Kwanini watu tunakuwa wazito kutoa taarifa Polisi?

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,901
Reaction score
14,611
Viashiria vya uhalifu vinaonekana hata wahalifu tunawajua mienendo na mipango yao.

Lakini mpaka litokee tukio, ndio utasikia..aaah wewe ulikuwa hujui?

Hivi hili jambo huwa linasababishwa na nini?

Zamani haikuwa hivi.

Hata mgeni akiingia mtaani/ Kijijini, watu wote Kijijini/ Mtaani tulifahamu mpaka watoto wadogo walifahamu.
Siku hizi jina la mpangaji mwenzako hata hulijui,achilia mbali majirani wanaokuzunguka.

( Kuna haja ya kurudisha utartibu wa zamani)
 
viashiria vya uhalifu vinaonekana hata wahalifu tunawajua mienendo na mipango yao.
....lakini mpaka litokee tukio,ndio utasikia..aaah wewe ulikuwa hujui?
Hivi hili jambo huwa linasababishwa na nini?
Zamani haikuwa hivi.
Hata mgeni akiingia mtaani/kijijini,watu wote kijijini/mtaani tulifahamu mpaka watoto wadogo walifahamu.
Siku hizi jina la mpangaji mwenzako hata hulijui,achilia mbali majirani wanaokuzunguka.(kuna haja ya kurudisha utartibu wa zamani)

1. Polisi wetu ukiwapa taarifa wataanza na wewe.... Yaani they treat you kama suspect na unaweza ukafungwa...
2. Polisi wetu wengine wanashirikiana na na wafanya matukio... Hivyo ukijifanya unatoa taarifa polisi wanatoa siri na utawindwa mitaani
3. Polisi wetu wanadhani the only way ya kupata info toka kwa mtu ni mateso makali... Sasa katika hali ya kawaida hakuna anayetaka kuteswa.. Mbaya zaidi wanaweza wakamtesa hadi mleta taarifa
 
hakika umenena vema sana. Sioni cha kuongeza, wacha wapigwe tu.
 
Kama polisi wenyewe tunawapa taarifa za uhalifu na baadae wanarudi kwa waandishi na kufanya clean up kwa mhalifu, sidhani kama kuna ulazima wa kuwapa ushirikiano!
 
Mwakyembe alishawahi sema ... JESHI LA POLISI TANZANIA NDIYO JESHI PEKEE DUNIANI LINALOSUBIRIA KULETEWA TAARIFA....
 
1. Polisi wetu ukiwapa taarifa wataanza na wewe.... Yaani they treat you kama suspect na unaweza ukafungwa...
2. Polisi wetu wengine wanashirikiana na na wafanya matukio... Hivyo ukijifanya unatoa taarifa polisi wanatoa siri na utawindwa mitaani
3. Polisi wetu wanadhani the only way ya kupata info toka kwa mtu ni mateso makali... Sasa katika hali ya kawaida hakuna anayetaka kuteswa.. Mbaya zaidi wanaweza wakamtesa hadi mleta taarifa

4. Imani ya wananchi dhidi ya porisi imekufa
 
Polisi wapo tayari kuua wapinzani kwa kuilinda CCM.
Wamejijengea uadui na wananchi kiasi kwamba hakuna mwananchi alie tayari kutoa ushirikiano na jeshi la polisi.
 
5. Polisi wazito kurespond kwenye matukia pindi wapewapo taarifa
6. Utawasikia gari halina mafuta
7. Lazima utoe hela ili taarifa yako ipewe uzito
8. Kuna hawa wanawaita wapelelezi yaani ni ishu kubwa hawa jamaa
9. Polisi wanaweka maslahi mbele kwenye kuifanyia kazi taarifa waliyopewa
10. Usipokuwa sehemu ya familia ya polisi au unajuwa na BOSS wao taarifa yako haitafanyiwa kazi
 
Polisi wenyewe sio professional kabisa, ukipeleka ripoti wanaanza na wewe.
wengi wao wanawaza rushwa tu.
NO PROFESHIONALISM KABISA
BURE KABISA
 
1. Polisi wetu ukiwapa taarifa wataanza na wewe.... Yaani they treat you kama suspect na unaweza ukafungwa...
2. Polisi wetu wengine wanashirikiana na na wafanya matukio... Hivyo ukijifanya unatoa taarifa polisi wanatoa siri na utawindwa mitaani
3. Polisi wetu wanadhani the only way ya kupata info toka kwa mtu ni mateso makali... Sasa katika hali ya kawaida hakuna anayetaka kuteswa.. Mbaya zaidi wanaweza wakamtesa hadi mleta taarifa

Thread Closed Umemaliza Kila Kitu.
 
sawiamkuu! polisi wetu wamefanya juhudi kubwa tuwaone kuwa ni maadui hatupaswi kushirikiana nao kwa njia yeyote ile!maana yao ya luisaidia polisi imeacha kumbukumbu mbaya kwa raia wema wengi tu!
 
