Kwanini Websites za Serikali ni Mbovu na Hazina Tija kwetu?

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
628
Haya malalamika ya websites za serikalini naona sasa yamezidi, kwenye Idara, Taasisi, Shirika, Bunge na Wizara malalamiko ni yaleyale, na mimi kweli nilijaribu kuingia katika zote, kuanzia TBC, Wizara, Taasisi na n.k. Jibu nililopata ni KWELI, hata wenye blog kama kina Michuzis, Chahali na Mjengwa wamewapiga bao kishenzi wale wasomi waliotengeneza hizo websites za serikali, tena yawezekana kwa gharama kiduchu kabisa..
Ilionisikitisha hasa ni ya TBC, yaani ni ya kitoto kabisa, kama vile imeandikwa na vijana wanaoanza kujifunza programming!
Hivi sisi waTZ tuna tatizo gani?! Kila sample za websites ziko online, kweli tunashindwa kutengeneza nzuri tu kama za www.bbc.co.uk kweli?
Ebu tuache uvivu na kujigamba twayajuwa mambo tuonyeshe umahiri wetu kuliko uozo huu...
 
Kiongozi, hawa jamaa hawataki kuingia gharama halali kuweka update na modification za web zao. Sanasana wanaajiri 'vitaalam' vya IT ambavyo vina elimu ya elementary tu kwenye masuala hayo. Wanakuwa wavivu au bahiri sana kutoa tenda kwa wabobezi wa mambo ya programming. Idara nyingi za serikali upande wa TEHAMA vitengo vinashikiliwa na vilaza tu, wengine hawana hata elimu ya programming.
 
Vyeti feki?!
 
Kuna kampuni moja hivi jina lake limenitoka ipo town hawa jamaa naona ndio walipewa shavu la kutengeneza tovuti nyingi za taasisi za serikali, kiukweli jamaa katika idea za designing wapo kawaida sanaaa na nadhani ndio madhara ya kujuana unaweza kuta jamaa walipata tender direct bila hata kupambanishwa na kampuni nyingine.
 
Ndio maana web nyingi zinafanana kimuonekano.
 
Eewa, asilimia kubwa ya tovuti nyingi walizotengeneza wao zinafanana sana, sasa sijui client ambao ndio taasisi za serikali waliwaambia zifanane au jamaa walikua out of idea kuwa na new design kwa kila tovuti.
 
Back
Top Bottom