu siku moja nilikuwa naongea na dada mmoja msabato akasema kwenye usabato hawana sikukuu ya krismas wala pasaka ila sikukumbuka kumuuliza kuhusu kwaresma kama kwenye usababato ipo au haipo?!
Mh! aisee!Asante sana kwa swali zuri
Kwaresma ipo kwa ajili ya watu wote lakini si kwa kila mtu
Baadhi ya madhehebu huamisha kwaresma kwa ukubwa kama Lutheran, Anglican, catholic, Moravian na mengine mengi lakini siyo yote, madhehebu mengine hupinga kwaresma kwa sababu ambazo wanazijua wao
Kupaka MAJIVU usoni ni thehebu ya Catholic pekee ndo hupaka MAJIVU uson, Sina uhakika kama na Lutheran nao hupaka majivu
Hao watu wanaoitwa wasabato achana nao wao ni wapinga KRISTO na wako wazi wala hawajifichi