Kwanini watanzania wanaogopa kupingana na CCM?

Kwanini watanzania wanaogopa kupingana na CCM?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,169
Reaction score
48,451
Halafu ' mkidudeliwa ' na ' kunyalandaliwa ' na ' wanaojulikana ' mnakimbilia ' Kulialia ' na kuomba misaada ili mponyeke.
Hii nukuu ya kunionya mimi toka kwa huyu Mwana JF mwenzetu imenishagaza sana. Imenishangaza kwa kuwa inaonesha kwenye nchi hii kuwa na mawazo tofauti na CCM ni jambo la hatari sana.

Lakini mawazo kama ya huyu mwana JF mwenzetu yako kwa watanzania wengi sana kiasi kwamba yanaleta swali la msingi ni kwa nini watanzania wanahofia kitakachowapata baada ya kuipinga CCM?

Mitaani inasemwa ukiipinga CCM kwenye nyumba yako kunaweza kupitishwa Barabara na nyumba yako kubomolewa, wafanyakazi wa Umma inadaiwa watafukuzwa kazi, kwa wanafunzi wa vyuo wanaambiwa watanyimwa mikopo, kwa wanasiasa wanaambiwa kitawapata kama kilichompata Lissu na mengi mengi sana.

Lakini CCM yenyewe inajinasibu kama ni chama kinacholinda amani na kupenda amani kwa watanzania. Kama CCM ni chama cha kupenda na kulinda amani ni kwa nini watanzania wenzao wanakiona kuwa kinaweza kuwapatliza kama wakipingana nacho?
 
You have to ignore him... Usiwape kiki Mataahira.
 
Poor in

1.Critical thinking

2.Reasoning

3.Dare to act.

Miaka ya akina Samwel Sitta Udsm ilikuwa kitovu cha kuzalisha think tank ya nchi, waliweza kupinga na kutoa kauli km vijana wasomi juu ya mienendo mbalimbali ya Nchi. leo msomi wa chuo cha Udsm hawezi hata kutoa mawazo juu ya yanayoendelea je unafikiri mTz wakaida anaweza???, wanazuoni ndio wamekuwa wapiga vigelegele juu ya mambo ya hovyoo yanayoendele.kipindi cha Kikwete watu km Bashiru ndio walikuwa vinara wakuandaa vuvguvugu la migomo hapo chuon, lkn leo wamezimwa kwasababu amegundua wasomi ndio wanaoweza kumwangamiza.
 
Mkuu si unajua tena kumpinga baba au mama yako unaweza pata laana halaf ukaonekana una jeuri.

Niko lumumba hapa wamesema ni comment hivyo.
 
Ulevi wa itikadi unawasumbua,wanaona usiye Ccm au usiye na chama, huna haki ya kuitwa Mtanzania wala kutoa mawazo yako.Ndo tulikofikia.
 
Kiufupi tu ni kwamba, yanayohubiriwa na hicho chama wakiwa nje basi utambue ni kinyume chake wanapokuwa wamejifungia ndani! Hivyo jamaa yetu Gentamycine yupo sahihi. Hicho chama na watu wake wapo tayari kufanya jambo lolote lile, liwe jema au baya ili tu waendelee kututawala watanzania! whether we like or not!
 
Tunahofia 'watu wasiojulikana'.Tunahofia kunyofolewa kucha zetu na kung'olewa meno bila ya ganzi.
 
Tunahofia 'watu wasiojulikana'.Tunahofia kunyofolewa kucha zetu na kung'olewa meno bila ya ganzi.
 
Na kwa nini kipindi cha uchaguzi bila Wakurugenzi kusimamia uchaguzi sisiyemu inawaogopa wapiga kura?
 
Umeshawahi kumuona shetani ? au kumsikia kama hujawahi nenda ccm utamuona ,heri ukutane na shetani kuliko ccm , ni watu Hagar sana has a hawataki kuachia madaraka nchi hii kwa amani ,katibu wao mkuu msomi aliyekitumikia chama kwa weledi mkubwa alipokuja kuwaambia ukweli kuwa ,chama cha ccm hakina dira ,Sera wala mwelekeo kitu ambacho ni kweli walichomfanyia mungu anajua ,sembuse sisi .Huyo Gentamycine kwa auna ya michango yake atakuwa senior mataga ,ambao hujidai wao ndio wao ,lakini wameruhusu mihimili miwili kuongozwa na bipolar disorder ,sass umahiri wao sijui huko wapi ? ni aibu sana kwa kitengo .
 
Kwani kwenye kupiga kura huwa ni kundi zima au mmoja mmoja?
 
Kwa siye wa Kiembembuzi hapa unamaanisha nini?
Kwanini watanzania (wapinzani) wanaogopa kiupinga CCM? Kichwa cha habari kina hoji watu wakipinge chama tawala (saying NO) hata kama kuna mazuri yanayofanyika.

Nitatoa mfano, watu walipinga Mh. Rais kujenga ukuta wa Mererani, leo hii mauzo ya Tanzanite kwa wachimbaji wadogo wadogo yameongezeka (kwa mwaka mzima) kutoka chini ya kilo 164 (mwaka 2016) mpaka zaidi ya kilo 700 (2018) na mapato kutoka milioni 71 mpaka zaidi ya bilioni moja, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 1400%
 
Back
Top Bottom