Kwanini wasanii wa kiislamu (bongoflavor) hawa-support mfungo wa ramadhani?

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
1,193
828
Habari wanachama wa JF.!!

Katika pitapita yangu ya pages za wasanii wa bongoflavor ambao ni WAISLAMU sijaona angalau post inayohusu kuhukaribisha MFUNGO WA RAMADHANI.

Mfano wa msanii/wasanii
-DIAMOND PLATNUMZ
-ALI KIBA
-JUX

NA WENGINEO WENGI.
KWANINI HIVI AU NDO U-SUPERSTAR?
NAWASILISHA.
 
Habari wanachama wa JF.!!

Katika pitapita yangu ya pages za wasanii wa bongoflavor ambao ni WAISLAMU sijaona angalau post inayohusu kuhukaribisha MFUNGO WA RAMADHANI.

Mfano wa msanii/wasanii
-DIAMOND PLATNUMZ
-ALI KIBA
-JUX

NA WENGINEO WENGI.
KWANINI HIVI AU NDO U-SUPERSTAR?
NAWASILISHA.
Ku post au kutou post hao wasanii ndio kunaufanya huo MFUNGO WA RAMADHANI unaongezeka/kupungua ubora wake ????
 
Kwanza kabisa unatakiwa kufahamu kuwa WAJIBU WA BINADAMU KIDINI si kama unavyochagua watu wa kuwa follow na kutowafollow Jamii forums, bali unatakiwa kufanya kila kilicho chema na kuachana na mabaya..

Sasa kama usanii tu hauruhusiwi kiislamu, kuna haja ya kuuliza unachouliza? Hakuna aliyehalalisha mahusiano yake kwa ndoa, japo ipo wazi wana wapenzi? Sasa huko kupost ndio kutawafanya wawe watakatifu?

Na wewe unaoshabikia mziki wao unatofauti ipi?

Nadhani tungekuwa na hofu ya Mungu, ni vyema tungewaasa waachana na Usanii, wabariki mahusiano yao, na mengine yafuate maana unapofunga bado upo na kimada, unabeef za kisanii za kutosha, unawapotosha watu na nyimbo zako, SIDHANI KAMA MAOMBI YATASIKIKA MTINDO HUU..
 
Habari wanachama wa JF.!!

Katika pitapita yangu ya pages za wasanii wa bongoflavor ambao ni WAISLAMU sijaona angalau post inayohusu kuhukaribisha MFUNGO WA RAMADHANI.

Mfano wa msanii/wasanii
-DIAMOND PLATNUMZ
-ALI KIBA
-JUX

NA WENGINEO WENGI.
KWANINI HIVI AU NDO U-SUPERSTAR?
NAWASILISHA.
Basi mkuu nawatungia mimi Shairi la Mfungo wa RAMADHANI !:-
Ramadhani Inakuja, Viumbe Tuwe Tayari
Bismillahi naanza, salaamu zipokeeni,

Mungu Atatuongoza, Atutoe mashakani,

Azidi Kutuongoza, Atunawiri machoni,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Viumbe tuwe tayari, inakuja Ramadhani,

Tukae tukifikiri, ikija tufanye nini?

Tufanye mengi ya kheri, na tusome Qur-ani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Tusipoteze wakati, kuzurura mitaani,

Au kusoma gazeti, asubuhi na jioni,

Au nyumbani kuketi, kuona televisheni,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Tusibaki kukoroma, kujibwaga vitandani,

Au kwenda kwenye ngoma, mchezo wa mashetani,

Au kwenye masenema, kwenye picha za kigeni,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Mwezi huo mtukufu, tayari upo njiani,

Kula chakula khafifu, acha nafasi tumboni,

Hapana ubadhirifu, Anaupinga Manani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Omba dua omba sana, mwezi huu wa imani,

Fursa kupata tena, hiyo haijulikani,

Leo upo twakuona, kesho upo kaburini,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Kwenda kucheza karata, ni madhambi ikhwani,

Faida hautopata, ni upuuzi kwa yakini,

Mwisho wake ni matata, na ugomvi barazani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Kwenda kufuata mpira, mpaka kule uwanjani,

Jambo hili linakera, zindukeni Waumini,

Wakati unatupora, majuto huja mwishoni,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Tusigombane na watu, kwa matusi hadharani,

Tazama Mtume wetu, ifikapo Ramadhani,

Huwa mpole wa watu, na mwingi wa ihsani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.




Mwezi mmoja sio mwingi, ndugu zangu kumbukeni,

Mema tufanye kwa wingi, iwe akiba mbeleni,

Tarawihi ni msingi, wa mwezi wa Ramadhani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.





Mungu Atupe subira, asitushinde shetani,

Mungu Atupe sitara, akhera na duniani,

Tunaomba maghfira, na ridha za Rahmani,

Inakuja Ramadhani, viumbe tuwe tayari.

 
Ukikumbatia dini lazima ikutoe kwenye dunia na ikutafutie njia ya akhera,muziki na uislamu mbalimbali sasa hata wao wanajua ukweli,karibu wote wao wanaishi na vimada na uislamu haukubali kabisa mambo hayo,
wataushangilia vipi mwezi wa ramadhani wakati mwezi huo unapingana na mambo yao mengi
 
yaani mkuu hilo unalosema wewe wala haliwaongezei, chochote, wote wanavaa vito, micheni, wanazini, yaani kiufupi lifestyle haisapoti uislam japo ni waislamu
 
Ramadhani ni mwezi mtukufu na funga ni ibada inataka mwanadamu ajipinde katika kumtukuza Mungu wake daima sio mwezi umeisha unarudia dhambi inakua sawa mtoto aliepelekwa shule na akamaliza bila kujua kusoma wala kuandika,sasa hawa wadogo zetu mwili kama daftari la mwandiko,wanaishi na mahawara,pombe kila pembe ya chumba,na wanaitamani dunia kuliko pepo unadhani wataacha kirahisi wewe angalia tu watasimama kufanya show ila wameikamia siku ya Eid ili wafanye show zao ndio utagundua funga ni ngumu wanatamani huu mwezi usingekuwepo.
 
Jakaya Mrisho Kikwete watamkumbuka sana kwenye futari la magimbi pale ikulu na chai ya ziwa si mchezo yaani ungekuta hadi sasa hvi wamesha post sana inst!! Sasa hvi akili zimewatoka
 
Back
Top Bottom