Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
Mmarekani aitwaye Max de Pree aliwahi kusema, The first responsibility of a leader is to define reality. The last is to say thank you.
Wapinzani nchini Tanzania wamekosa fadhira kwa Rais Kikwete pamoja na kuwasaidia sana katika ukuaji wao kisiasa!
Rais Kikwete baada ya kuingia madarakani na kukuta hali ni mbaya kwa upande wa wapinzani, hakusita kumteua Ismail Jussa wa chama cha wananchi CUF kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuupa upinzani angalau uhai wa kisiasa.
Ikumbukwe kuwa, wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005, Kati ya viti 182 vya Ubunge Tanzania Bara, CCM walishinda viti 175. CHADEMA walipata viti 5, TLP 1 na UDP 1 huku CUF na NCCR-Mageuzi wakiwa hawana hata mbunge mmoja. Kwa lugha nyingine, upinzani bungeni ulikuwa ni kama kutafuta sindano kwenye mchanga wa baharini.
Ni katika utawala wa Rais Kikwete ambapo upinzani umeshika kasi mpaka unahatarisha maisha ya chama kikongwe barani Africa kinachoitwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati wa utawala wa Rais Mkapa, upinzani kwa Tanzania Bara ulikuwa unakufa kila chaguzi kama siyo kila siku. Wakati akiingia madarakani mwaka 1995, Jumla ya kura za wapinzani kwa upande wa ubunge zilikuwa asilimia 41, mwaka 2000 zikapungua na kuwa asilimia 35 na mwaka 2005 zilipungua zaidi na kuwa asilimia 29.
Mwaka 1995, Viti vya upinzani katika Bunge la Jamhuri vinavyotokana na majimbo ya uchaguzi vilikuwa 46 kati ya viti 232, mwaka 2000 vilipungua na kuwa viti 29 kati ya viti 232, na haikuishia hapo, mwaka 2005 vikapungua zaidi na kuwa viti 26 kati ya viti 232.
Kwa upande wa Tanzania bara peke yake, mwaka 1995 wapinzani walipata viti vya ubunge 22 kati ya viti 182, na mwaka 2000 walijikuta wakipata viti 14 kati ya viti 182. Hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2005 ambapo walipata viti 7 kati ya viti 182.
Utendaji wa Rais Kikwete unavifagilia kwa umakini vyama vya upinzani njia ya kuelekea Ikulu bila ya vyama hivyo kuwa na input inayoeleweka achilia mbali kuonekana kama vina nia madhubuti ya kushinda chaguzi za udiwani, ubunge na Urais.
Utendaji wa Rais Kikwete unamfanya awe ni mpinzani ndani ya CCM kutokana na matokeo ya utendaji wake ndiyo maana kuna baadhi ya wanachama wa CCM walishtuka mapema baada ya kung'amua na kutaka kutenganisha kofia ya Mwenyekiti na Rais wa Tanzania.
Kutokana na utendaji wa Rais Kikwete na serikali yake, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 uliwaleta bungeni CHADEMA wakiwa na wabunge 48, CUF 36, NCCR-Mageuzi 3, UDP 1 na TLP 1, Hili ni ongezeko kubwa sana kwa kipindi kifupi.
Kama hiyo haikutosha, Rais Kikwete aliwaongezea wapinzani mbunge mwingine mmoja (James Mbatia) ili wapambane vizuri na CCM!
Kwa sasa wapinzani wako kimya wanasubiri fadhira nyingine ya Rais Kikwete itakayotokana na kumteua mgombea wa Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015 ambaye hachaguliki ili ahakikishe kazi iliyomleta Ikulu anaimaliza!
Rais Kikwete is on 'mission and he is close to pulling it off!
Wahenga walisema, the gratitude of a donkey is kicks.
Wapinzani toeni angalau shukrani kwa Rais Kikwete!