Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,970
- 146,266
Kwanza kabisa si muhimu kukumbuka kila kitu ulichosoma. Kuna mambo mengi yanaandikwa kuchombeza narrative, unatakiwa kujua kipi ni muhimu hutakiwi kusahau, na kipi si muhimu unaweza kusahau bila kupoteza maana ya kitabu. Ikibidi hata kwa kuandika points muhimu.I am inspired!
Mkuu! Binafsi ni mpenzi sana wakusoma vitabu, lakini sometimes napata shida, nasahau some information nilizosoma kwenye kitabu.
Swali langu linakuja, ni kwanamna gani unaweza absorb too much information bila ya kusahau? Je kuna techniques au ni umezaliwa hivyo, au sisi wengine tuna low IQ😁
Mimi napenda si tu kusoma vitabu, bali pia hata kufuatilia mazungumzo ya waandishi wa vitabu kama ya kwenye vipindi vya BBC World Service, C-SPAN, Book TV etc. Ukifuatilia mazungumzo haya utagundua kuwa hata waandishi wenyewe wa vitabu, ingawa wameviandika na ni wataalamu wa subject matter, mara nyingi hawakumbuki kila kitu walichoandika. Kumbukumbu za kiutu haziruhusu kukumbuka hivyo, ingawa kuna watu wanaweza kukumbuka mengi zaidi ya wengine, possibly kwa sababu wame specialize kwenye kitu fulani. Ni rahisi kwa profesa wa historia kukumbuka mambo mengi sana kuhusu vitabu vyake vya historia kwa sababu labda kafundisha somo hilo kwa miaka mingi na hata vitabu vyake vinatokana na notes zake za darasani.
Which brings another point, njia moja nzuri ya kukumbuka ni kufundisha, kuhadithia, kuelezea. Mimi nina tabia hiyo sana. Mara nyingi utakuta hata hapa JF huwa naelezea sana mambo ya kwenye vitabu nilivyosoma au documentaries nilizoona, inasaidia kuelimisha wengine lakini pia inanisaidia hata mimi kuweza kuelewa na kukumbuka hilo jambo vizuri, na pengine ninapokuwa naona kuna pengo, narejea kusoma nikumbuke vizuri, kama kitu ni muhimu.
Pia, kwenye mambo ya muhimu ni vizuri kusoma kwa intention, unataka kupata nini kutoka hicho kitabu? Ukisoma hivyo utakuwa unatengeneza uelewa ulio na logical consistency ambao umejiunganisha na mambo mengine.
Mimi napenda sana kusoma vitabu vya marais wa Marekani, nchi ninayoishi sasa. Nimesoma "Truman" cha David McCullough na set ya vitabu vitatu vya Lyndon B Johnson vya Robert Caro. Siwezi kukumbuka kila kitu. Kitabu cha Truman kina kurasa 1120. Vya Robert Caro viko vitatu. Siwezi kukumbuka kila kitu, lakini, leo ukiniambia habari ambayo haipo kabisa katika maisha ya Truman,kwa mfano Truman alikuwa Nazi, au alikuwa ni draft dodger, nitakataa kusema tuupime ushahidi zaidi, kwa sababu habari hiyo haipo katika account ya David McCullough.
Mimi hupenda kuunganisha facts na larger narrative ili kukumbuka, na in fact kuelewa zaidi ya kukumbuka. Ni kama unavyoweza kuelewa hesabu ukaweza kuifanya tena na tena bila kutegemea sana kukumbuka. Ila kukumbuka kila kitu kwenye kitabu cha kurasa 1120 ni vigumu na wala kitabu hakikuandikwa kwa nia hiyo.
Hata mimi pia kuna mengi sikumbuki na pengine sikumbuki hata kuwa sikumbuki mpaka ninapokuwa kwenye maongezi stimulating kuhusu hizo mada, na hapo ndipo najipima na kujua nakumbuka yapi na yapi inabidi kuyarejea.