kwenye kujenga nchi lazima tuambiane ukweli siyo porojo! nashindwa kuelewa propaganda zitaisha lini, hatari sana chama kutumia umaarufu wa mgombea kuhadaa wananchi, kwanza sera zinazouzika, mchezo wa kitoto sana huu kutembelea umaarufu wa mgombea huku chama kikibaki dhoofu bin hali! kwanza kwa faida ya watanzania wanapaswa kuelewa utendaji, utii na utumwa ni mafiga matatu ya udhaifu wa kufikiri! kiongozi wa nchi anatakiwa awe mbunifu, mtendaji na mwenye uwezo wa kuhoji, kusifia utendaji maana yake kutukuza wanaomtuma hata kama wachafu, kwenye chama kilichojaza wahafidhina sipati picha atatumwa na wananchi au wahafidhina wanaoamini watatawala milele? NAWAZA TU KWA SAUTI.