Mtanzania Mkenya
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 238
- 387
Kuna madai ya kuwa album haziuziki au hazina biashara nzuri kwa wasanii wa Bongo flava, hivyo imepelekea wengi wao kutegemea shows na biashara zao binafsi.
Mwezi uliopita nchini Kenya, jamaa anayefanya HipHop anayejulikana kama Rabbit a.k.a King Kaka a.k.a Kaka Sungura alibuni mbinu ya kuuza album yake ya "Its The King" kwa kusimama katikati ya jiji la Nairobi na kuuza mwenyewe. Alitumia mitandao ya jamii kuwataarifu mashabiki wake sehemu ya mji atakapopatikana, hivyo mashabiki walijitokeza kum-support. Aliwapa fursa mashabiki wake kupiga nae picha na ku-post katika instagram yake, ku-sign autograph na kuongea nao stori mbili tatu na kuwa close nao.
Amini usiamini, alifanikiwa kuuza nakala 3,149 kwa bei ya Kshs.200. Pesa za nakala hizi kwa bei hiyo ni Kshs.629,800.
Tutumie mfano huu huu wa Rabbit kwa msanii wa Tanzania na pesa za Kitanzania. Nakala 3,149 kwa bei ya Tanzania Tshs.4,000(buku nne). Msanii anapata takriban Tshs.12,596,000.
Kwa msanii wa Tanzania, hii ni fursa na njia nzuri ya kujitengezea kipato. Tengeza album nzuri. Tangaza kwenye mitandao ya kijamii. Wafahamishe mashabiki wako wapi utapatikana kwa mfano Kariakoo, Mbezi, Kimara. Wauzie nakala. Socialize na mashabiki wako kwa kupiga stori mbili tatu, piga nao picha, post kwa instagram account, facebook ili kuvutia wengine, sign autographs wakihitaji. Msanii piga biashara jo wacha kuzubaa.
Kumbuka album zina umuhimu sana kwa msanii. Kwanza inakujengea heshima kama msanii. Pili ni njia nyengine ya kipato tukiweka mbali shows. Tatu inaonesha jinsi gani unavyo-grow kikazi kutoka album moja hadi nyengine. Album inakupa changamoto ya kufanya kazi zijazo kwa ubora zaidi so unakuwa na targets. Kwa hiyo ni kitu muhimu sana kwa msanii.