popo1986
JF-Expert Member
- Jul 30, 2014
- 1,120
- 371
Leo majira ya saa kumi jioni maeneo ya ubungo katika ukumbi wa Blue Pearl..askofu Josephat Gwajima wa kanisa la ufufuo na uzima, ametunukiwa nishani ya "Doctor of philosopy in Theology...PhD", ambayo amekuwa akiisomea kupitia chuo cha Omega Global University chenye makao makuu yake South Africa...
Nnilishuhudia leo umati wa wakazi wa DSM wakielekea na kutoka pale blue pearl Hotel ubungo plaza..
shikamoo.. Bishop,Dr. J.Gwajima.:smile-big:
Nnilishuhudia leo umati wa wakazi wa DSM wakielekea na kutoka pale blue pearl Hotel ubungo plaza..
shikamoo.. Bishop,Dr. J.Gwajima.:smile-big:
Leo Jumamosi hii ya Tarehe 7-03-2015, Mchungaji Kiongozi na mwanzilisha wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Duniani, Askofu Dr. Josephat Gwajima anatunukiwa Shahada ya Falsafa (Doctor of Philosoph) PHD na Chuo Kikuu Cha Wamarekani OMEGA ambacho makao yake makuu kwa Africa yako Afrika Kusini. Mahafali hayo ambayo yamefanyika katika Ukumbi mkubwa wa Plue Pearl (Ubungo Plaza), yalihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, Viongozi wa Dini na Maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha OMEGA.
Shahada hii pia inajumuisha kazi na mchango wake kwa jamii ya Tanzania, Africa na Duniani kwa Ujumla. Machache kati ya kazi Zake
A) Askofu Dr. Josephat Gwajima, katika uchunguzi wake amegundua Injili iliyoletwa na wakoloni iliyopelekea kujengwa kwa makanisa na madhehebu mbalimbali ilikuwa na lengo la kiutawala. haikulenga hasa kujenga msingi wa Neno la Kweli lakini ililenga kuwafanya waafrika watawalike. misingi hii ambayo bado tunaitumia mpaka leo si uhalisi wa Biblia. Askofu Dr. Josephat Gwajima, amekuja na uchunguzi wake uliopelekea kuandikwa kwa kitabu "THE AFRICAN CHURCH IN AN AFRICAN PERSPECTIVE" ambacho kimetafsiriwa kwa kishwahili kama 'Kanisa la Afrika Katika Mtazamo wa Kiafrika' . Katika Kitabu hiki anaelezea misingi ya kweli ya Kibiblia katika kuanzisha na kuendeleza makanisa yetu Afrika.
B). Askofu Dr. Josephat Gwajima, ametunga kitabu maarufu 'Maombi ya Kushindana" ambacho kimetafsiriwa kwa lugha 16, nakala ya kitabu hicho ni moja kati ya nakala zinazoongoza kwa usambazaji hapa Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na nchi nyingine.
C).Askofu Dr. Josephat Gwajima, ametunga kitabu "Ressuraction and Life' ambacho kimetafsiriwa kwa lugha ya Kijapan, kiingereza na kikorea. kitabu hiki ni maarufu sana Nchini Japan na kinashika nafasi za juu katika usambazaji wake nchini humo.
D). Mbali na Nakala hizo lakini pia Askofu Dr. Josephat Gwajima, Ametunga Vitabu ambavyo ni maarufu hapa Tanzania na Duniani kama vifuatavyo.
MSINGI WA KIROHO
KANUNI YA KUJENGA KANISA LA MAELFU (MEGA CHURCH)
GHARAMA YA KUJENGA KANISA LA MAELFU
NENO NI MUNGU NA MUNGU NI NENO
USHINDI KWA DAMU YA YESU
SILAHA ZA VITA VYETU
VIFUNGO VYA ROHONI, MWILINI NA NAFSINI.
HATARI YA NDOTO
MAOMBI YA KUBOMOA MADHABAHU
SHERIA MBILI ZA ROHONI
JINSI YA KUTUNZA MUUJIZA WAKO
MASHETANI KATIKATI YA UZAO WA WANAADAMU
KIBALI KILICHO IBIWA
FUMBO LA MAUTI
KULOGA KWA KUPIGA MAFUNDO
MICHORO YA GIZA
MIMI SI KAMA WALE
USINGIZI WA KICHAWI
DAMU INENAYO MEMA
VIKAO VYA UHARIBIFU
BARAKA KATIKA MAPAMBANO
NGUVU YA MSALABA
UBATIZO WA KIBIBLIA
MKATE WA KILA SIKU
SERIKALI YA MASHETANI
MAOMBI YA KUGHAIRISHA MABAYA YALIYOPANGWA YAMPATE MTU
MAJESHI YA WAFU
SHERIA ISHIRINI ZA UONGOZI
E). Askofu Dr. Josephat Gwajima, amekuwa mstari wa mbele kukemea kwa uwazi propaganda za Udini zinazojipenyeza kwenye misingi ya Dola hili la Kidemokrasia.
F). Askofu Dr. Josephat Gwajima, Pia Amekemea kwa Uwazi serikali ya nchi hii pale ilipokwenda kinyume na maadili ya uongozi bora na misingi ya haki kama vuguvugu la Ugonjwa wa Dengu, Mauaji ya Albino na kuwakemea watawala wanaokwenda kinyume na maadili ya utumishi wao. pia amekuwa mstari wa mbele kuipongeza serikali kwenye hatua zake za kuwaletea maendeleo wananchi wake.
G).Askofu Dr. Josephat Gwajima, ametembelea na kufanya mikutano zaidi ya nchi 38 za Afrika, Marekani, Canada, nchi zote za Ulaya zinazounda shirikisho la Umoja wa Ulaya, Uingereza, japan, Korea, China, na katika mikutano yake yote hiyo imekuwa ikihudhuriwa na maelfu ya watu ambayo inapatikana Youtube.
Kila la Heri Askofu Dr. Josephat Gwajima.