Kwanini Watazania ni masikini?

nombo toby

Member
Aug 9, 2016
47
41
Inaonekana kuwa takribani miaka kadhaa inayofika hapo mbeleni watanzania wengi watakuwa kwenye dimbwi la umasikini na hata kukosa direction ya maisha yao.

Elimu inayotolewa Tanzania humfanya mtu atumie muda mwingi kusoma mambo mengi ambayo haendi kutumia baada ya kuhitimu ngazi aliyopo.
Watanzania wamejikuta wakisoma miaka na miaka ili kusudi apate makaratasi(vyeti), makaratasi ambayo hayatoi mafanikio katika maisha yake.

Hivi hakuna maisha bila ajira za serikari au watu binafsi? Matajiri wengi wamesoma chuo kikuu? Hivi umewahi ona tajiri ameajiriwa? Umewahi ona Nesi tajiri? Umewahi ona Askari tajiri? Umewahi ona Mwalimu tajiri?

Sasa kwa nini unasoma bila malengo? Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2019 watanzania wengi watakuwa wanaishi na makaratas (vyeti) wakitafuta kazi badala ya kutafuta pesa.

NB. Tutafute maarifa tusitafute makaratasi.
 
Kila mtu akijiajiri mwenyewe wafanyakazi watatoka wapi? Acha hzo weye siye wajasiria tutapata wapi cheap labor:):),

Kwanza unatakiwa kufahamu tu kuwa duniani hatukaa tufanane, dunia yote vitu vimeumbwa viwili viwili, dume na jike, mchana na usiku,

Waajiri na waajiriwa, matajiri na maskini, mbinguni na jehanamu,, huwezi kubadili iwe moja ni ngumu..
 
Sababu kubwa tunategemea sana kuajiriwa nasio kujiajiri.
Hatuna uthubutu na tamaa ya kutimiza tunachoamini.
Hatupo tayari kufanyakazi zinazoonekana si za hadhi yetu hatakama kazi hizo zinalipa,kifupi tunachagua kazi.
Support ya serikali nayo ni changamoto nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom