Kwanini watu wanaojifanya wana dini wanapenda sana kuhukumu?

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Aug 22, 2014
516
903
Kuna hawa watu wanajifanya wana imani fulani haijalishi muislam au mkristo, kwanini mnapenda sana kuhukumu watu?

Hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani mtu anakuona unakula anaanza kuleta stori zake ooh utaenda motoni kuchomwa moto mara ooh Mungu hapendi utalaaniwa.

Kwanini mnapenda kuhukumu watu? kufunga kwa mtu we inakuhusu nini? we ndo unaandika dhambi za mtu?

Tuheshimiane jamani, mwisho wa siku kila mtu atalipwa kwa anachofanya yeye kama yeye si mtu mwingine anafanya nini! halafu unajuaje fulani ni mtu wa imani fulani kwa kuangalia jina?

Wengine wana majina ya kiislam na kikristo lakini wapagani. Kama umeamua kuabudu Mungu wako abudu wewe kama wewe si kuhukumu watu wengine, hilo jukumu si lako!!
 
je wajua maana ya kuhumu?
mfano mtu ameshuhudia unaiba, una kamchepuko halafu anakwambia ukweli kuwa acha hiyo ni dhambi haifai. hajakuhumu. ila akisema wewe ni mzinzi ama mwizi hutaenda mbinguni!! kahukumu.
Biblia inasema waambie wana wa yakobo makosa yao na wana israel Dhambi zao. Upo hapo?
 
Hakuna mwana wa Israel wala yakobo hapa tz, tumejaa akina Mwakalindile, Msuya, Lema, Msigwa...
 
Mkuu hata kama mkara, mhehehe bado ukifanya kosa wapaswa kuambiwa ama ukitenda dhambi basi uambiwe sio kufunuka funuka. ila sio kuhukumu!!
 
Mkuu natamani ningekua nakuona unampa hayo makavu kuna jamaa niko nae ofcn ndo michezo yake hyo mpk anakua kero yani
 
Ni nasaha tu mkuu kwasababu wakuambiwa ni binadamu tunaotenda dhambi ukimwambia mbuzi hafanyi kitu so tuvumiliane
 
je wajua maana ya kuhumu?
mfano mtu ameshuhudia unaiba, una kamchepuko halafu anakwambia ukweli kuwa acha hiyo ni dhambi haifai. hajakuhumu. ila akisema wewe ni mzinzi ama mwizi hutaenda mbinguni!! kahukumu.
Biblia inasema waambie wana wa yakobo makosa yao na wana israel Dhambi zao. Upo hapo?

"Kuhumu" hata mimi siijui ni nini
 
Mkuu hata kama mkara, mhehehe bado ukifanya kosa wapaswa kuambiwa ama ukitenda dhambi basi uambiwe sio kufunuka funuka. ila sio kuhukumu!!
Kuambiwa sawa...ila usilete habari za akina Yakobo mara Israel mkuu...hizi hadithi hazituhusu kabisa...zaidi tu ni kiherehere chetu na kujikomba kwa waarabu na wayahudi na mizimu yao.
 
Hakuna mwana wa Israel wala yakobo hapa tz, tumejaa akina Mwakalindile, Msuya, Lema, Msigwa...
Ahahahaaaaaa....umenifurahisha sana mkuu.
Ni ujinga sana kuleta hadithi za wayahudi na waarabu kuja kutuonyea huku kwetu Makwale,Sitimbi,Ngarananyuki,Kilolo,Mlalakua...etc
 
Walokole na wavaa visuruali vifupi ndio wanaoharibu dunia hii ya sasa....I,e ni zaidi ya janga.
 
hukumu kipimo sio binadamu kwa hukumu yoyote (kama ipo)standard ya hukumu ni sheria kama kuna sheria halali imekiukwa kwa namna yoyote ile inampasa mtu huku ielweke vyema Mungu ndie Mhukumu mkuu wa Watu wake aliwaumba yeye na anajua mapungufu yao Tatizo!
kumhukumu mtu kwa mtazamo wa mtoa mada ni kule kumsema mtu kwa uasi ambao yeye(mtoa hukumu)hana viwango vya ukamilifu ule ambao yeye mwenyewe hata akiwa nao hapaswi kujiinua bali ajione kuwa hafai siku kwa siku ndio msingi wa ukamilifu wa kiimani
''Watu wa Mungu wanawezwa na Mungu mwenyewe''alinifundisha mama yangu.
 
Ni kawaida kwa binadamu kutotaka kukosolewa mfano mzuri ni JPM

Mkosolewaji huleta swaga kama zako(Mara oohh kila mtu na kaburi lake, Baki nayo hayanihusu, wewe ni nani wa kuhukumu,n.k) yote hiyo ni kudivert from the main course na UKWELI DAIMA MCHUNGU ILA NDIO DAWA
 
Back
Top Bottom