Kwanini zamani ilikuwa ikitokea mkala kitoweo cha Kuku basi paja anapewa baba?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Miaka hiyo kabla ya ujio wa hawa uzao wa ma-.com. ilikuwa ikitokea siku kuku akachinjwa baba anapewa nyama za paja(ni lazima), filigisi,na sehemu nyingine muhimu. Huku watoto tuliambulia utumbo, mwisho wa bawa la kuku, na makanyagio bila kujali tulijitoa namna gani kufanya riadha na huyo kuku.

Kwani paja lilikuwa na kitu gani special kipindi hicho?
 
1. Heshima
2. Hadhi
3. Minofu mingi (japo wataalam na wazoefu wanasema kidari ndo kina nyama nyingi)
4. Shape yake inatia hamasa kuila si sawa na kula shingo ya kuku au mbavu hata mabawa (japo mbele chicken wings zinauzwa aghali sana).
5. Woga tuu... na ubabe...
6. Linaongeza nguvu za kiume.
 
Miaka hiyo kabla ya ujio wa hawa uzao wa ma-.com. ilikuwa ikitokea siku kuku akachinjwa baba anapewa nyama za paja(ni lazima), filigisi,na sehemu nyingine muhimu. Huku watoto tuliambulia utumbo, mwisho wa bawa la kuku, na makanyagio bila kujali tulijitoa namna gani kufanya riadha na huyo kuku.

Kwani paja lilikuwa na kitu gani special kipindi hicho?
Paja sidhani ila Firigisi ilikuwa ni lazima apewe mkubwa kiumri hasa baba au kama mmeoa sehemu moja na mkaalikwa ukweni ni lazima Firigisi apewe Mume mkubwa vinginevyo ataona kadhalilishwa na ngumi zinaweza zikafumuka ukweni.
Ni mambo ya kimila tu hasa kwa watu wa pwani na maeneo mengineyo.
 
1. Heshima
2. Hadhi
3. Minofu mingi (japo wataalam na wazoefu wanasema kidari ndo kina nyama nyingi)
4. Shape yake inatia hamasa kulia Juana si sawa na kula shingo ya kuku au mbavu hata mabawa (japo mbele chicken wings zinauzwa aghali sana).
5. Woga tuu... na ubabe...
Hapo naona namba 5 tu inabeba vyote. Uoga ulizidi.
 
Paja sidhani ila Firigisi ilikuwa ni lazima apewe mkubwa kiumri hasa baba au kama mmeoa sehemu moja na mkaalikwa ukweni ni lazima Firigisi apewe Mume mkubwa vinginevyo ataona kadhalilishwa na ngumi zinaweza zikafumuka ukweni.
Ni mambo ya kimila tu hasa kwa watu wa pwani na maeneo mengineyo.
Muda mwingine firigisi zilikuwa anapewa mgeni kama si baba.

Kuhusu mama sijui alikuwa anaambulia nini maskini.
 
Baba wa familia anafanya kazi kubwa ya kuhangaika na kutumia nguvu kutafuta pesa kwa ajili ya familia.. hivyo kwa sababu za kiafya anahitaji protein kwa wingi.

Protein kwa wingi inapatikana kwa kula minofu ya nyama ambayo hupatikana kwa wingi maeneo ya mapaja.

Firigisi pia ina protein kwa wingi.
 
Aisee....
 
sisi nyumbani haikuwa tatizo sana maana kimsingi kuku ana sehemu 6 zenye minofu,mapaja,mabaja ya ndani,na kifuani kuna minofu mikubwa sana ukigawa mara2.wakati familia yetu tulikuwa 5.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom