katika utafiti wangu nimegundua mambo machache ambayo yanafanywa na wa mama wengi, ambayo hupelekea watoto wengi kumpenda zaidi mama kuliko baba..
1:-wazazi wengi wa kike wamekua na silika ya kufanya kila kitu kwa mtoto kwa kuwaonyesha watoto zao kuwa wana huruma ya kumjali sana mtoto kuliko mzazi wa kiume, eg utasikia mtoto anaambiwa pale anapokosea "kama baba yako angekuwepo hapa leo ungepigwa sana".
2:-Wanaume wengi tumejisahau sana kutimiza wajibu wetu kama baba, yaani tumesahau kuzungumza na watoto wetu kwa kujifanya tupo serious na kazi sana, mwisho hata linapokuja suala la mtoto kuhitaji mahitaji yake kama ada,nguo, na mahitaji mengine kwa ujumla mama ndiye atakae onekana katoa pesa hata kama zimetoka kwa mwanaume, hali hii huwajengea dhana watoto kuwa kumbe baba hatujari ila kwa juhudi za mama ndo maana tunapata mahitaji, wa mama nao pasipo haya husema " baba yenu yupo busy na wanawake wala hana time na familia, nishukuruni mimi mama yenu nisingekuwa mimi hata sijui mngekuwa wageni wa nani.
3:-Wanawake wengi wamekuwa kama mwiba kufitinisha kati ya watoto na BABA zao, eg unakuta wazazi wa kike aliachana na mumewe kwa fumanizi, lakini atakopo ulizwa na wanae kwa nini mlitengana na baba, ataanza kujenga hoja za uhasama kwa kudai, baba yenu alikuwa ananitesa, nashinda na kulala siku3 pasipo, kula yeye yupo busy na wanawake zake wakila raha, nilikuwa nampenda sana baba yenu lakini alinifukuza mchana kweupe kama mwizi, yaani namchukia sana baba yenu mimi..
NOTE:Kwa haya machache hivi kuna mtoto gani atakae mpenda baba kuliko mama, wazazi wa kike punguzeni visasi, wanaume tunawapenda sana watoto zetu..
Sent using
Jamii Forums mobile app