Kwanzajamii limeingia kaburini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanzajamii limeingia kaburini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumaku, Dec 22, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jarida la Kwanzajamii halikuonekana mitaani leo. Kwenye mtandao wa kwanzajamii.com nimeunasa mjadala wa wadau wenye kulaumu uongozi wa gazeti hilo kushindwa kulitoa mara moja kwa wiki na kulifanya kuwa la mara moja kwa mwezi. Je, kwanzajamii ndio linaingia kaburini?


  • Mara moja kwa mwezi ni kuliua hili gazeti kabisa, hasa hasa ukizingatia kuwa gazeti la Kwanzajamii linashindana na utitiri wa magazeti mengine madogo.
   Nafikiri uamuzi wa bodi umeigia ktk mtego wa ‘group-thinking’, hivyo mimi kama ‘mjumbe wa kudumu wa wasomaji’ ktk bodi yenu, nawatahadharisha hiyo ‘kurudisha majeshi nyuma’ ni kosa kubwa kabisa.
   ‘Majeshi yasirudi nyuma bali yashikilie eneo (Market-share) yaendelea mbele kwa ‘formation’ mpya, maana ukiachia hiyo ‘market share’ basi eneo litachukuliwa na majeshi ya upinzani.
   Lets think outside the box, brand/product ya jamiikwanza itapotea kabisa kwa kurudisha majeshi nyuma. Kwanzajamii ishikilie kuendelea kutoka mara nne kwa mwezi kama kawaida.

   # 15 December 2009 at 1:16 pm
  • Joseph Mbele said: Mimi pia siafiki wazo la kulichapisha gazeti hili mara moja kwa mwezi. Bora liendelee kupambana na hali na kutoka kila wiki. Juhudi zifanywe za kuwatafuta wachangiaji wengi wa makala, wenye moyo wa kuchangia elimu na ujuzi wao kwa jamii.
   Tuna walimu katika shule zilizozagaa nchi nzima, na wanafunzi wa vyuo vikuu, na watafiti, na kadhalika. Hata wanasiasa wameshajitokeza na kujieleza katika KWANZA JAMII. Mkondo huu ungeendelea, ili mradi gazeti liendelee kuwa chombo cha kuelimishana. Watafutwe maofisa kilimo, madaktari, na kadhalika, wachangie uzoefu na mawaidha yao.
   Kama ni soko, gazeti lisambazwe pia Kenya, Uganda, Burundi, na Rwanda.
   Pamoja na kuwa tunayo magazeti yenye kuelimisha nchini Tanzania, lakini tunayo pia magazeti mengi ya udaku. Ingekuwa KWANZA JAMII ni gazeti la udaku, nisingejali iwapo linaamua kutoka mara moja kwa mwezi. Ni muhimu KWANZA JAMII lichapishwe kila wiki, ili angalau lichangie mapambano dhidi ya udaku.


   # 16 December 2009 at 9:13 am
  • Mgayamlongo said: Ni habari yenye huzuni,kwani sio wengi wanaweza kupata mtandao wa internet.
   Nimekuwa nikiangalia matangazo katika gazeti la KWANZA JAMII,kwani vyombo vya habari vingi hupata nafuu ya gharama za uendeshaji kwa njia ya matangazo.
   Mwenyekiti awe muwazi,kama ni mtaji,auze hisa.Kulipoteza kwa kipindi gazeti kisha kulirejesha ni kuwakimbiza wateja/wasomaji.
   Kimtazamo habari nyingi zitapita bila kutolewa maoni katika kipindi husika. WADAU MKO TAYARI KUNUNUA HISA ILI GAZETI LITOKE KILA WIKI?

   # 16 December 2009 at 11:41 pm
  • Evarist Chahali said: Wataalam na wachambuzi wapo lakini si wote watakaojitokeza kuandika makala aidha kutokana na kutingwa na majukumu au hawajashawishika kufanya hivyo. Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuanzisha kampeni ya kupata waandishi/wachambuzi wa kujitolea. Ni njia ya aina hiyo inayoziwezesha taasisi kubwa zinazotegemea volunteers kujimudu. Hakuna ubaya kumwomba flani atoe mchango wake. Ila wazo la toleo moja kwa mwezi ni sawa na kulichimbia kaburi jarida hili.
   
Loading...