Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

tumuamin zitto au padre mzinifu.

Na nyie ndiyo type ya watu anaohitaji Zitto kwenye ACT. Watu wasiokuwa na uwezo wa kuhoji na kujua ukweli. Endelea kuwa gizani. Hapa hoja ni nini? je umesoma kilichoandikwa au unavamia tu bila kujali contents? Pole sana.
 

[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Utabiri kinzani na mchanganyiko:

NAVAA VIATU VYA "SHEIKH YAHYA" KWA MUDA.!

Apumzike kwa amani huko alipo mnajimu mkuu, ustaadh, mtaalamu wa nyota na anga za mbali, bingwa wa kusoma alama za nyakati, mtaalamu wa kuita na kufukuza majini marehemu Sheikh Yahya Hussein. Miaka kadhaa baada ya kifo chake leo naomba kurithi kazi yake japo kwa dadika chache.

Nimesoma interview ya leo ya ZZK na gazeti la JamboLeo ameeleza juu ya umakini wa usalama wa taifa. Amesema wanaopuuza usalama wa taifa ni watu ambao hawafikiri vizuri.

Kauli hii ya ZZK imenifanya nijaribu kuunganisha dots na hivyo kuweza kufanya utabiri wangu vzr.

Dot ya kwanza. Siku chache zilizopita maafisa wa juu wa Usalama wa taifa waliripotiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Ndg.Edward Lowassa na kuwa wanamuunga mkono kwny mbio zake za Urais. Usalama wanaodaiwa kumuunga mkono Lowassa ndio haohao ZZK anawasifia leo kuwa wako makini.

Dot ya pili. ZZK wakati anafukuzwa CHADEMA alisema ipo siku atakuwa kiongozi mkubwa nchini na eti chadema watamheshimu kwa hilo.

Dot ya tatu. Fedha nyingi na nguvu kubwa inayotumika kukitangaza chama cha ACT inatoka wapi?

UTABIRI.!

Mpango wa ZZK kuanzisha chama cha ACT wakati akiwa bado mwanachama wa CHADEMA ni mpango ulioratibiwa vizuri na usalama wa taifa wanaomuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa.

Lowassa is very strategic person. Anajua kuwa hawezi kupitishwa na CCM kugombea Urais. So ametafuta chama mbadala. Chama ambacho kitamfanya ashinde kirahisi.

Lowassa anajua kuwa akijiunga CHADEMA hatapokelewa na hata akipokelewa hawezi kupewa nafasi ya kugombea Urais. So ndoto yake itakuwa imekufa. Sasa afanyeje ili agombee nje ya CCM na kushinda?

Mbinu aliyotumia ni kuanzisha chama ambacho kitapata support CCM na upinzani. Na chama hicho ni ACT.

Alichofanya Lowassa ni kutafuta mtu mwenye ushawishi ndani ya CHADEMA ambaye akiondoka anaweza kuhama na wafuasi wengi. Na mtu huyo ni ZZK.

So ZZK kazi yake kubwa ni kuibomoa CHADEMA. Aondoke na wafuasi wengi wa CHADEMA kwa kadri iwezekanavyo. Ndio maana hadi sasa hatujasikia mtu kutoka TLP, UDP au PPT Maendeleo, kajiunga na ACT. Wengi tunaowasikia wametoka CHADEMA. Hiyo ndiyo kazi aliyopewa ZZK. Kuibomoa CHADEMA.!

Na wapo wabunge kadhaa wa CHADEMA watakaojiunga na ACT baada ya bunge kuvunjwa (baadhi majina tunayo). Wamehofia kujiunga sasa hivi kwa sababu watapoteza "kiinua mgongo" chao kama ilivyokua kwa Fredy Mpendazoe mwaka 2010. So baada ya bunge kuvunjwa mwezi July kuna utitiri wa wabunge wa CHADEMA watajiunga ACT.

Baada ya hapo Lowassa mwenyewe atajiunga ACT akifuatwa na mamia ya wabunge wa CCM na mawaziri lukuki. Wapo wafuasi na viongozi wa vyama vingine vya upinzani ambao nao watajuinga ACT. Kufikia hapo ACT kitakuwa chama tishio kwa CCM na upinzani maana kina wafuasi kutoka chama tawala na upinzani.

Wakati CCM na CHADEMA wakiwa kwenye taharuki ya mpasuko kwenye vyama vyao, ACT watatumia fursa hiyo kujinasibu na kujitafutia uhalali kwa wananchi. Ushawishi wa Lowassa na ZZK utawafanya watu wengi wajiunge na ACT kutokea CCM na Upinzani hasa CHADEMA.

