Kwanini wanawake wanaumizwa?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,678
1. Wanasikiliza mioyo na kuacha kusikiliza akili zao. Unaona mabaya yote, ila unachagua kuoverlook because 'unampenda'

2. Hauhakiki kama maneno yake yanafuatana na matendo yake. Kama anasema anakupenda lazima aoneshe kwa matendo kuwa iko hivyo. Usikabidhi Moyo kwa mtu ambaye matendo hayalingani maneno.

3. Unaamini atabadilika, au mbaya zaidi 'nitambadilisha'. Acha nikupe ukweli: "Mwanaume habadiliki tabia kwa ajili ya mwanamke. NEVER. Mwanaume anabadilika kama AKIAMUA mwenywe kubadilika". So hakuna remedy, kama Ana viwango vya chini, don't take him. Kama kubadilika abadilike mwenyewe ndio aje

4. Kuwa na ninachokiita "selection process" isiyobadilika. Unaweza ukaumizwa kila wakati maana staili yako ya kuwachagua ni ile ile. Mpiga gitaa, mcheshi, mwenye degree. Allow the Spirit to intervene your selection process

5. Misamaha feki. Msamaha na kusamehe ni jambo la kiMungu kabisa. Na wakristo inatupasa tusamehe. Ila mtu anakosea kosa lile like kila wakati wewe unasamehe tu. Wakati mwingine msamehe ila muachane. Maana mkishaoana ataendelea
6. Kuwa na matarajio makubwa Sana (expectations). Putting a man on pedestal ni hatari. Mwanaume ni mwanaume. Na ana mapungufu yake

7. Kutokutambua uhusiano umeishaisha muda mrefu. Kama mtu hajielewi mwambie aongee wazi what he wants. Maana wanaume anaweza akakupotezea muda mrefu for nothing.

8. Kupenda ukiwa umefumba macho. Watu wanakwambia, wewe husikii. Wewe hujali. U r in love

9. Kuamini ataachana na yule wa sasa aje kwako. Hapa pana maumivu makubwa Sana

10. Hii naamini ndio sababu kubwa kupita zote: WANAUME/WAKAKA hawahusiani kwa namna inavyopasa na wadada. Unamlead on Dada wa watu for months as if Una lengo kumbe hauna. Sasa hii tabia na nyingine kama hizi zikome kabisaaaaa. Maana kama wanaume wangewapenda kikweli Dada zetu wasingetapata shida kujua namna gani ya kuenenda. Kama lawama mimi najibebesha na kuwabebesha wanaume.
 
Naona Leo umetuamulia mkuu unashusha uzi baada ya uzi. Siti ya mbele nangoja waje tujue kama yana ukweli haya.

Mr Romantic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…