Bandugu, tumeshuhudia mwizi akiuawa na wananchi wenye hasira pale Mwananyamala leo. nataka kuuliza watendaji wa LHRC, je
1) mwizi huyu ambaye ni marehemu hana haki ya kusikilizwa ?
2) nini tofauti ya haki kati ya mtu huyu na yule ambae ameiba fedha za umma /fisadi ambaye anatumbuliwa jipu hadharani?
3) kwa nini vitendo kama hivi vya wananchi. LHRC huwa hawavitolei mmatamko hata kidogo miaka yote lakini lakini anayeiba fedha za umma akitumbuliwa tu jamaa hawa wanakimbia haraka na kutoa matamko ya kutahadharisha ?
4) tukisema LHRC huwa wanawatumikia wale ambao wanafaida au interest nao ambao labda huwafadhili kinamna tutakuwa tumekosea ?
5) kama jamaa hawa wanatumikia watu fulani fulani kwa maslahi binafsi kuna haja gani chombo hiki kuwepo nchini mwetu? kwa sababu wananchi tumeshapata wasiwasi nao na tumeondokewa na imani kabisa nao. hatuwahitaji katika maendeleo ya nchi yetu na hasa katika kipindi hiki.
6) kama basi kuua mwizi hadharani inaruhusiwa kulingana na muono na sheria zao kwa nini basi wasiruhusu kwa sheria hizohizo zikatumika katika kuwashughulikia mafisadi hadharani na kuwatumbua ?
tupeni mwongozo wajameni