Wakati wa uchaguzi ACT itapata kura nyingi kutoka kwa waliokua supporters wa CHADEMA na waliokua supporters wa CCM na vyama vingine vya upinzani. So ACT itapunguza kura za CCM na za CHADEMA kisha watachanganya pamoja na kudeclare ushindi.

Baada ya hapo Edward Lowassa atatangazwa Rais kupitia ACT na ndipo atamteua ZZK kuwa Waziri mkuu. Na hapo ndipo litakapotimia lile neno la ZZK kuwa "ipo siku nitakuwa kiongozi mkubwa nchini na CHADEMA wataniheshimu"

Mkakati huu unadaiwa kupangwa kwa ustadi mkubwa na Usalama wa taifa ndio maana ZZK amediriki kusema "wanaobeza usalama wa taifa hawajui kazi yake".

‪#‎MWISHO WA UTABIRI‬.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Copy and paste...👆👆
 
Kwa lugha nyepesi ni kuwa Zitto ni msaliti wa wananchi...
 
Wewe usipopigwa ban kwa siasa chafu basi thread hii itafugwa....
 
Jasiri haachi asili.. ZZK hakuanza hizo tabia Leo, tangy UDSM mwendo ni huo huo... Tunaomjua wala hatushangai
 
Mh!kazi kweli kweli,akika aliye msafi,Mungu atupe macho yakuona watanzania tumchague raisi na wabunge aliowakusudia yeye
 
Hakuna Cha Chadema Wala Ccm Hivi Nivyama Tu,mabadiliko Yanaletwa Na Mtu Yeyote Mwenye Uzalendo Wakweli, asiembinafsi,mwenye Uchungu, huruma Na Ari Ya Kuthamini Wengine Thats Why Hata Madictator Wengi Wamefanikiwa Kuleta Mabadiliko'hayo Mengine Propaganda Za Vijiweni Tu!
 
Jaribu kuwa mstarabu huyo anayemsema ni mzinifu kamzini mama yako.changia hoja sio matusi

namsaidia mkuu, kamzini Rose Kamili na ndiyo kisa cha kufukuzwa upadre na kwa sasa anazini na Josephine. Hiyo ni kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno uzinifu
 
namsaidia mkuu, kamzini Rose Kamili na ndiyo kisa cha kufukuzwa upadre na kwa sasa anazini na Josephine. Hiyo ni kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno uzinifu
Zito ni msaliti coz ametengeneza chama ndani ya chama pinzani wakati ni mpinzani. Alafu alitaka uongoz alipokosa akaona akaanze chama chake na aje kuwa kiongoz mkuu na hivyo ndivyo imedhihirika. Angalaia hata mikutano yake yani yeye ni kiongoz mkuu kama alivyo mbowe. Na hiyo ndo nafasi alikuwa anaitamani. Mroho kabisa. Huyo mwenyekeiti aliopo hapo ni geresha tu na ndo mana wamemuweka mwanamke ili asikinzane na kiongozi mkuu. Hahahahaa
 


Zito ni msaliti coz ametengeneza chama ndani ya chama pinzani wakati ni mpinzani. Alafu alitaka uongoz alipokosa akaona akaanze chama chake na aje kuwa kiongoz mkuu na hivyo ndivyo imedhihirika. Angalaia hata mikutano yake yani yeye ni kiongoz mkuu kama alivyo mbowe. Na hiyo ndo nafasi alikuwa anaitamani. Mroho kabisa. Huyo mwenyekeiti aliopo hapo ni geresha tu na ndo mana wamemuweka mwanamke ili asikinzane na kiongozi mkuu. Hahahahaa
 
Padri slaa ni mzinifu, amezaa na Josephine je alimuoa? Sasa mnaambiwa mzinifu mnatoa mipovu kwa Padri kaoa?
 

Nimekapenda sana hako ka utabiri kako mkuu japo siwezi kukachangia maana naogopa kutukanwa na mi nkajibu mwisho nikalambwa ban
 
ndomana wanasiasa huwa nawatazama kwa jicho la pili. Hapo zamani za kale kulikuwepo na mtu, mtu huyo hata zamani hizi yungali hai. Mtu huyo aliitwa CCM B. Loooo! cjui nani alimtajia jina hilo, ila CHADEMA wanajua. Lakini haaaa, leo CHADEMA WAPO NAYE CHUMBA KIMOJA. Umhhh, nisije sutwa bureeeee, huenda mtu huyo siku hizi ametorokea CDM B badala ya CCM B. Siasa bwana haaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…