Polisi wapo tayari kuua wapinzani kwa kuilinda CCM.
Wamejijengea uadui na wananchi kiasi kwamba hakuna mwananchi alie tayari kutoa ushirikiano na jeshi la polisi.
Ukiona raia wanachoma vituo vya polisi (Bunju) unapata picha kamili ya mahusiano ya polisi na raia. Lakini sidhani kama kuna polisi analiona hili. wao wanajua mtuhumiwa ni mtaji wa bia. Mdogo wangu alillalamikiwa na jirani kwamba alitaka kuwapiga watoto wa jirani, lakini hakuwagusa, aliwekwa ndani, eti kumtoa mtu wa malalamiko ya mtaani ambayo yanamalizwa na mjumbe/familia ni sh elfu kumi. Hili ni jeshi shenzi.
 
Ukiwa una lengo sahihi ya kuwasaidia.. kwa mfano usifanye hivi fanya vile ili kujaribu kuzuia uhalifu, watakujibu usitufundishe kazi tunajua tunachokifanya
 
Daladala ilinichomekea nikamgonga kwa nyuma, polisi mmoja alichukua leseni yangu wakati tunaendelea kuelewana na konda. tulielewana vizr ila leseni yangu na funguo waligoma navyo hadi nikatoa hela ya bia.

NIKIKUMBUKA UTENDAJI WAO HAWA WATU. NASHINDWA NISEMEJE. JAPO SIKUBALIANI NA WALIVYOFANYIWA NA WALE MAGAIDI KULE SITAKI PROBLEM
 
Coz ni kutokana na hofu natumaini ya kuendelea kuishi na ukifanya tasmini wabongo wengi twayapenda maisha yetu hata kama uwakika kula kesho hatuna
 
1. Polisi wetu ukiwapa taarifa wataanza na wewe.... Yaani they treat you kama suspect na unaweza ukafungwa...
2. Polisi wetu wengine wanashirikiana na na wafanya matukio... Hivyo ukijifanya unatoa taarifa polisi wanatoa siri na utawindwa mitaani
3. Polisi wetu wanadhani the only way ya kupata info toka kwa mtu ni mateso makali... Sasa katika hali ya kawaida hakuna anayetaka kuteswa.. Mbaya zaidi wanaweza wakamtesa hadi mleta taarifa
Hyo number mbili ndo usiseme ndo zao wanawajua wahalifu na hawawashughulikii kabisa, mana kuna wahalifu wanasema si tunajuana na mapolisi kabisa. Na ukitoa taarifa si ajabu wa kutaje mpeleka taarifa.
Rushwa ukipeleka tatizo Mpaka uwahonge afisa upelelezi ndo wafatilie hasa kituo cha mabatini wanaongoza kwa rushwa na kuwajua wahalifu. Labda haya matukio yatawa amsha usingizini.
Mwenyewe hata nione nini siwezi Ku report police.
 
Daladala ilinichomekea nikamgonga kwa nyuma, polisi mmoja alichukua leseni yangu wakati tunaendelea kuelewana na konda. tulielewana vizr ila leseni yangu na funguo waligoma navyo hadi nikatoa hela ya bia.

NIKIKUMBUKA UTENDAJI WAO HAWA WATU. NASHINDWA NISEMEJE. JAPO SIKUBALIANI NA WALIVYOFANYIWA NA WALE MAGAIDI KULE SITAKI PROBLEM
Uonevu wao wa kijinga ndo sababu iliyo wawekea uadui. Tena hawa mapolisi wa pikipiki ni waonevu balaa wakikukuta na gari lazma wakutaftie kosa au waku force kutoa hela.
Inabidi wabadilike bila hvo wataendelea kuumia tu.
 
Back
Top Bottom