Kwanini Waziri Magufuli amekosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Waziri Magufuli amekosea

Discussion in 'Great Thinkers' started by Geza Ulole, Jan 3, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Kwanini Waziri Magufuli amekosea
  Tunapoongelea utawala wa haki na sheria tunazungumzia ufuataji wa sheria na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa nchi yetu kila siku kwa maana tunajua nchi bila sheria na taratibu ni kama uwendawazimu! Sasa kama serikali yenyewe kupitia wizara ya Ujenzi haifuati utaratibu katika kupandisha nauli yaani inajipandishia bila idhini ya SUMATRA, je pale wauza mafuta wanapokataa kushusha bei za mafuta wanapoamriwa na EWURA tumlaumu nani?

  JK aliwalaumu wauza mafuta kwa kukataa kupunguza baei ya mafuta katika salamu zake za kufunga mwaka, je si muda muafaka pia kuanza kuwalaumu TEMESA pia kujipandishia bei bila ya kufuata taratibu yaani idhini ya EWURA? Au hizi sheria ziko kwa ajili ya wananchi wa kawaida tu? yaani wamiliki binafsi (hapa tunaongelea wa Kitanzania maana hata wale wa kigeni sheria huwapitia kando pitia suala la Songas na upandishaji wa bei ya gesi)!

  Natoa ushauri tuangalie hii tabia ya kutofuata taratibu isije ikafika kiwango cha kutoweza kushikika/kuratibiwa maana tunaona hili ni janga la kitaifa maana mbali ya hii mada hata mavyuoni wakuu wa vyuo hawafuati taratibu na sheria, tunaona wanafuta serikali za wanafunzi kinyume na miongozo ya vyuo inavyosema!

  Vilevile tunaona mikopo wanapewa wasiostahili, mikataba pia inasainishwa kwa watu wasio na uwezo bila kufuata taratibu za utangazaji wa tenda! Hata bungeni napo chombo cha kutunga sheria wanajipandishia mishahara na kujilipa bila ya utaratibu! Mawizarani pia huko mishahara inalipwa kama wanavyojitakia wao (wakubwa) na hata malipo ya kampuni zinazojenga barabara zetu yanafanywa kwa matakwa ya wakuu wanavyojiskia na kusababisha gharama kuongezeka mara dufu maana kuna matozo ya muda wa nyongeza kwa kutozingatia muda wa mkataba uliowekwa!

  Tusisahau TANESCO nao naskia wako mbioni kuongeza umeme kwa 254.6% kwa kila unit ya umeme inayotumika! Sijawahi ona dunia hii gharama zikiongezeka zaidi ya 50% ya gharama halisi iliyopo ilhali mishahara ikibaki kama ilivyo na ongezeko la ukali wa maisha ukiwa juu ya 20%!

  Kwa kifupi hii nchi baada ya kipindi kirefu cha kukosa "check and balance of power" inaelekea katika ile hali ya "failed state" maana kila vigogo (mawaziri na wale woote waliopewa dhamana) wanajiamulia tu kiutashi na matakwa yao na tunasubiri tu pale wananchi watakapochoka na hali halisi iliyopo na kuingia mitaani labda tuliyempa dhamana (kupitia kura) ya kuwaongoza wao (to check them) ataamka na kujua majukumu yake ni nini japokuwa atakuwa amechelewa! Jamani naombeni mtafakari hili...ninawasiwasi huu mwaka machafuko yatatokea maana hii serikali imeshindwa kuja na majawabu ya mambo muhimu kwa wananchi wake! Mungu ibariki Tanzania

  Last edited by Geza Ulole; Today at 17:35.

  MY TAKE
  Moderator naomba usiiondoe hii topic watu wai-discusss

   
 2. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Did you mention Magufuli to call JF attantion?
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  what do u think? the opinion doesn't make a sense to u?
   
 4. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  honestly, sijaiona sababu ya magufuli kuwa head of the topic sir!.. i like ur post but the tittle, no sir!
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Kwa vile hufahamu taratibu za uendeshaji wa serikali! na si lazima utakachopenda wewe nami nipende ila ninakuhakikishia nilichoandika kimepimwa na kina nguvu ya hoja leta hoja tukujibu na uweke ushabiki pembeni!
   
Loading...